Shukrani zangu za dhati kwa wana JF

Shukrani zangu za dhati kwa wana JF

Kwa jinsi hiki kifo kilivyoniumiza realy sitaki hata kuiona ID yako KOKUTONA rafiki yangu mungu akupe nguvu mimi nisingeweza vumilia kwakweli.karibu sana

kwanini sasa unaimention hujui kwenye notification utaikuta bado..

aisee ni bad news acha tu..
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Kokutona.. Mungu na aendelee kukutia nguvu..!
 
Tumshukuru Mungu kwa kila jambo kwa maana yeye ndiye muweza wa yote.

Pole sana
 
Hakika Mwenyezi Mungu hampi mja wake mtihani ambao hawezi kuushinda.
Naamini huu ni mtihani tuu na kwa nguvu zake naamini utaushinda.
Tupo pamoja sana.
 
The joy of the Lord is our strength... May he give you that joy..stay blessed
 
KOKUTONA, undugu ni kufaana kama hivi. Kurudi kwako kutushukuru kuna maana kubwa sana kuwa pole tulizokupa hazijapotea bure. Asante sana na wewe na pole sana na msiba, Mungu atakusaidia kukuponya na maumivu unayoyapitia

Na nazidi kufarijika zaidi.
 
Kwa jinsi hiki kifo kilivyoniumiza realy sitaki hata kuiona ID yako KOKUTONA rafiki yangu mungu akupe nguvu mimi nisingeweza vumilia kwakweli.karibu sana

Kwa msaada wa Mungu Nivea yote yanawezekana.
 
Last edited by a moderator:
Mpendwa KOKUTONA, narudia tena kusema sina cha kusema zaidi ya kumwombea mtoto wetu apumzike kwa amani. Bahati moja nzuri ni kuwa mtoto huyu amezikimbia tabu na mateso ya dunia iliyojaa uzandiki, dhuluma,fitina, majungu, ukatili, ubabaishaji, wizi na ufisadi na kuelekea mbinguni kuimba na malaika.

Pamoja na kwamba ametutoka duniani na kueleekea kwenye haki, amani na furaha bado haitoshi, kwa akili zetu binadamu kukubali ukweli huu. Inauma sana kushuhudia mtoto asiye na kosa anatangulia mbele ya haki akiyaacha mafisadi, majambazi, mabakaji, mauaji na majangiri yakijivinjari na kupafanya duniani pasiwe sehemu salama ya kuishi.

Pamoja na yote hayo.... Eee Mungu, ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, lakini baba kama imekupendeza, basi mapenzi yako na yatimizwe.

Pole sana KOKUTONA, mapenzi ya Mungu yametimia.
Bwana Ametoa, Bwana ametwaa, mapenzi yake yametimia.

Umeniliza Asprin
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom