Shukrani kwa ukaribisho - Anna Tibaijuka

Karibu sana mama yetu hapa jukwaani ..naamini utasaidia kutupa mwanga na mwongozo wa mambo mbalimbali ..Onyegele mawe!
 
Kati ya vitu ambavyo umepiga hatua kubwa kisiasa kwa sasa, ni uamuzi wako wa kujiunga JF kwani hapa naamini ndipo katika Tanzania watu wanashinda muda wote.Hivyo hapa ukiwa na tatizo unataka kusikia au kupata habari kutoka kila kona ya nchi yetu basi utapata bila shida.

Kama ulishauriwa na mtu kujiunga hapa basi aliyekushauri amekupeleka hatua kumi mbele katika safari yako ya kisiasa.Naomba uamini hili ninalikuandikia.Jf kuna watu ambao wana uwezo kukutathmini na kukupa kile unachostahili.Hapa utapata mengi sana.kama unahitaji kujua tabia ya wafanyakazi wa wizara yako basi hapa ndipo umepatia.Hapa watu hawamwogopi mtu kumwanika.Utafaidika sana na jukwaa hili.

Mwisho nakushauri uwe mvumilivu maana hapa ukikosea wana jamvi watakupasua.Ukifanya vizuri hapa watakupa credit.Hivyo majibu utakayokuwa unatoa hakikisha ni ya uhakika.Kama wengine walivyokutahadharisha kuna watu wana data za sauti,video, picha na document.Wataanika hadi utashangaa.

Nakutakia kila la heri.
 
karibu! ila akina JF sasa hivi watakuita wewe ni mwana freemason eti tu kwakuwa umejitokeza katika jamvi na wao hawataki kuamini kama ni wewe kweli au ndoto.
Wana JF wamezoea kujifichajificha na kamwe hawapo tayari kusimamia ukweli wakiwa hadharani jamvini.:shut-mouth:
 
Karibu sana JF mtani wangu Prof. Anna Tibaijuka. Natambua kwamba umeshakaribishwa lakini ni vizuri nami nikitia ubani.

Naamini kupitia JF utatusaidia sana kujua mambo mengi yanayojiri wizarani kwako na pia kupitia JF utajifunza na kutambua kero mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi wanaohitaji huduma wizarani kwako.

Nakuomba uwe muwazi na mwepesi wa kushughulikia mambo yote ya msingi utakayoyakuta hapa kwani wengi tuna imani kubwa na uwezo wako wa kutenda kazi.
 
Last edited by a moderator:
karibu sana mama, katika kukuhoji pia tutajifunza kupitia majibu yako ambayo umesema yatakua evidence based.
 
Kwa hakika inatia moyo kuona watu mahiri na makini wakijitokeza hadharani kwamba ni wapenzi wa Forum hii iliyowahi kjpigwa madongo kama kijiwe cha umbeya.
Kujitokeza kwa ID halisi kutawatia moyo wengi wenye nyadhifa katika jamii na wana JF kufanya hivyo.
Nina uhakika viongozi wengi tu huingia humu akiwamo 'Mkulu' wa Magogoni.
Big up Mama Tibaijuka!
 
Mama Tibaijuka,

Mimi nakupongeza sana kwa kuwa member hapa. Ila niseme kuwa nakuheshimu sana si kwa sababu ya uprofesa na au uwaziri bali nakupongeza kwa ile kazi kubwa uliyofanya ya kuanzisha na kuendesha Baraza la Wanawake Tanzania. Ilikuwa ni kazi tukufu na laiti lingekuwa linafanya kazi hadi sasa Tanzania ingekuwa imebadilika sana. Pale ulionyesha njia na njia sahihi. Kwa hiyo kwa asili wewe ni mwanaharakati na mwanamwapinduzi wa taifa la Tanzania. Kwa hiyo kwa kujiunga na JF naamini kuwa umerudi nyumbani! Na wenzetu wanasema "So welcome back where you belong prof!
 
