Shroud of Turin (sanda aliyovikwa Bwana Yesu inayoonyesha sura yake) ni kweli ilikuwa ya Yesu Kristo?

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,373
SEHEMU YA I

Na Da'Vinci XV



13D137E9-0DD5-4972-85FD-303F49FB428C.jpeg


Naam,

Kesho huko kiama nitaketi nanyi wahenga , mnithibitishie ambayo mlinisimulia kama ni kweli au ni visasili tu au ni stori za Awafu mwenye nguvu kule darasa la Nne.

Mmenisimulia mengi mengi mno, mmenisimulia hadithi za Chief Songea Mbano na Mputa kule Songea walivyopambana na Mkoloni kuitetea ardhi yao. Hamkuishia hapo mkanisimulia hadithi za Adolph Hitler kule Ujerumani na Nazi yake.

~ Mkanisimulia hadithi za Madiba na Soweto yake.
~ Mkanisimulia hadithi za Christopher Columbus na ugunduzi wa bara America.
~ Mkanisimulia Habari za Mzanaki Kambarage Julius na Bibi Titi mohammed na Tanganyika yao.
~ Mkanipa hadithi za mwanasayansi namba moja duniani Leornardo Da'Vinci na Monalisa Wake.
~ Mkanirusha hadi Marekani Mkanipa hekaya za Abraham Licoln, John F Kennedy na Washington yao.
~ Hamkutosheka mkanisimulia hadithi za Charles Darwin na hadithi zake za Nyani na Sokwe Mtu.

E76A59CB-7152-49A9-B9AF-4BDA42D89254.jpeg


Halafu mkatulia mkavuta kiko mkaagiza na kinywaji , kisha mkaturejesha kwenye Imaani na Kila mtu akachagua anachokiamini,na Kwa bahati Sarafu moja ikatupwa chini ikiwa na pande mbili za waumini.

Na karibu waumini sote tumeikimbilia sarafu hiyo yenye pande mbili amabazo ni Wafuasi wa Muhammad mtoto Kiarabu aliyezaliwa na Abdallah bin AbdulMutwalib na Amina Bint Wahab Huko Makka, halafu kuna upande wa mtoto wa Maryam aliezaliwa huko Bethelem Israel.

Halafu stori haikushia hapo na ikaelezwa wototo hawa wote wanatoka kwa baba mmoja kama alivyo yule Babu yao ambaye ni Mume wa Sarai na Hajiri waliowazaa mitume Isaka na Ismael.

Na kwa yakini yangu na nafsi yangu na kupitia nyaraka nlizosoma kuwahusu sikutaka kudiriki kwenda tofauti na Ubongo wangu kuamini ya kwamba huenda wakawa ndio wanaadamu wenye Akili kupita yeyote dunia hii Usinulize kwanini hii ni Yakini na nafsi yangu.


51C07386-4B1B-47B9-9C8E-475E4E172B46.jpeg


Ushawahi kuiskia SHROUD OF TURIN?

A919AD1C-8AA0-4785-9BDB-E774ACAFBB4B.jpeg


Wakati mmoja nliketi nikimsoma, Mtaalamu wangu Leornardo DaVinci halafu nikakutana na makala zinazomuelezea yeye kwa namna ya kumkosoa ya kwamba huenda aliupumbaza ulimwengu kwenye mambo mengi sana likiwemo hili, la Sanda aliyovikwa bwana Inayoonesha Sura yake. How? Karne ya 16 huyu bwana aliwezaje?

Lakini, sawa tunakubali Da Vinci alikuwa mwanadamu mwenye akili sana na Mbobezi wa Kuchora lakini vipimo kadhaa vinaonyesha athari za picha hiyo hazikuwa za kuchora bali ni picha halisi zinazoakisi ya kwamba kuna kiumbe kilivikwa nguo hizo na kama kweli Leornardo DaVinci alifanya ghilba basi alicheza mchezo ambao unabaki kuthibitisha kiumbe huyu alikuwa na akili isiyo kifani.

NB: Huo ni mtazamo tu wa mtu au watu fulani wasiokubaliana na SHROUD ya kwamba ni Sanda aliyovikwa Bwana.

