ministrant
JF-Expert Member
- Jan 17, 2014
- 554
- 1,134
Wakuu kumekuwa na hii changamoto iliyojitokeza hivi karibuni kwa Shule nyingi za Msingi zinazomilikiwa na Watu au Taasisi binafsi kulazimisha wazazi wawalipie watoto wao wakae Boarding kwa kisingizio cha kupata muda wa kutosha wa kujiandaa na Mitihani ya Taifa ya Darasa la Nne na la Saba.
Binafsi sioni tija ya jambo hili kwakuwa kulala shule hakumfanyi mwanafunzi kuwa bora zaidi ni kuwaongezea tu wazazi gharama za maisha zisizo na mantiki yoyote ile.
Pia kulingana na mmomonyoko wa maadili uliokithiri hasa vitendo vya usagaji na ushoga vijana wa rika hili wako hatarini zaidi hivyo wanahitaji ukaribu zaidi na wazazi ili kuratibu malezi na ulinzi wa watoto hawa ukizingatia. Hii ni kwasababu vijana wa rika hili hawana ujasiri wa kujitetea ikitokea aidha walimu, walinzi au wahudumu wengine wa shule za bweni wakiwashawishi kufanya vitendo hivyo na hata kuna uwezekano wa kufanyiana wao kwa wao.
Nitoe wito kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu iingilie kati jambo hili na kizipiga marufuku shule zinazolazimisha jambo hili na badala yake liwe hiyari kwa mzazi kuamua kama anataka mwanae akae Bweni ama la.
Shule hizi zinapatikana zaidi katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.