Show za kibabe

Show za kibabe

Meli ya Kifahari ya abiria iliyo kubwa kuliko zote duniani ijulikanayo kama “Icon of the Seas” , imewasili kwa mara ya kwanza huko Miami nchini Marekani, ikitokea Finland ambako imeundwa.

Meli hiyo ilipokelewa kwa shangwe kubwa katika Bandari ya Miami na wakazi wa eneo hilo, mashabiki wa kampuni ya Meli za Royal Carribean na Wafanyakazi waliokuwa na shauku kubwa ya kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Pamoja na kuwa na hifadhi kubwa ya maji (waterpark) kuliko Meli zote duniani, meli hiyo ina vitu vingi vya kipekee ambavyo havikuzoeleka.

Ina urefu wa futi 154 kutokea chini, ina ghorofa 20, ndani yake kuna vitongoji nane. Ina jumla ya vyumba 2805 na inao uwezo wa kuchukua jumla ya abiria 7,600.

Meli hiyo itatoa huduma za safari za siku saba kwa watalii kwenda Mashariki au Magharibi mwa visiwa binafsi vya Karibeani.

Icon of the seas imetengenezwa katika mji wa Turku, nchini Finland, ilifanyiwa majaribio ya kwanza Juni 2023.

Meli hiyo ijulikanayo ”Icon of the Seas” inatarajiwa kuzindua rasmi safari zake Januari 27.

FB_IMG_1705128302528.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 2870361

Sent using Jamii Forums mobile app
IMG-20240113-WA0007.jpg
 
Nime penda ujumbe wa kwenye mabango, lakini kwani sisi bongo hatuna ujumbee wa kiswahili, 😄
Unamaanisha hizi jumbe ziwekwe kwa kiswahili?
Cha kwanza nafkiri kwa ajili ya hadhira lengwa ndio maana ya kuweka jumbe hizi.

Ila kuna sehemu niliona jumbe za kiswahili wamechanganya na kingereza.
IMG-20240113-WA0012.jpg
 
Back
Top Bottom