Shukurani wana jf!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shukurani wana jf!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by goodmother, Oct 16, 2012.

 1. g

  goodmother Senior Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  takribani miezi 2 iliyopita niliingia hapa jamvini kuomba ushauri wenu, nanyi bila hiyana mlinishauri kadiri mlivyoona inafaa nashukuru sana kwni ushauri wenu niliuzingatia na mimi nikachanganya na mawazo yangu, nilikaa na mume wangu tukazungumza tuakakubaliana kutengana kwa muda wa mwezi mmoja ili kupima mienendo yetu ikiwemo yeye kuacha tabia zake, na kuahakikisha kweli watoto wanaosemekana ni wakwake wakapime DNA. alikubali mapendekezo yangu akafanya vile na watoto wameonakana siyo wa kwake!! kwani nilmwomba kama kweli ni wake asiwatelekeze kama alivyokuwa anafanya hapo awali,, mimi sipendi mtoto ateseke kwa kweli na nilipoona mazingira ambayo hao watoto walikuwa wanaishi nilingiwa na huruma na ndiyo sababu ya kumwomba awahudumie kama kweli ni wakwake. amekubali kujirekebisha ikiwemo pia mimi kurekebisa mapungufu ambayo alinieleza niyarekebishe,. NASHUKURUNI SANA KWANI USHAURI WENU NDIYO ULIONIPA UJASIRI WA KUONGEA NAYE KWA UTULIVU NA YEYE KUNIELEWA KULIKO ILVYOKUWA AWALI NILIKUWA NANYAMAZA NA WAKATI MWINGINE KUGOMBANA NA KUSUSA !! NAOMABA MUNGU AWE KWELI AMEJIREKEBISHA. NAZIDISHA SHUKURANI KWENU.
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  utukufu ni kwa bwana my dear!
  kumbe yule dada wa bar alikuwa anamsingizia
  endelea kumuombea mume wako maana ni bwana ametenda
  usichoke kuomba
   
 3. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Mshukuru Mungu kwa kila jambo, kila jambo hutokea ili tujifunze na kujirekebisha,
  ushauri wangu, mshirikiane ktk shida na raha siku zote za maisha yenu, lakini unapaswa pia kumwomba Mungu
  kila siku **b4 yo go to slp and b4 yo go to job** (Maombi ya Familia)...this is nice one i have experienced
   
 4. g

  goodmother Senior Member

  #4
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  nayeye ndivyo alivyoniambia nimshirikishe kwa kila jambo, kwani aliona kama vile simpi umuhimu kwani mambo mengi ambayo hayahusiana na familia yetu yaani mimi na yeye nilikuwa nafanya mwenyewe bila kumshirikisha. nashukuru nimegundua mapungufu na nazidi kumwomba MUNGU. pia yeye ndiye amekuwa kiongozi wa sala kwa familia pindi anapokuwa nyumbani.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  ungekumbushia kidogo ni thread ipi?
  tujikumbushe
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri hata mie sijui kitu gani kinaendelea......
   
 7. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Kwani unatungiwa mtihani?

  Nakuja Masaki leo

   
 9. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Tunakutakia ndoa yenye amani na upendo. Zingatieni na jitahidi sana kutekeleza makubaliano yenu ili msije mkajikuta mnarudi kwenye hali ile ile ya awali.
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Yaliyopita si ndwele..............!!
   
Loading...