Lakini dunia nzima inaamini nini kuhusu SHROUD hii aliyovikwa Bwana Yesu?

64702FA7-DFC5-4780-9A10-950B7BD3DC68.jpeg


Shourd of Turin, ni miongoni mwa zile bidhaa adimu za kiimani kama ilivyo Holy grail, Shroud of Turin Iliteka vichwa vingi vya habari za huko Marekani na ripoti za dunia kiujumla haswa 80s kwenda 90s na gazeti la Time (1998) liliandika habari zake kwa kina.

Lakini Shourd ilianza kuteka vichwa vya dunia katika miaka ya 80s, ikajiongezea umaarufu kwa sababu ya pande ambazo zilizuka kwenye Ukosoaji kutokana na Ithibati tofauti tofauti na kwa kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo shroud ilivyopata umarufu zaidi kutokana na Tafiti zilizofanyika kwa ajili yake huku watafiti wengi wakitaka vipimo na Utafiti zaidi juu ya hilo.

JE, SHROUD OF TURIN NI NINI?

E8AD8CC2-A137-4D62-A7A1-DDE20F0DB0EB.jpeg


Shourd ni kitambaa au nguo ambayo mtu alitumiwa kukafiniwa (kufunikiwa) na kuzikwa kwacho, au wengine huita sanda a Turin ni mji unaopatikana huko kaskazini magharibi mwa nchi ya Italy.

Sasa hii Shourd of Turin ni Kitambaa (Sanda) iliyopo katika kanisa moja huko Turin Italy ambayo alivikwa Bwana Yesu baada ya Kusulubiwa, na nyaraka tofauti tofauti zinaeleza ya kwamba Kitambaa hiki kimekuwepo nchini Italy huko Turin toka mwaka 1578, The linen cloth is about 14 ft 4 in. long by 3 ft 8 in. wide (437 × 111 cm). Na sanda hii ni nzito mfano wa T-Shirt ya kawaida tu (0.35 mm).

3D277AB8-728A-4408-B5A8-C72B81684D63.jpeg

Watu wengi wanadhani kitambaa hiki kuwa miongoni mwa masalia (Relic) matakatifu sana yaliyobaki kwa sababu nyaraka nyingi za kale kwa muda mrefu zimeeleza kuwa ni nguo pekee ya kweli ambayo alifunikwa Bwana Yesu Kristo na kuzikwa kwayo.

Madai haya yanaipa nguvu sana malighafi hii na kuonekana ni malighafi halisi kutokana na vipimo vilivyoonyesha picha kamili iliyopo kwenye Shrourd, kwamba ni ya mtu ambaye alisulubiwa kama vile Yesu kristo, ambaye amesimuliwa katika Biblia Takatifu agano jipya kwamba alisulubiwa.

JE, SHROUD OF TURIN INAONYESHA IMAGE GANI HASWA?

B5AF59B4-3F83-4B0E-8FEF-5D64824756F1.jpeg



Sanda hii imeonyesha vitu vingi ikiwemo athari na Mabaki ya Moto na mengineyo, kama inavyoelezwa kwenye Makala tofauti hayo sio katika msingi wa mada ya yetu.

Kitu kikubwa tunachokihitaji hapa ni picha ya Ambaye alisulubiwa iliyojitokeza kwenye sanda hiyo, na kukafiniwa na Sanda hiyo.

Picha hii inaonyesha majeraha yaliyopo kwenye kichwa ambayo Inaelezwa yawezekana yalitokana na taji la miiba alilovikwa Bwana wakati wa Kusulubiwa.

Lakini picha hii pia tafiti zinasema inaonyesha alama ya shavu kuvimba, pua iliyopinda kutokana na majeraha na athari za majeraha mengine usoni.

Jeraha lingine ni mfano wa duara (la mkuki) katika ubavu lenye ukubwa sawa na size ya mikuki wa Kirumi lakini katika jeraha hilo pia kuna damu inayonyesha alama za damu inayotiririka kwenda chini.

