Shukrani kwa ukaribisho - Anna Tibaijuka

Karibu sana na labda mie nikuombe uwashauri na viongozi wenzako kujiunga nasi ili tuweze kwa pamoja kushauriana na kuhojiana kuhusiana na utendaji wetu wa kazi kwa ajili ya kusukuma fikra chanya kwa Taifa letu Tanzania.
 
Karibu saaana mama tiba tunakuheshimu sana tunategemea mabadiliko pasipo kujali itikadi za vyama. Karibu mhe sana
 
Je hati ya viwanja namba 100 na 101 pale block 22 kibada vimefutwa (revoked)? kama ni kweli watu wenye viwanja wasiowafanyakazi wa wizara ya Ardhi haki zao zinakuwaje? Kwanini hati za baadhi ya wafanyakazi wenu wenye viwanja block 22 vimefutwa na kupewa vingine? na nani kawajibishwa kwa kufanya ''double allocation" kwenye mradi wa viwanja '20000'?

Nataraji mod atakusanya threads zenye hoja hii zilizoandikwa hapo kabla.

Nasubiri majibu!
 
Anna Tibaijuka,

Karibu sana mama! Washauri viongozi wengine nao kufanya kama wewe kwani inaweza kusaidia maana masuala yanayohitaji majibu ktk mijadala ni mengi tutapunguza pressure zisizo za lazima!
 
Last edited by a moderator:
Mama nashukuru naomba umlete na Mkama na Makamba maana walikuwa wa kwanza kuishutumu Jf kuwa ni chanzo cha CCm kufanya vibaya na kwamba Jf ni chaka la Chadema.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Anna Tibaijuka,

Kwanza kabisa nakupongeza sana kwa ujasiri uliouonyesha wa kujiunga kama verified user...karibu saana!

SWALI: Kwanini isiwepo maximum limitation ya kiwango cha ardhi ambacho mtu mmoja anachotakiwa kuhold?

Kuna uwezekano mkubwa kuwa miaka michache ijayo Tanzania kutakuwa na uhaba wa ardhi kutokana na ardhi kumilikiwa na watu wachache.
 
Last edited by a moderator:
Nilipokuwa UN tulikuwa tunahimizwa na Katibu Mkuu wetu Kofi Annan kukutana na vijana MTV. Ni utamaduni ambao nimeona unaweza ukatufaa pia Tanzania. Pia kizazi changu tulimshuhudia Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akifika mara kwa mara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuongea na wanafunzi na walimu. Chuo kilikuwa kimoja. Sasa ni vingi. Jamvi linatusaidia kuwafikia kwa pamoja. Wanasema "technology shapes institutions". Tunakwenda na wakati.
kwani siku hizi 'walipiga marufuku' kwenda kutoa miahadhara pale (au vyuo vingine)!
rais wetu (bosi wako) pamoja na kutunukiwa hizo PhD za heshima lakini sina kumbukumbu kumsikia akifika huko kuwapa japo neno. Nakuomba umshawishi naye ajiunge nasi hapa hivyo kupunguza lile pengo la kuhofiana (suspicion) kama yu wamoja na wananchi wake
 
WanaJF

Walionikaribisha – Ninawashukuru. Sikutegemea wala kustahili ukarimu huu. Asanteni sana.

Walioona sistahili
- Ninawapongeza kusema ya moyoni mwao.. Naomba mnikubali kama siyo kwa nafsi yangu, kwa sababu nyie kama mimi ni waumini wa demokrasia ya kweli. Kila mtu awe na haki ya kushiriki katika Jukwaa hili. Hata wa miaka 47 tunaweza tukaleta ya historia ambayo ndiyo hujenga ya kesho. Wenzetu wanasema “ A people with no history have no future”.

Na mbona nimechelewa wengine wamehoji?
Ni kweli. Ila, nadhani ni vyema kutambua kwamba Jukwaa hili, wengi wenu mkiwa vijana, ilibidi lipewe nafasi kukua na kuchanua kabla watu kama mimi hatujaingia na mawazo ambayo labda yangelifanya kusinyaa. Sasa limekomaa, hoja na maswali muhimu yanajitokeza kwa hiyo tunaweza tukajibu inapostahili. Ninawapongeza waanzilishi na Gold Members. Hongereni sana.

Imeulizwa, je nitashiriki mara kwa mara?

Wakati ninaomba ”moderator” anisaidie kukusanya maswali yenu yote yanayohusu kazi yangu, na nitakuwa ninayajibu baada ya kufanya utafiti ili nilete “evidence based reporting” katika jamvi letu, kwa sasa niseme tu katika dunia ya leo, viongozi hatuna budi kuwa kwenye majukwaa ya wananchi hasa vijana, taifa la leo na kesho.

Nilipokuwa UN tulikuwa tunahimizwa na Katibu Mkuu wetu Kofi Annan kukutana na vijana MTV. Ni utamaduni ambao nimeona unaweza ukatufaa pia Tanzania. Pia kizazi changu tulimshuhudia Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akifika mara kwa mara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuongea na wanafunzi na walimu. Chuo kilikuwa kimoja. Sasa ni vingi. Jamvi linatusaidia kuwafikia kwa pamoja. Wanasema “technology shapes institutions”. Tunakwenda na wakati.

Kazi ni nyingi ninaweza kuchelewa kujibu hoja zenu ila kwa msaada wa mode nitajitahidi.

Mbarikiwe. Pamoja tunaijenga Tanzania imara leo na kesho.


Mama Tibaijuka
Nakupongeza sana kujiunga Jamvini ambako najua utaweza pata changamoto zinazo husu wizara yako na Jimbo lako. Swali langu ni je? TOKEA UCHAGULIWE KAMA MBUNGE WA MULEBA KUSINI NI KWA KIWANGO GANI UMETEKELEZA AHADI ZAKO? KAMA WAZIRI WA ARDHI: NINI MSIMAMO WAKO KUHUSU MGOGORO WA MRADI WA UUZWAJI WA VIWANJA KATIKA MANISPAA YA BUKOBA? Katonda akuwe amaani akwongeze Ekisha kyo kwenda abantu bawe.
 
WanaJF

Walioona sistahili - Ninawapongeza kusema ya moyoni mwao.. Naomba mnikubali kama siyo kwa nafsi yangu, kwa sababu nyie kama mimi ni waumini wa demokrasia ya kweli. Kila mtu awe na haki ya kushiriki katika Jukwaa hili. Hata wa miaka 47 tunaweza tukaleta ya historia ambayo ndiyo hujenga ya kesho. Wenzetu wanasema “ A people with no history have no future”.

Usijali mama hivi ndivyo tulivyo cc sisiem tunakabiliana na changamoto wazi wazi, huko cHadema hatumuoni yeyote hapa ila Zitto. Kubwa uwe kama cc kukubali kupokea changamoto bila kupandisha pressure, maana kuna Mi-Chadema humu akili zao kama walianguka kwenye ngazi na kujipigiza kichwa walipokuwa watoto, hamna hamna zero kwa kuongea na kufikiri. lakini pamoja tutaonyesha dhamira ya kweli ya sisiem katika baraza hii uwe mstahamilivu. Si mbali utaona karaha za hawa Ma-Chadema waliotafuta majongoo wakiwa watoto. - Karibu katika kuitangaza sisiem.
 
