Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,663
- 167,602
- Thread starter
- #21
lazima umpende huwa anasifia zigo lako.
Hatari sana sheikh, mzigo unatikisika kwa mirindimo ya biti la Ice Ice Baby by Vanila Ice
lazima umpende huwa anasifia zigo lako.
Kaka katika uislam kuna waumini wa namna 3.
...
Kwa hio si vyema tukaanza kumkufurisha Sheikh Kipozeo...tumwache atutamanishe na Raha za Peponi...
Mwenyezi Mungu ndie mwenye elimu zaidi..kuliko mimi...
Kuna moja anakwambia "Mito ya Peponi"huyu ustadh hanaga habari na michongo ya kuuaua yeye waga anawazia mizigo minene peponi...hana muda na mambo ya kujilipua..
[h=2]Sifa za mito ya peponi.[/h]Pepo imetengenezwa kwa mabustani mazuri mazuri na mito aina tofauti inayopita mbele yake. Mwenyezi Mungu S.W.T. katuelezea katika Suratil Baqarah aya ya 25, "
]وَبَشِّرْ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الأنْهَارُ[
Maana yake, "Na wabashirie walioamini na kufanya vitendo vizuri, kwamba watapata mabustani yapitayo mito mbele yake."
Mtume S.A.W. alipokuwa katika safari yake ya usiku wa Israa alioneshwa mito hiyo ya Peponi naye akasema. Katika Hadithi iliyopokelewa na Anas bin Maalik R.A.A. kasema, "
''رُفِعَتْ لِي السِدْرَةُ ، فإذا أربعة أنهار : نَهْرَانِ ظَاهِرَانِ ، وَنَهْرَانِ بَاطِنَانِ ، فأما الظَّاهِرَانِ فَالنِّيلُ وَالْفُرَاتُ ، وَأَمَّا الْبَاطِنَانِ : فِي الْجَنَّةِ (سَيْحَانُ وَجَيْحَانُ😉
Maana yake, "Nikapandishiwa juu (mti wa) Mkunazi (katika mbingu ya saba), tahamaki (nikaona) mito minne: mito miwili iliyo dhahiri, na mito miwili iliyofichika. Ama ile iliyo dhahiri ni (mto) Nile na Euphrates. Na ama ile iliyofichika ni mito miwili katika Pepo (Saihaan na Jaihaan)."
Mto mmoja wa Peponi unaitwa Kawthar na ambao Mwenyezi Mungu S.W.T. amemuahidi kumpa Mtume wetu S.A.W. kwa ajili ya kumliwaza baada ya kufiliwa na mtoto wake. Maadui zake walifurahia sana kitendo hiki cha kufiwa mwanawe kwani wao walikuwa wakiona hapana kheri kubwa katika dunia hii kama kuwa na mali na watoto wanaume. Lakini neema za Mwenyezi Mungu hazina kikomo na anampa amtakae. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Surat Kawthar aya ya 1, "
]إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ[
Maana yake, "Hakika tumekupa kheri nyingi." Mtume wetu S.A.W. kwa kuwafahamisha Masahaba zake aliwauliza kwa njia ya maswali kuhusu mto Kawthar katika Hadithi iliyopokelewa na Anas bin Maalik R.A.A. na kutolewa na Muslim, kasema, "
''أتَدْرُونَ مَا الْكَوْثَرُ ؟ قَالُوا : اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ ! قَالَ : هُوَ نَهْرٌ وَعَدَنِيهِ الله عَزَّ وَجَلَّ ، عَلَيْهِ خَيْرٌ كَثِيرٌ''
Maana yake, "Mnajua nini Kawthar?" Wakasema: "Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wajuao!" Akasema (Mtume S.A.W.): "Huo ni mto alioniahidi Mwenyezi Mungu Mtukufu (kunipa) una kheri nyingi."
Mito ya Peponi si mito ya maji peke yake bali pia kuna mito ya vinywaji aina nyingine mbalimbali kama vile: Mito ya maziwa, mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywao, na si kama ule ulevi wa duniani wa kutoa akili na kuumiza kichwa. Na pia kuna mito ya asali iliyosafishwa yenye ladha nzuri kabisa kwa wanywao. Kama alivyotufahamisha Mwenyezi Mungu S.W.T. ndani ya Qur`aani, kasema katika Surat Muhammad aya ya 15, "
]مَثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ فِيهَا أَنْهَارٌ مِنْ مَاءٍ غَيْرِ آسِنٍ وَأَنْهَارٌ مِنْ لَبَنٍ لَمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُ وَأَنْهَارٌ مِنْ خَمْرٍ لَذَّةٍ لِلشَّارِبِينَ وَأَنْهَارٌ مِنْ عَسَلٍ مُصَفًّى…[
Maana yake, "Mfano wa Pepo walioahidiwa wacha Mungu ina mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya ulevi yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa…"
Katika Pepo kuna mto mwingine unaoitwa Baariq ambao uko katika mlango wa Pepo, mto huu ni makhsusi kwa ajili ya watu waliokufa mashahidi na ambao walioko bado katika Barzakh (maisha baada ya kufa), roho zao zitakuwa kwenye mto ule. Kama ilivyoelezewa katika Hadithi iliyopokelewa na Ibn Abbas R.A.A. na iliyotolewa na Ahmad, Tabarani na Haakim, "
''الشُّهَدَاءُ عَلَى بَارِقِ نَهَرٍ بِبَابِ الْجَنَّةِ ، فِي قُبَّةٍ خَضْرَاءَ ، يَخْرُجُ عَلَيْهِمْ رِزْقُهُمْ مِنَ الْجَنَّةِ بُكْرَةً وَعَشِيًّا''
Maana yake, "Mashahidi (watakuwa) kwenye mto wa Baariq katika mlango wa Pepo, katika mnara wa kijani, inatoka riziki zao kutoka Peponi asubuhi na jioni."
Makala haya yametolewa kutoka katika kitabu changu, "Neema za Peponi."
[h=3]Sheik Kipozeo-Peponi kuna Pombe - YouTube[/h]Kuna moja anakwambia "Mito ya Peponi"
Kuna moja anakwambia "Mito ya Peponi"
kumbe huyu ni shehe wa wanawake, pombe na nyama, kama bwana wa kisukuma vile
Hatari sana sheikh, mzigo unatikisika kwa mirindimo ya biti la Ice Ice Baby by Vanila Ice