Shukrani zangu za dhati kwa wana JF

Shukrani zangu za dhati kwa wana JF

Kokutona, hatujawahi mimi na wewe kumuongelea huyu mwanao. Lakini nimeumia sana sana juu ya hili. Pole. Naogopa kusema nisije nikamkufuru Mungu. Ujasiri wako unanitoa machozi.

Pole tena.
 
Sina maneno mazuri yanayotosha kueleza ninavyoguswa na appreciation hii. Ila tu naomba Mungu wa rehema aendelee kuwapa nguvu. Mungu awabariki sana.
 
KOKUTONA pole sana mama! Mshukuru muumba atoaye na achukuaye. Mungu ana makusudi yake. Muombe yeye daima!
Much love dada and welcome back!
 
Last edited by a moderator:
Wakati mwingine unaweza kuishiwa na maneno kwa kudhani kuwa yale uliyo nayo hayatoshi kuwakilisha kile unachokusudia kukisema lkn hakuna namna tutaendelea kukuambia Pole sana Mpendwa wetu. Sikuamini SMS niliyoipokea toka kwako siku ya jumatatu 25. 03.2013 kwani kwa bahati mbaya nilikuwa mbali na mtandao about a week so sikujua what was going on. Mungu ni wa ajabu sana tumwache aitwe Mungu maana hatuna uwezo wa kuyafahamu makusudio yake na mipango aliyo nayo juu yetu na sababu za kuyafanya yote haya.....

Kinachotupa faraja ni kuona kuwa amekupa nguvu ya kukabiliana na Jaribu kubwa kabisa katika maisha yako na hatimaye umekubali kilichotokea na maisha yanaendelea. La msingi tuendelee kumshukuru kwa kila jambo kama maandiko yanavyotuasa ingawa kiukweli yanapokuja magumu kama yaliyokupata mpendwa wety KOKUTONA inakuwa vigumu! Karibu tena Jukwaani, Maisha ni lazima yaendelee tukitumaini ipo siku nasi tutaungana na mpendwa wetu kwenye heri ya milele.
 
Last edited by a moderator:
kwanini sasa unaimention hujui kwenye notification utaikuta bado..

aisee ni bad news acha tu..
haya mambo mkuu wangu ndetichia yasikilizie na kuyaona kwa watu tu yakikufika acha tu ndio utaona kila kitu kinabana wacha tu wacha tu aiseeee niliumia sana nimejikuta namwangalia sana mwanangu ambaye yeye alifikisha 1yr tr 10/02/2013 yani ni same age nasikitika sana navaa kiatu kuwa ni mimi nimempoteza mtoto wangu yule alivyona mbwembwe na mapenzi ya kweli kwangu nikifika pale nyumbani ananipokea kam mfalme akiniita kwa mbwembwe mwishowe ananiamba mamaaaaa nyonyo haihaihai ,nikipitiliza tu muda wakurudi nyumbani ataanza kulia wee mpka huo muda ntako rudi so ni rafiki aisee hayo mazingira ni magumu kuamini nakuyazoea tushukuru mungu ada yetu ana mjua mungu ndie aliyempa huyu mtoto other wise mhhhhh
 
Once again, pole sana rafiki KOKUTONA......
mara zote kumbuka kuwa Mungu ni Mwema sana kwako.
Karibu tena jamvini
 
Last edited by a moderator:
KOKUTONA, Mungu alikuwa na uwezo wa kutokuliruhusu hili kutokea lakin je kwann ameruhusu hili litokee??

Mungu ni mwema sana na ninaamini furaha yako itazidi zaid siku utakapokuta mwanao kifuani mwa Abraham amelazwa pamoja na malaika, nina amini utafurah sana kwan utasema kwa ujasiri TALANTA NILIYOPEWA NIMEIZALISHA.

Kwasasa mshukuru Mungu, jitie moyo endelea kuomba ujasiri na faraja ya Kimungu huku ukikumbuka kwamba furaha uliyoipata siku ulipomzaa mwanao inatakiwa iwe sawa na shukurani unazotakiwa kumrudishia Mungu siku hii ambayo amemtwaa.

love you too dear.
 
Pole sana KOKUTONA, na pia tunawashukuru wana Jf wa Tanga kwa kumfariji mpendwa wetu. Mungu awabariki sana!
 
Last edited by a moderator:
Ahsante kwa shukran zako mpendwa, nimefurahi sana kukuona tena Jukwaani KOKUTONA. Kwa mara nyingine pole sana dada.
 
Last edited by a moderator:
Amani ya Mungu ikufunike, utapata watoto wengine kwa msaada wa Mungu, mwachie yeye tu atakufariji
 
once again ..pole sana KOKUTONA.. Mungu aendelee kukufariji na kukutia nguvu!
 
Last edited by a moderator:
Mwenyezi Mungu,Muumba Mbingu na nchi+vyote vilivyomo,akupe faraja na nguvu..kwake yy hatutapungukiwa kitu
 
Pole sana,
kwa kuwa Mungu wetu ni mwaminifu sana atakupa tu watoto wengine.
 
Mungu azidi kukutia nguvu..Akupe wana na vitukuu..Akukumbuke kama alivyomkumbuka Ibrahim na Sara na hata Ayubu ambaye alipoteza watoto kumi kwa mpigo lkn Mungu alimjalia tena.
 
Pole Sana, MUNGU atoae Faraja ya kweli akufariji na kukushika ktk kipindi hiki kigumu sana

Pole Sana
 
Amina Mkuu, Mungu ni mwema na atazidi kukuonekania kwa namna yake na kwa wakati wake. Si kwamba kakujua, alijua, si kwamba hakuona, aliona, si kwamba hajui is your first born anajua, sasa kwa nini ameruhusu??? Hili ndio eneo ambalo linataka kuwa na subira na moyo wa shukurani kwake maana ana plan nzuri sana kwako, kumbuka hili kaka:- Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani, wala Si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini .....''
 
Back
Top Bottom