Miradi iliyoachwa na Wakoloni kabla ya uhuru

Miradi iliyoachwa na Wakoloni kabla ya uhuru

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,638
Reaction score
220,410
Ifuatayo ni miradi mikubwa iliyojengwa na wakoloni:-

1. Ujenzi wa Bandari ya DSM
2. Ujenzi wa Bandari ya Tanga
3. Ujenzi wa Bandari ya Mtwara
4. Ujenzi wa uwanja wa ndege wa DSM
5. Ujenzi wa uwanja wa Bandari ya Pemba
6. Ujenzi wa Ikulu ya DSM
7. Ujenzi wa Dsm College (Baadae ikaboreshwa na kuwa UDSM baada ya uhuru)
8. Ujenzi wa Bandari ya Zanzibar
9. Ujenzi wa reli ya kati, Dar-Tabora-Mwanza, Tabora -Kigoma
10. Ujenzi wa mji wa Tanga + Master Plan
11. Ujenzi wa Jiji la DSM + master plan yake
12. Ujenzi wa Bandari ya Mwanza
13. Ujenzi wa bandari ya Bukoba na Musoma
14. Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay
15. Ujenzi wa Bandari ya Ujiji Kigoma
16. Uundaji wa meli ya MV. Liemba (Ziwa Tanganyika)
17. Uunzi wa meli ya MV. Victoria (Ziwa Victoria)

18. Ujenzi wa shule za Sekondari za kale, mfano Mzumbe, Ilboru, Tanga Tech, Moshi Tech, Mazengo, Mtwara Tech, Tabora Boys+Girls, Pugu, Kibaha, Minaki, Bwiru boys & Girls, Msalato, Ifunda, Iyunga, Mkwawa, Nganza, Tosamaganga, Kilakara, nk

19. Ujenzi wa Ikulu ya Z'bar
20. Ujenzi wa majengo mengi ya Wizara za serikali, vituo vya polisi, magereza na Mahakama.
21. Ujenzi wa shule za msingi za serikali na za Seminari
22. Ujenzi wa makanisa, mf. St. Joseph na Azania Front (Posta Dar) na Misikiti kwa upande wa Z'bar
23. Ujenzi wa hospitali kubwa, mf. Muhimbili
24. Ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme mf. Hale + Nyumba ya Mungu.
25. Ujenzi wa vyuo vikuu vya kati, mfano Dar Tech, Arusha Tech, vyuo vya Ualimu, Kilimo, nk
26. Ujenzi wa reli ya Tanga
27. Ujenzi wa gridi ya kwanza ya Taifa ya umeme
28. Uanzishaji wa mashirika ya umma mfano Posta na simu pamoja na Benki yake
29. Ujenzi wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar (Leo Shamba la Bibi)
30. Ujenzi wa vivuko, mfano Kigamboni na Posta jijini Dar
31. Na kadhalika na kadhalika.

Lakini pamoja na yoooote hayo, miradi hiyo yooote, Bado wazee wetu wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, walisimama mbele ya kadamnasi na kuwaambia wananchi kuwa hao watu (wakoloni) hawafai, waondoke watupishe. Na kweli wakapisha rasmi Desemba mwaka 1961.

Sasa mwaka huu 2020, mimi ni nani hata nisimpinge ccm kwenye uchaguzi huu, pale anapotumia miradi ya maendeleo kadhaa iliyojengwa na serikali anayoiongoza, kama kigezo cha yeye kutaka kuchaguliwa tena na kubakia madarakani?

Tafakari...!!!.
 
Basi labda mchague walevi na wazinzi angalau watawafundisha kutembea na wake za watu na wizi kuliko wanaojenga miradi mikubwa, ...
Ustadhati Barbarosa, Hii ndio imani kuu unayoikili msikitini?

Lahaula, Hakika itikadi kali kama hizi na Imani kali zimemponza Mrisho Gambo Arusha, Akiwaaminisha waumini atawapa eneo la wazi

Sasa na wewe ni wale wale, Kama una hasira na upinzani Vaa bomu jitoe muhanga au nenda kwa wenye itikadi wenzako huko Allepo Syria au Baghdad
 
images.jpeg
images (2).jpeg


We utakuwa na mtindio wa ubongo wewe.. hujui walichofanya
 
Ukizicheki kwa makini zinamanufaa kwake sana
 
Sasa mwaka huu 2020, mimi ni nani hata nisimpinge ccm kwenye uchaguzi huu, pale anapotumia miradi ya maendeleo kadhaa iliyojengwa na serikali anayoiongoza, kama kigezo cha yeye kutaka kuchaguliwa tena na kubakia madarakani?

Tafakari...!!!.
Hapana.

Zipo hoja za msingi sana kumkataa Magufuli kuliko kutumia upotoshaji wa namna hii.

Hii inakosa ukomavu wa mawazo kabisa.

Nina hakika 100% huyu sio mkuu 'Sky...'; sijui kwa nini anakubali kuuza jina kwa hoja dhaifu kama hizi.
 
Ni madarasa makubwa mawili tu ndio yaliyojengwa na Wakoloni katika shule ya Ilboru, kanisa la KKKT na majengo mengine yalijengwa na wanawake wa kiarusha/kimasai walioitwa ''Ndoye o' matofali'' mwaka 1904.
 
Back
Top Bottom