Shule za binafsi na ada za kuruka

chobu

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
308
26
Naiomba Wizara ya Elimu ifuatilie hizi shule za binafsi; kwa kweli ni unyonyaji mtupu. Hebu fikirieni jamani mtoto wa shule ya msingi unamlipia 2,800,000/= kwa mwaka. Hapo bado kila term ununue vitu vifuatavyo, ambavyo gharama yake ni mbali na school fees navyo ni;
1. NIDO kubwa - 42,000/=
2. OMO kgm 4 - 20,000/=
3. kuonyoa nywele - 10,000/=

pamoja na vyote hivyo bado watoto wadogo wa chekechea kuanzia miaka mitatu hawapati mlo kamili kabisa. Unapochukua watoto wadogo chini ya miaka mitano katika shule zenu za binafsi, mnatakiwa mjipange sawasawa, sio kufikira pesa tu lakini afya za watoto hamzijali. Mimi naona wakati umefika sasa wa hizi shule kuchunguzwa upya tena kwa ukaribu sana. Wanatoza ada kubwa lakini huduma zenyewe ni mbaya. Ni hatari sana kwa afya za watoto chini ya miaka mitano. La msingi kabisa shule hizi hazina hata maji ya kutosha ya kunywa watoto, inabidi wazazi wawanunulie watoto wao maji ya kunywa. Hivi hamuoni umuhimu wa maji safi ya kunywa mashuleni? Mazingira yenyewe si mazuri hakuna uwanja wa michezo, watoto hawapati hewa safi maana eneo lenyewe dogo na lipo kwenye High Density. Ilikuwa ni nyumba ya kuishi ikageuzwa shule. Hii ni hatari kabisa, na viongozi wahusika wanaangalia tu!
Mfano wa shule: ni HAZINA INTERNATIONA SCHOOL iko magomeni.
 
hizo sisi tunaosomesha sent kayumba gharama hizo hazituhusu sana! msc. ada kwa mwaka ni 1,763,000/= nyie huko shule ya msingi 2,000,000/= poleni sana
 
Supply and demand, supply and demand my friend. Wewe umedemand na wao wamesupply tatizo liko wapi sasa?
 
Bongo tambarale kila kitu shwari tuu. Ada shule ya msingi kubwa kuliko hata mtu anayesoma digrii. Kazi kwelikweli.
 
Mwishowe utasema serikali iingilie kati bei kubwa ya cadillac, BMW, benz au hata bei za simu kama Samsung galaxy, Nokia N8 n.k. Au utasema Ndodi ashushe bei iwe kama ya Babu!!

Hakuna anayekulazimisha kupeleka watoto kwenye shule za bei mbaya. Ni mapesa uliyonayo ndio yamekuruhusu kwenda huko. Sisi wengine watoto wetu wanasoma shule za kawaida za serikali, watoto wanarudi nyumbani tunagombania ukoko wa wali pamoja, baada ya hapo tunafundishana kidogo, na mwisho wa siku watoto wanafaulu mitihani vizuri tu.
 
Back
Top Bottom