C0BA4CDA-E0FB-4AC3-99A4-B694B0A397B5.jpeg

Lakini pia, Picha hii inaonyesha majereha ya Misumari ambayo ilipigwa katika, kifundo cha mkono (Wrist) na hii kidogo imekwenda tofauti na Riwaya na hata Movie tulizoonyeshwa ya kwamba Bwana alisulubiwa kupitia Kupigwa misumari kwenye Viganja vyake.

Pia hii inaambatana na damu inayochururuzika kutoka katika Kifundo hicho kutokana na Jeraha hilo la Damu.

5BF36EF6-9C5B-4766-961D-BA1D40C0AEA8.jpeg

Lakini pia picha hii inaonyesha majeraha tofauti tofauti ambayo Msulubiwa aliyapata kutoka na Kunguka na watafiti wakahitimisha , ni dhahirii mengine yalitokana na kuanguka chini zaidi ya mara moja pale alipokuwa anakumbana na kadhia ya Msalaba alioubeba mgongoni mwake.

6A5440D7-53D5-4561-89AF-565A6F043EA4.jpeg

Lakini hata mabegani , picha hizo zilionesha michubuko iliyotokana na kubebwa kwa kitu kizito mfano wa Msalaba.

Pia zinaonyesha alama za mijeledi na alama za misumari kwenye Miguu ya Bwana, lakini wataalamu wanaeleza ya kwamba shape ya miguu katika picha hiyo inaonyesha Rigor mortis(muscle stiffness baada ya kifo) ya kwamba bwana alikufa akiwa bado Msalabani bado.

9150B62A-0461-42CA-A0BC-04C5E0A569CE.jpeg


Lakini zaidi zaidi , katika utafiti Sanda hiyo haina mabaki yoyote kama ya mwili (nyama) wa Bwana.
Picha inayonekana vizuri zaidi katika sehemu zote ni Picha za kichwani.

E6FCCA0B-3888-4110-9E42-86450C2212A4.jpeg


Picha hii ina mtazamo halisi wa mbele wa Mwanaume mwenye pua ndefu, masharubu, ndevu nyingi, na nywele zilizogawanyika katikati ya pande zote mbili za kichwa.

Na picha hii ndio dhana na silaha kubwa Iliyofanya watu wa sasa kutengeneza mtazamo wa Bwana Yesu hivi sasa alifananaje.

610F585E-BE4A-41A2-98CF-E42194257AB8.jpeg


Je, ni kweli picha hii ni ya Bwana Yesu au laah?

HISTORIA YA SHROUD OF TURIN

816A2A25-E66F-4756-BAF5-85323FBA7191.jpeg


Inaelezwa Sanda hii ilikuwepo tangu kusulubiwa kwa Bwana Yesu hadi sasa lakini shroud hii ilipelekwa huko Turin Italia, mwaka wa 1578 na imehifadhiwa katika Kanisa St. John The Baptist huko Turin tangu 1694.

Na imehifadhiwa hapo kwa ajili ya maenesho mamilioni ya watu kutoka pande zote duniani huja kuzuru, kuomba, kujifunza na hata hupiga picha ili kuona na kubaki na kumbukumbu za mtu aliyesulubiwa ambaye wao huamini ni Bwana Yesu Kristo.

B63DC1F9-49B3-4234-9583-F3EF01DDCE9C.jpeg



TAFITI MBALIMBALI KUHUSU SHROUD OF TURIN

Utafiti wa kisayansi kuhusu shroud ulianza mwaka wa 1898 wakati mpiga picha muitalino aitwaye SECONDO PIA , alipochukua picha ya kwanza ya kitambaa hicho.

Na inaelezwa kwamba alitegemea, picha hiyo ingekuwa mbaya kinyume chake picha hiyo ilitokea vyema tu. Na hilo likathibitisha picha hiyo ilikuwa sahihi na si ya kuchorwa, na kadri miongo ilivyozidi kwenda ndivyo watafiti mbalimbali walipoongeza kasi ya utafiti wao juu ya sanda hiyo.

