Shukrani kwa wana MMU na CC!!

Shukrani kwa wana MMU na CC!!

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,252
Reaction score
11,653
Napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya wadau wa Tanga, kuwashukuru wana MMU na CC walitutembelea hapa Tanga kuanzia Tarehe 28 hadi 30 Disemba 2012.

Binafsi nilifarijika na ninashukuru sana kupewa nafasi ya upendeleo kuwapokea wageni wote kwa niamba ya wenzangu.

Ila kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa kibinadamu, naomba radhi kwa kushindwa kuwa na wageni wetu kwa muda wote waliokuwepo hapa Ta. Hata hivyo,timu ya ardhini iliweza kujipanga vizuri na kuziba mapengo yote kiasi kwamba mambo yote yalienda kama yalivyopangwa. Kwa hiyo, napenda kuwashukuru wadau wote wa Ta ambao walichukua jukumu la kuwa na wageni wakati waliokuwa nasi...shukrani za pekee kwa Mwanyasi, KOKUTONA, Arabela, @CHUAKACHARA na wengine wote ambao walitupa support kwa namna moja au nyingine.


Mwisho, nawashukuru wageni wote walitutembelea wakiongozwa na mkuu PakaJimmy, Mama wa nyumba Blaki Womani, kubwa lao Preta, Makamanda wote wa ukweli Filipo, marejesho, Arushaone, Lily Flower (mama wa nyuki wa mashine), Smile, Madame B, watu8 na anonymous member(s)!!

Shukrani pia ziwaendee wadau wote ambao wamekuwa nasi kwa mawasiliano ya kila namna, teacher gfsonwin na LiverpoolFC (ahsante kwa msaada wa kiroho), Mzee wa Rula, sweetlady, charminglady, King'asti, Husninyo, babu Asprini, Kaizer, Mungi, @Mr Rocky, Erickb52....na wengine wote ambao kwa namna moja au nyigine wametuunga mkono. Bila support yenu tungepwaya kwa namna fulani.


Naomba mapungufu yetu yote mtuachie ila mema yote ya Ta muyafikishe kwa wale wanaotamani kuja kupaona Ta....


Mungu awabariki sana na wale ambao wameshapita hatua ya kuishi nyuma ya keyboard tuonane 2013...

Babu DC!!
 
Asante kwa mrejesho huo. Kuweni na amani na matarajio mapya katika mwaka mpya 2013.
 
Makao makuu ya nchi Babu DC....DODOMA


Ngoja wadau wa Ta na A Wings walifanyie kazi kwanza....

Umetuandalia nini??

Hapa Ta,...kuna watu walitaka kufanya experiment kuprove kama kweli maji ya bahari yana chumvi au ni uongo..lol

Na wengine walienda kuhakikisha kama kweli baharini kuna mamba au la!!

CC: Lily Flower, Blaki Womani, PakaJimmy na Filipo...

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Ngoja wadau wa Ta na A Wings walifanyie kazi kwanza....

Umetuandalia nini??

Hapa Ta,...kuna watu walitaka kufanya experiment kuprove kama kweli maji ya bahari yana chumvi au ni uongo..lol

Na wengine walienda kuhakikisha kama kweli baharini kuna mamba au la!!

CC: Lily Flower, Blaki Womani, PakaJimmy na Filipo...

Babu DC!!

huku semi arid region sijui kunapatikana nini,labda wine za zabibu na karanga babu.
 
Last edited by a moderator:
nilisali babu ila tu sikuwa na access na net.


Poa kabisa teacher,

Nilitaka kushangaa kwani nakuaminia...huwezi kuwaacha wanao na wajukuu bila kuwaweka chini ya ulinzi imara wa Jehova!!

Ubarikiwe sana!

Babu DC!!
 
Back
Top Bottom