Mheshimiwa Prof Tibaijuka,

Karibu sana jamvini, hapa ndio barazani kwetu ambapo jiwe huitwa jiwe na tofali huitwa tofali.
Inahitaji mtu mwenye ujasiri wa hali ya juu kama wewe kujiunga hapa kama verified user kwani wengi tunao humu lakini wamejificha kwa kutumia ID kificho ili waweze ku comment na kutoa hoja.

Mfano wako inabidi uigwe na viongozi wengine pia ili kutoa nafasi kwa wananchi wa kawaida kama mimi kuweza kukuliza maswali ya msingi kwa faida ya taifa letu kwa ujumla bila kujali itikadi

Once again karibu sana jamvini, jukwaa ambalo ukipitia threads nyingine unaweza kukwazika lakini najua una ujasiri wa kuvumilia ndio maana umeamua kuingia hapa kama verified user.
 
Karibu sana mama!

Mi napenda kukuuliza Serikali ina mpango gani kuhusu upimaji wa viwanja na miji kwa maeneo yote Tanzania? Halimashauri zote zina maafisa ardhi, Town planners, Land surveyors, Cartographers, Land Valuers lakini suala la kupima na kurasimisha ardhi ili miji yetu ipendeze imekuwa si tatizo tu bali ni kero kubwa. Pindi itokeapo wakipima viwanja vichache, serikali huviuza kwa bei kubwa sana bei ambayo hairandani hata kidogo na kipato cha mtanzania wa kawaida ambao ni wengi.

Pia kuna suala la watumishi wa halimshauri idara ya ardhi kujimilikisha viwanja vingi vingi pindi serikal inapotangaza na kuuza viwanja, na huwa wanauza fomu nyingi kuliko idadi ya viwanja ambapo mimi nadiliki kusema kuwa ni WIZI. Ni wachache sana wanaofanikiwa kupata kwa njia hio na ni viongozi wenye majina makubwa kama Lako mama. Baadae watumishi wale huanza kuviuza viwanja hivo kwa bei kubwa sana ambapo maskini huendelea kuwa maskini kwani haweza kumiliki ardhi kwa utaratibu huo. Swali langu ni kwamba, JE UNALIJUA SUALA HILI? NA UMEJIPANGAJE KULIFANYIA KAZI?

Jambo jingne ni kuhusu jiji la Dar es salaam kwa sasa linapanuka sana na ni kwa kasi ya ajabu, JE kwanini upimaji wa viwanja hauendani na kasi ya ukuwaji wa jiji la Dar es salaam? watu wanajenga kweny maeneo yasio rasmi kwa sabab serikal haijapima viwanja na hata ukiwa na eneo lako ukiomba kupimiwa, mlolongo utakaokutana nao ikiwa ni pamoja na RUSHWA hautatamani kurud tena idara ya Ardhi. Hamuoni ni kero kubwa kila siku watu wanaumwa kipindu pindu na wanaathirika na mafuriko kwa sababu hakuna miundombinu ya maji taka? na miundo mbinu ya maji taka haiwez kuwepo bila eneo husika kurasimishwa.

Nina masuala mengi sana mama yanayonikera lakini kwa leo naomba unijibu hayo tu. Otherwise nakutakia kazi njema mama!
 
Karibu sana Mama hapa jamvini. Amin Amin nakwambaia si mwili na nyama vilivyokuongoza kuona umuhimu wa kujiunga na wanajamvi bali kwa kwa uweza wa roho ya mabadiliko katika kuijenga Tanzania ya kweli ili vizazi vijavyo vifaidi maziwa na asali ya Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar a.k.a Tanzania.
Mungu Mbariki Mama Ana TIbaijuka
Mungu ibariki Tanzania
 
karibu sana mama Tibaijuka..