628FF9FA-4468-405B-B48F-114E75FD9E95.jpeg


Watafiti kwa ujumla walihitimisha ya kuwa mwili huo wa mtu aliyesulubiwa alikuwa amefungwa katika shina kama ilivyoonyeshwa katika picha katika kitambaa hicho, na njia pekee iliyotoa majawabu kwa kina ilikuwa ni ule utafiti uliofanywa Mwaka 1978.

9485C6FB-3D66-444A-9CF0-A74CBEBDEC1F.jpeg


Utafiti uliofanywa mwaka 1975 na mwanafizikia kutoka AirForce Academy, ukatoa idhini kwa Vatcan kutoa Ruhusa kwa Watafiti wanasayansi 26 kuja kuchunguza zaidi kuhusu sanda hiyo na katika tafiti ambazo zilifanyika ni pamoja na;

  • Light (up to 1000x) and electronic microscopy Photography , waveleghths tofauti tofauti mbele na nyuma ya kitambaa hicho.
  • UV spectrophotometry of fluorescence and absorption radiography thermal photography.
  • Mass photography.
  • Laser microprobe Raman spectroscopy.

FC1C55E6-C00D-472C-9AEC-A8F23E2B4A3D.jpeg


Mambo mengi yalivumbuliwa lakini uwepo wa protein katika kitambaa hicho ndio ulitiliwa mkazo na Watafiti wakajaribu kupima ili kubaini kama ni kweli kilichokuepo ni protein inayotakana na Damu. Na utafiti ukaonesha uwepo wa damu katika sanda hiyo.

Na tafiti nyingi zikafanyika na kuleta majibu ya kwamba picha iliyo katila shroud hiyo haikuwa kitu cha kutengenezwa bali uhalisia kabisa mtu aliyekafiniwa na kitambaa hicho.

SEHEMU YA 2

SHROUD OF TURIN, JE , NI KWELI ALIYEVIKWA SANDA HIYO ALIKUWA NI BWANA YESU? TAFITI ZINAHITIMISHA VIPI?


Inaendelea


SEHEMU YA II
SOMA


Shroud of Turin (Sanda Aliyovikwa Bwana Yesu Inayoonyesha SURA Yake). Je, ni kweli ilikuwa ya yesu kristo?
 

Attachments

  • F0B03E29-73E5-4DD7-A4C0-AAD165C93297.jpeg
    F0B03E29-73E5-4DD7-A4C0-AAD165C93297.jpeg
    7.9 KB · Views: 33
Kuna yule aliyebaka kitoto , akalala na mke wa mtoto wake na kulala na jimama

Yule sio Scammer ? Coz kabla hajafa alisema hajui anapokwenda na hajui atakachofanyiwa na hajui pia mwisho wa waumini wake
Sasa mbona inaonekana kama alitayalishwa kama wanavyofanyiwa waisilamu,yaani alizikwa uchi,alivishwa sanda tu,na hakuzikwa na jeneza,wakati wale mafarao wa kale ambao wanachuliwa kama wadhambi ndiyo wanaozikwa na nguo wakiwa ndani ya majeneza,je tunajifunza nini?
 
Sasa mbona inaonekana kama alitayalishwa kama wanavyofanyiwa waisilamu,yaani alizikwa uchi,alivishwa sanda tu,na hakuzikwa na jeneza,wakati wale mafarao wa kale ambao wanachuliwa kama wadhambi ndiyo wanaozikwa na nguo wakiwa ndani ya majeneza,je tunajifunza nini?
Sehemu ya pili mkuu
Ina uchambuzi mwingine, tutajua zaidi cles zinaongelea nini kuhusu maiti yake kuoshwa au laah
 
Sasa mbona inaonekana kama alitayalishwa kama wanavyofanyiwa waisilamu,yaani alizikwa uchi,alivishwa sanda tu,na hakuzikwa na jeneza,wakati wale mafarao wa kale ambao wanachuliwa kama wadhambi ndiyo wanaozikwa na nguo wakiwa ndani ya majeneza,je tunajifunza nini?

Kuzikwa bila nguo ndio kutakuingiza mbinguni?

Je kutembea au kupiga mswaki kama Yesu ndio kutakuingiza mbinguni?

Shughulika na roho , Na sio mwili unaooza
 
Back
Top Bottom