miss pablo
JF-Expert Member
- Jul 9, 2018
- 5,414
- 10,970
Mkuu... nimekaa shule za masista na tunakula.kawaida kbs ila hizo operating costs zake hasa chakula nakuambia usiongee. Ni vile shirika lilikua kubwa. Tena siyo miaka hii. Nilikua naaminika sana hivyo mambo mengi nainteract japo sinofficially. Miaka ya early 2000s. Na boarders tulikua tunalipa 2.7mil.Nimetamani sana nikutane nawe Pendo, lakini kwa kina inahitajika mjadala wenye maslahi ya elimu kwa taifa letu. Endelea kutafakari.....
Na tunafahulu. Kumbuka pia hata kama hao wengine wanapata As shule za kawaida lakini exposure haziwezi lingana na kujielezea. Siku hizi watu wengi sana hatujui kujielezea kwa kingereza aisee. Form 1 nilifahulu na nikapangiwa korogwe girls. Na nilienda. Huwez amini nimefika pale kuna watu nao wamekuja form 1 hawajui hata kuandika jina. Sijui wamefahulu vipi. Wa eng med tulikua wachache sana kama 6 hv kati ya wanafunz 250 darasa letu. Wako watoto smart wanajiweza kwa kupambana ila majority hapana aisee na wamedahulu shule kubwa vile imagine. Kwakua elimu ya bure ni hovyo na nilijikuta naenjoy ule uhuru wa ile shule maana si lazima kusoma hakuna matron mpk mwl wa zamu awe mkali afatilie. Wakati huko private yaan kabla ya kengele yaan ushafika eneo husika. Hakika kule nilitoka na li 3 langu la nguvu yote hayo tulikua tunajazwa upepo kwann tutumie gharama kubwa kuendelea private wakat korogwe ni shule kubwa na nzuri sana. Na hata mzazi alipotaka nihamisha anirudishe private maana nilikua naumwa umwa daily niligoma kwasababu nimeshaonja raha ya kuwa free muda wowote hapo shule tofauti na private. Unaona madhara ya ucheap hayo? Na kati ya darasa zima 1 zilipatikana 8 kama sikosei. Baadaye akili zimenijia ndo najilaumu jinsi nilikua mpumbavu. Nikuhakikishie sikua nasoma kbs. Yaan mwl anavyotoka ndo na mm nimefunga daftari wakati private kila siku heka heka mitihani, walim muda wote wapo around. Yaan akili inakua active. Advance nikarudi zangu Baobab. Tuligharamika lkn matunda yalionekana. Nilipangiwa huko ifakara girls. Wana mashamba hukoo yaani unaitwa jina upangiwe mistari wengine wanakujibia hajaja huyo. Tusidanganyane kulima jembe la mkono ndo kujifunza maisha na teknolojia hizi wakati napaswa kuwa darasani muda huo na si kutafuta malengelenge.
Pia kumbuka mashule wana ujenzi daily. Marekebisho ya hapa na pale. Zote hizo ni gharama. Siyo government meza hamna, ukuta umepasuka na hakuna kinachofanyika lakini private huchukua hatua mara moja.
Umeme siku hizi ni gharama vibaya mno. Yaaan gharama zake kubwaa sana sana sana. Watalipiaje gharama? Nakuomba ulipie hiyo gharama mkuu mtoto asome usilalamike. Kama unataka mwanao apate C hayaa. Mtoto anatakiwa apate mazingira tulivu asome.