Mimi naomba ufafanuzi kwa nini hawa wawekezaji tusiwape maeneo ambayo yàpo wazi kwenye nchi yetu wafanye hiyo miradi yao kuliko kuhamisha wananchi ambao tayari wameshaijijengea makazi yao ya kudumu kwa dhiki na pesa za kuunga unga wanatolewa mfano kinachoendeleq kigambani kwa sasa..la serikali kwa nini haina mipango ya muda mrefu kama utengaji wa maeneo kwa ajili y shughuli maalum badl ya kusubiri kuhangisha watu ambo wapo mahali fulani watolewe ili waje wawekezaji mfqno Loliondo..ni lini iwazara naz setikali yenu itawaonea huruma hawa walalahoi
 
Unaona mbali sana Mh. Mama Prof. Anna Tibaijuka.

Wewe ni mwanamapinduzi wa Kweli, ninafahamu ugumu wa kuwa kwenye mfumo kama wa sasa, si kila ndoto uliyonayo inaweza kutimia maramoja. Ila uwepo wako katika mfumo huo unatupa matumaini kuwa mabadiliko hayako mbali, wakati utasema na Mungu akupe afya, uhai na nguvu zaidi ya kufanya mambo unayotaka yatokee ili yatokee na kunufaisha wananchi walio wengi kama ulivyoonyesha katika kipindi kirefu cha sehemu nyingi ulikotumika.

Ninajua ugumu ulionao si kila aliyeko ndani ya CCM anakufurahia, kwani ukweli ni kwamba wewe ni adui wa Wanaojipenda wenyewe na si nchi hii, na ndio maana miaka fulani ulikuwa tishio kwa watawala waliokuwa na nia tata dhidi ya nchi yetu.

Ninajua kuwa bado wapo binadamu wa namna hiyo ambao wamekiharibia sana sifa chama chetu! Ila ndoto yangu ni kuwa Iron Lady kama wewe Mungu atakupa nnafasi ya kufanya kwa uhakika yale hasa uliyoyataka kwa nchi hii, kwa sasa ninadhani bado unashida nyingi ikiwemo wale wenye kulinda maswahi yao kwa nguvu zote. Wakati utasema. Kuwepo kwako kwenye mfumo huu kunanithibitishia nia njema kabisa ya Mh Rais Kikwete kwa nchi yetu.

Mungu akubariki.
 
Tunapoteza muda mwingi kupongeza kwa kitu cha kawaida, au ni kwa sababu tumezoea watawala ambao hawajiamini hata kusema wameamkaje asubuhi mpaka waambiwe na wasaidizi wao? Hatuna tofauti na wabunge wanaotumia muda wote kupongeza na kutoa pole za misiba bungeni.

Swali:
Mama Tibaijuka unaamini kuwa uongozi wa serikali na chama chako vinafanya yale yanayotakiwa kwa ajili ya maisha na maendeleo ya watanzania? Unadhani Tanzania inastahili kuwa hapa ilipo kimaendeleo na huduma za jamii? Nini mchango wako kuhakikisha kuwa vizazi vijavyo vinaikuta nchi yenye mwelekeo?
 
Nini msimamo wako kuhusu upuuzi wa mkuu wa mkoa wa Arusha? Hili jukwaa siyo saluni, shiriki mara kwa mara
 
Karibu sana Prof. Tunaomba pia ukawashawishi na viongozi wengine wajiunge katika jukwaa hili. Wa kwanza ukamshawishi mama Rwakatare. Hakika ujasiri na upeo wako utaongeza maana na umuhimu wa jukwaa letu.
 
Binafsi nmefurahi sana kwa mama kuja jamvini, karibu sana. Kwangu mimi amekuwa Waziri wa kwanza kumwona humu. Lakini pia ameonesha ujacri mkubwa na kufuta dhana ya baadhi ya mawaziri wengine ambao wana mawazo hasi na jamvi hili. Mama karibu na na2maini utaenjoy sana. Hakika wewe ni Prof. KARIBU
 
Naomba Kujua ni Lini Vichochoro vilivyo zibwa na kugeuzwa maduka vitafunguliwa? Hili ni kwa Arusha, inakera sana njia za watu kupita kuguezwa akingi au maduka
 
Karibu Mama,uzoefu wako utatusaidia kufafanulia mambo mengi ambayo tunapotoshwa na wababaishaji.
:israel::israel:
 
Back
Top Bottom