Mapinduzi ya kilimo hayataletwa na jembe la mkono

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,303
Leo kwenye pitapita zangu mtandaoni nimeona post ya viongozi kugawa majembe ya mkono kwa wakulima huku mkuu wa wilaya akiwataka vijana wakachukue utajiri kwenye kilimo.

Binafsi nimeona hilo tukio ni la kisiasa sana na lingepaswa kufanywa mwaka 1880 kabla ya mkutano wa Berlin. Kwa nyakati hizi halifai. Wakulima makini washavuka kabisa kwenye kutegemea jembe la mkono. Ninashauri serikali iwezeshe wakulima na kuacha siasa kwenye kilimo.

=====

1695803380589.png


Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Ng’waniduhu Malenya amewataka Wananchi hususani Vijana kutokaa vijiweni wakilalamika kuwa hakuna ajira na maisha magumu na badala yake wajiongeze kwa kujishughulisha na kilimo ambacho amesema kinalipa na wapo waliotajirika kupitia kilimo huku akisema Wilaya hiyo imepanga kufanya mapinduzi ya kilimo.

DC Ngollo amesema ili kuwafanya Wananchi washawishike kulima amenunua na kugawa bure majembe 500 kwa Wakazi wa Wilaya hiyo ikiwa pia ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuinua Sekta ya Kilimo nchini.

"Tunataka tufanye mapinduzi ya kilimo, Mh.Rais August 08,2023 alitangaza Mkoa wa Ruvuma kuwa tunaongoza kwa uzalishaji kwahiyo Mkoa wa Ruvuma ni Baba lao kwa uzalishaji wa chakula na Namtumbo tukiwemo”

Malenya ametoa majembe hayo wakati wa Kilele cha Jukwaa la Utambuzi wa Fursa za Kilimo, Biashara na Utalii (Namtumbo Kihenge) lililofanyika Namtumbo na kuhudhuria na Wadau mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo, pia Benki ya NMB ni miongoni mwa Wadau walioshiriki, Wadau wengine ni TFS, TIC, ASA, Nyerere National Park, Mantra Tanzania Rosatom na SONAMCU.

Millard Ayo
 
Teknolojia za vifaa vya kulimia zipo, tatizo ni kuzifanyia matangazo zijulikane kama zipo badala yake wanakaa wanafanya siasa za hadaa umaskini unazidi kuongezeka kwa wananchi wao.
 
Jembe lin apindua pale lilipokata tu lakini sio kuleta mapinduzi ya kilimo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom