Shukrani kwa marafiki

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,767
Reaction score
288,340
Napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Fixed Point, farkhina, Nivea, snowhite, Ablessed, zumbemkuu, Dr measkron, Rocky, KOKUTONA, Heaven on Earth, Arushaone, Chocs, Watu, cacico, amu, Karucee PIC, @Jawilat , Ladyfurahia, 24hrs, Rapherl, watu8, Katavi, Dr MziziMkavu, Matola, asigwa, Kongosho, Judgement, Salary Slip, charminglady, Ngongoseke, Manyanza, Ruttashobolwa, grafani11, Decapitator na wengine wengi hapa jamvini ambao kwa namna moja au nyingine wamechangia sana kupunguza kifungo changu kwa kosa linaloitwa "name calling" ambacho kilianza rasmi November 11, 2013 na kutakiwa kuisha December 10, 2013 8.00am EAT.

Kosa langu ni hili hapa:

You have been banned for the following reason:
We give ZERO Tolerance for Name Calling! Follow Forum Rules [Mohamed Mwaupete AKA Taswira AKA gaidi mwigulu]


Pia napenda kumshukuru mmoja wa wapishi wazuri sana hapa jamvini, muungwana na mstaarabu farkhina. Huyu bidada baada ya kusikia tu nimefungiwa akanipa ruhusa bila masharti ya aina yoyote ile kutumia ID yake wakati wowote ule na pia alinipa password yake na kuniruhusu kuandika chochote kile nitakacho hapa jamvini. Nikamwambia kama nitaamua kuandika kwa kutumia ID yake basi chini nitaweka jina langu, lakini idea ya kutumia ID ya mwanachama mwingine kuandika hapa niliiona ngumu kidogo hivyo nikamwambia nisingependa kumuingiza kwenye matatizo. Akanijibu kama ataingia matatizoni na uongozi wa JF basi hakuna tatizo lolote na kunitaka niwe huru kuitumia ID yake wakati wowote na niandike chochote kile. Ukweli ni kwamba sikuwahi kuitumia ID yake maana akili yangu ilikuwa imegoma kabisa kufanya hivyo. farkhina nakushukuru sana kwa imani ya kiwango cha juu uliyokuwa nayo kwangu, ahsante sana.

Fixed Point yale ya kukufahamisha kuhusu kifungo changu hapa jamvini yalikuwa ni mazungumzo tu baada ya habari 🙂🙂 hukuniambia kwamba utafungua uzi ili kuomba kusitishwa kwa kifungo changu ila nashukuru sana kwa juhudi zako na wengine niliowataja hapo juu na wale ambao sikuwataja kwani badala ya kuchezea wiki nne lupango nimekaa lupango wiki moja tu hivyo kufupishwa kwa kifungo changu kwa wiki tatu, ahsante sanaaaaa.


 
Last edited by a moderator:
Ah pole kwa yaliyokukuta na Karibu tena jamvini...
 
Reactions: BAK
BAK hakika nilisikitika sana ila nimepata furaha kubwa kukuona tena!

Ninategemea uwepo wako usio na kikomo mkuu, jitahidi sana kuwaepuka wajinga ufike safari yako salama.



Welcome on boad once again and please stay safe
 
Last edited by a moderator:
Hahahahaha lol! Hongera zako NN kwa kuweza kumudu kipindi kirefu hivyo bila kibano. Aisee kama kuna mtu aliyebadilika hapa jamvini hakuna kama wewe, maana miaka ya nyuma ulikuwa ukianza kuporomosha matusi dah!!!!! Ulikuwa huishi kula kibano karibu kila wiki lakini siku hizi umepoa kama maji ya mtungini 🙂🙂 Sijui ndio kuzeeka huko? hahahahah. Na zile IDs zako chungu nzima ukifungiwa hii unaibuka na nyingine 🙂🙂 By the way msalimie sana Bwan'Chuchu 🙂🙂

Teh teh teh...wengine bans tushazizoea. Kwanza nashangaa karibu miezi mitatu sasa sijapewa ban.

Naona mods wamezubaa siku hizi.

Ila pole.
 
wakati mwingine mods nao wanakuaga na hila....
 
Reactions: BAK
BAK karibu tena jamvini we missed you brother.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Praise the Lord I am very happy you are back pacha . Kiukweli I was away for sometime and when I came back I was shocked to hear that BAK uko lupango. Nimefurahi mno welcome back brother
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK

Aisee umenifanya nicheke sana. Ama kweli tumetoka mbali.

Kuna mambo huwa nayakumbuka hapa hadi najawa na simanzi ya furaha.

Salamu zako zimefika.
 
Missed u too Dr, thanks a lot for your efforts. I saw some of your contributions kule pasua kichwa, I am impressed and please keep it up.

BAK karibu tena jamvini we missed you brother.
 
BAK, pole sana kwa masahibu. Almost toka nimekuona humu sijawahi kuona umepata ban, japokuwa lile jukwaa la stress huwa linakustress kweli kweli.

Uungwana ni vitendo, pole sana kwa yaliyokukuta ila nashauri usi~quote kosa lililokusababishia adhabu manake hapa niko tempted kulitafsiri maana yake na mie nilitumie.

Haya karibu uwandani.
 
Last edited by a moderator:
Umeona eeh!!!! hahahahaha lol!

Aisee umenifanya nicheke sana. Ama kweli tumetoka mbali.

Kuna mambo huwa nayakumbuka hapa hadi najawa na simanzi ya furaha.

Salamu zako zimefika.
 
Hahaha ila kiukweli you have really changed. Kweli shetani akizeeka anakuwa malaika. Kuna siku nilijiona tukipelekana pwani kwenye thread ya kitambo, nikacheka sana. Usinikondeshee paw wangu tafadhali.
Teh teh teh...wengine bans tushazizoea. Kwanza nashangaa karibu miezi mitatu sasa sijapewa ban.

Naona mods wamezubaa siku hizi.

Ila pole.
 
Hahaha ila kiukweli you have really changed. Kweli shetani akizeeka anakuwa malaika. Kuna siku nilijiona tukipelekana pwani kwenye thread ya kitambo, nikacheka sana. Usinikondeshee paw wangu tafadhali.

Wewe mbona umenikuta nishatulia. Unless labda ulikuwepo 2006, 2007, na 2008 kwa jina jingine.

Lakini kuanzia 2009 na kuendelea me no longer a badass. I have mellowed dramatically.
 
Niliona umepotea nikajua tu labda umebanwa na wanajeshi au umezuka sehemu sehemu kufuatilia mambo muhimu, nashukuru sana Mkuu. Mimi mwenyewe nilikuwa shocked lol! fikiria unataka kuingia huku unakuta umetundikiwa hicho kitanzi kwamba umepewa kibano lol!!! kisa "name calling"

you have been banned for the following reason:
We give ZERO Tolerance for Name Calling! Follow Forum Rules [Mohamed Mwaupete AKA Taswira AKA gaidi mwigulu] Date the ban will be lifted: 10th December 2013, 08:00


basi nikamwambia pacha wako na unamjua na upole wake akaniambia BAK umekosa omba samahani yaishe, sasa mie nikamwambia samahani siombi maana sioni kosa langu lol!!!! acha atake kuangusha mchozi hahahahahah akaanza kunitafsiria sheria za JF ili nilielewe kosa langu utadhani na yeye ni MOD lol!!!! mpaka nikamuonea huruma dah!!!! lakini namshukuru sana yeye na wote waliohusika katika kupunguza kibano changu.


Praise the Lord I am very happy you are back pacha . Kiukweli I was away for sometime and when I came back I was shocked to hear that BAK uko lupango. Nimefurahi mno welcome back brother
 
BAK karibu tena jamvini muungwana wetu.
Happy to see you again
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…