Shule binafsi kulazimisha darasa la 4&7 kulala bweni

StingRay

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
503
628
Wahusika wa Wizara ya Elimu mnaosimamia Kata, Wilaya, Mikoa na ngazi ya Taifa yaani Waziri, hili suala la shule binafsi za msingi kulazimisha watoto wa darasa la Nne na Saba kulala bweni ni halisi na linafaida kubwa kiwango cha kubadilisha maana halisi ya "Elimu ya Msingi" kuwa la lazima Tanzania??

Yaani mzazi analazimika kulipa fedha karibu mara 2 ya ada ya kawaida ya mwaka, mfano mathalani ada ni 1,500,000/= unalazimika kulipia 2,500,000/= kwa darasa la 4&7 hii imekuwa kawaida tu na wasimamizi wa elimu mnaliona hili. Elimu ya msingi ya Tanzania inakuwa hovyo sana na wasimamizi wanaangalia tu.

Natamani kusikia tamko la hili kama ni halali ama la kutokana na muongozo wa Wizara na sera zake zinazohusu sekta ya elimu.

Walimu na wadau wa elimu mnaliona je na kulima hili?

Nawasilisha.
 
Kama elimu ni gharama, jaribu ujinga uone gharama yake!

Sioni sababu ya kulalamika, maana kilia shule ina policy yake as far haivunji misingi na sheria za nchi! Hakuna sheria inayokataza shule kwamba wanafunzi wasilale bweni iwe darasa la kwanza, la pili au nne na saba kama ulivyosema!

Kwa kuwa lengo lao ni kujaribu kumsimamia mtoto afaulu vizuri sioni kosa lao!

Kama gharama kubwa kwako shule husika hamisha mtoto wako aende shule nyingine! Wanao afford gharama na wanaojua umuhimu wa elimu wataendelea kulipa ada.

Watanzania tunapenda kulialia sana hata vitu vinavyohitaji akili ya kawaida tu kufanyia maamuzi tunatupia serikali lawama!

Jiongeze mpeleke shule siyo size yako mhamishe mtoto au ukiona na huko kwingine ghali, mpeleke mtoto public schools gharama ndogo sawa na bure tu!
 
Maskini huwa hasomeshi mtoto shule ya private ya pesa nyingi. Hamisha mwanao hiyo shule sio Saizi yako katafute za saizi za kipato chako

Hata jambo dogo la kujiongeza tu watanzania ni kulialia tu! Shule kama haimfai mtu si kumwondoa mwanao na kumpeleka sehemu nyingine.

Sioni kama. kuna .sheria inayonyima shule kuwa na bweni, kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi zaidi!
 
Wahusika wa wizara ya elimu mnaosimamia Kata, Wilaya, Mikoa na ngazi ya Taifa yaani Waziri, hili suala la shule binafsi za msingi kulazimisha watoto wa darasa la Nne na Saba kulala bweni ni halisi na linafaida kubwa kiwango cha kubadilisha maana halisi ya "Elimu ya Msingi" kuwa la lazima Tanzania??

Yaani mzazi analazimika kulipa fedha karibu mara 2 ya ada ya kawaida ya mwaka, mfano mathalani ada ni 1,500,000/= unalazimika kulipia 2,500,000/= kwa darasa la 4&7 hii imekuwa kawaida tu na wasimamizi wa elimu mnaliona hili. Elimu ya msingi ya Tanzania inakuwa hovyo sana na wasimamizi wanaangalia tu.

Natamani kusikia tamko la hili kama ni halali ama la kutokana na muongozo wa Wizara na sera zake zinazohusu sekta ya elimu.

Nawasilisha....
Kazana kutafuta hela mkuu
 
Kama elimu ni gharama, jaribu ujinga uone gharama yake!

Sioni sababu ya kulalamika, maana kilia shule ina policy yake as far haivunji misingi na sheria za nchi! Hakuna sheria inayokataza shule kwamba wanafunzi wasilale bweni iwe darasa la kwanza, la pili au nne na saba kama ulivyosema!

Kwa kuwa lengo lao ni kujaribu kumsimamia mtoto afaulu vizuri sioni kosa lao!

Kama gharama kubwa kwako shule husika hamisha mtoto wako aende shule nyingine! Wanao afford gharama na wanaojua umuhimu wa elimu wataendelea kulipa ada.

Watanzania tunapenda kulialia sana hata vitu vinavyohitaji akili ya kawaida tu kufanyia maamuzi tunatupia serikali lawama!

Jiongeze mpeleke shule siyo size yako mhamishe mtoto au ukiona na huko kwingine ghali, mpeleke mtoto public schools gharama ndogo sawa na bure tu!
Okay lakini jaribu tena ku-revisit post yako kwa kuangalia vipengele hivi;
1-"Elimu ya Msingi" kwamba ni lazima aipate
2- Darasa la 4&7
3- Ada kupanda 1,500,000/=>>>>2,500,000/=

But be critical to the argument, from local to global....
 
Tatizo lako kipato chako kidogo

Hiyo shule sio Saizi ya kipato chako Hamisha mwanao mpeleke kwenye Saizi ya kipato chako
 
Sasa YEHODAYA hapo kwenye jina lako hili weka "Wizara ya Elimu" kwamba ndiyo imejibu....
Unaonaje hilo jibu?? Umejibu hoja au kipengele kwenye hoja? Think don't rush....
 
Jamaa ana hoja nzuri sana ila anajibiwa majibu ya kipumbavu
Watu wamevurugwa kila kitu wanaona utani anayejua umuhimu wa malezi ya wazazi kwa mtoto mdogo wa umri huo ameelewa umuhimu wa hii post ,tatizo lililopo nadhani ni kutokana na kwamba mtoa post kagusia suala la gharama za ada na bweni ss tunawaza tu pesa hatuangalii misingi mingine ya maisha kwa mtoto.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom