Shukrani kwa Jamii forums.

Wakukaya2

Member
Apr 26, 2023
75
87
Wiki tatu zilizopita, niliandika humu Jamii forums, juu ya kuishauri serikali kufungua mpaka wa Mozambique na Tanzania ( Mto Ruvuma). Ili kuruhusu korosho ya Mozambique kuingia Tanzania, nikaeleza kinaga ubaga sababu ya hoja zangu. Nashukuru wenye mamlaka wamechukua maamuzi, mpaka umefunguliwa, Tena sio kilambo na Mtambaswala, Bali ni Chihanga Newala, ambapo ni eneo sahihi na Karibu hasa na maeneo yanayolimwa korosho. Vijana wengi Leo wanaelekea Mozambique kununua korosho kwa bei poa na kuziketa Tanzania. Ahsante jamiiforums
 
Ulinzi pia uimarishwe. Maana wale jamaa waliojificha eneo la Cabo Delgado huwa hawaoni kazi kuua watu wasio na hatia pale wanapopata nafasi ya kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom