Shukrani kwa wana MMU na CC!!

Shukrani kwa wana MMU na CC!!

Napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya wadau wa Tanga, kuwashukuru wana MMU na CC walitutembelea hapa Tanga kuanzia Tarehe 28 hadi 30 Disemba 2012.

Binafsi nilifarijika na ninashukuru sana kupewa nafasi ya upendeleo kuwapokea wageni wote kwa niamba ya wenzangu.

Ila kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa kibinadamu, naomba radhi kwa kushindwa kuwa na wageni wetu kwa muda wote waliokuwepo hapa Ta. Hata hivyo,timu ya ardhini iliweza kujipanga vizuri na kuziba mapengo yote kiasi kwamba mambo yote yalienda kama yalivyopangwa. Kwa hiyo, napenda kuwashukuru wadau wote wa Ta ambao walichukua jukumu la kuwa na wageni wakati waliokuwa nasi...shukrani za pekee kwa Mwanyasi, KOKUTONA, Arabela na wengine wote ambao walitupa support kwa namna moja au nyingine.


Mwisho, nawashukuru wageni wote walitutembelea wakiongozwa na mkuu PakaJimmy, Mama wa nyumba Blaki Womani, kubwa lao Preta, Makamanda wote wa ukweli Filipo, marejesho, Arushaone, Lily Flower (mama wa nyuki wa mashine), Smile, Madame B, watu8 na anonymous member(s)!!

Shukrani pia ziwaendee wadau wote ambao wamekuwa nasi kwa mawasiliano ya kila namna, teacher gfsonwin na LiverpoolFC (ahsante kwa msaada wa kiroho), Mzee wa Rula, sweetlady, charminglady, King'asti, Husninyo, babu Asprini, Kaizer, Mungi, @Mr Rocky, Erickb52....na wengine wote ambao kwa namna moja au nyigine wametuunga mkono. Bila support yenu tungepwaya kwa namna fulani.


Naomba mapungufu yetu yote mtuachie ila mema yote ya Ta muyafikishe kwa wale wanaotamani kuja kupaona Ta....


Mungu awabariki sana na wale ambao wameshapita hatua ya kuishi nyuma ya keyboard tuonane 2013...

Babu DC!!

Great speech Dark City na mume wangu watu8 alilindwa na shosti Madame B nashukuru wamerudi salama
 
Last edited by a moderator:
Nipo Nimejaa tele kama Mdomo na Ndago.
Afu KOKUTONA Me mbona ni binti mtulivu jamani, lakini babu Dark City kanikazania mimi ni mtukutu.
Mwamie mimi nimeokoka tangu Tanga, nampenda sana Yesu.

Ha ha ha haaa, kweli kabisa ulikuwa bonge ya mpole. babu Dark City ana refer kipindi kile ulivyokuwa mdogo, na hajakuona siku nyingi mjukuu wake anadhani uko vile vile

BWANA YESU ASIFIWE Madame B
 
Last edited by a moderator:
Yesu huyu huyu wa Kanisani, au hukuniona Babu Jamaniiiiiiiiiiiii...............!!!!!!!!!!!!!


Haya bwana,

Usinikumbushe mambo ya wale shemeji zangu wanaimba Yesu na Maria X 10 au zaidi wakati wanapiga mechi za ugenini!!

Titaendelea na mjadala kesho.

Lala ukue mtoto.....

Babu DC!!
 
Back
Top Bottom