Karibu sana Prof. Anna Tibaijuka JF, where we dare to speak openly....Unaweza ukafungua mlango kwa wengine pia kuja hapa na kujionea jinsi watu walivyokuwa na uchu...Utakutana na watu mbalimbali hapa mama, wenye kukukwaza na wasiokukwaza lakini chukulia yote ni kazini....Kila la kheri mama
 
Karibu Prof, hakika wewe ni prof wha ukweli, lazima tukubali kwenda na wakati. Karibu sanaaaaaaaa. Kuna Siku nilikusikia kwenye luninga, ukisema maeneo Kama ya mwananyamara, manzese yapimwe, zijengwe nyumba , maduka nk kuliko vijana ambao ndo wazalishaji Kuliko kiuishi bunju, mbali na mjini. Idea Yako mama bado ipo? Na Kama ipo lini itatekelezwa. It was vey nice idea and too professorial
 
asante sana mama Ntibaijuka kwa maneno yako mazuri,ninajivunia utendaji wako uliotukuka kipindi kile ulipokuwa unafanyakazi UN,ulikuwa kweli ni hardworking woman, najua wewe ni mtu sana wa vitendo lakini kwa ushauri wangu sidhani kama utendaji wako uliotukuka utaweza kuendelea nao huko uliko hasa CCM.

Tumeshuhudia watendakazi hodari wengi wakiwa nje ya CCM kweli ni mahodari lakini wakishaingia kwenye hiki chama tu basi anakuwa si yule tena,tatizo haliko kwa baadhin yenu tatizo ni mfumo wa hiko chama alichoingia hakina utamaduni wa kuwafanyia kazi wananchi waliowachagua bali ni kujali matumbo yao tu. Na usije jikuta heshima na imani uliojijengea hasa kwa sisi vijana ikaondoka yoote kwa sababu ya hicho chama unachokiwakilisha(CCM).

Kwa kipindi hiki jaribu kuchukua japo baadhi ya mambo waliokuambia wapinzani usiwe kama wale wenzako ambao kazi yao ni kuwaponda wapinzani kana kwamba hawana jambo zuri walilowashauri yaani wapo kichama zaidi badala ya kutusaidia sisi wananchi matatizo yetu mbalimbali.

Na mwisho mungu akujalie katika utendaji wako wa kazi,hadi sasa wewe ni mmoja wa mawaziri wachache wenye kupendwa na vijanakutokana na kutokuwa na ushabiki wa kichama upo unapigania nchi yako.
 
Naona rundo la maswali lkn jibu hata moja silioni ndio maana nasita kuuliza swali linalonitatiza , au anayakusanya kwanza?
 
Karibu dadangu, tufufue harakati ya Baraza la Wanawake Tanzania. Ilituacha bila dereva.
 
Mama Shikamoo!!!

Kama nilivyokuwa nimeahidi toka mwanzo kuwa hapa JF utapata mengi mimi leo nataka nikupe "Umbea" kwamba kuna Mbunge wangu wa jimbo la Segerea anaishi maeneo ya Segerea Rufita. Nyumba yake amejenga katika eneo la wazi jambo ambalo ni kinyume na taratibu za Wizara maana eneo la wazi ni kwa manufaa ya jamii. Eneo kama lile tayari amekosesha jamii kupata huduma za maendeleo kama vile Shule, Viwanja vya watoto kucheza, Kituo cha Afya nk. Tuma vijana wako wafuatilie nawe utakuwa umejiridhisha kwa haya maneno ninayokwambia, Leo ni siku ya Mama Duniani, NANI KAMA MAMA?
 
Karibu sana mama Anna mimi kama mtanzania wa kawaida nina swali moja tu kwako nalo ni kuhusu Ardhi, Hii serikali yetu ina mpango gani kuhusu kumhakikishia mwananchi wa kawaida uhakika wa pale anapoishi kuwa hatasumbuliwa au kuhamishwa hamishwa bila ridhaa yake kupisha uwekezaji kila mara? Nauliza hivi kutokana na hali ilivyo sasa kila anapokuja mwekezaji hapa nchini mwathirika wa kwanza ni mwanachi wa kawaida kufukuzwa katika ardhi alikozaliwa na kupelekwa sehemu nyingine pasipo ridhaa yake.
 
Back
Top Bottom