Show ya Lema vs Pinda featuring Makinda

Du....!!! ki ukweli hapo hachomoki ila akitumia ile njia yake ya kawaida ya kulia na wabunge kumuonea huruma basi itakuwa kiulaiiiiiiini anapigiwa na makofi,,, ila swala la hawezi kulidanganya bunge mimi sikubaliani nalo kwani yeye sio maraika..:A S 20::A S 20::A S 20::A S 20::A S 20::A S 20::A S 20::A S 20::A S 20::roll:
:A S 20:
 
mi nangoja kumuona bwana Pinda akimwaga machozi... ha ha ha ha huyu jamaa ni msuluhisha migogoro na mzindua visima , UWAZIRI KASINGIZIWA..i mean uwazuru mkuu....kazi za hisani zinamfaa zaidi
 


MAMA SPIKA ANNA MAKINDA, BUNGENI KUHESHIMIWE TU 'NGUVU YA HOJA'
KWA WASHIRIKI WOTE; UMRI, VYEO NA USOMI TUKASUBIRIANE MITAANI


Bungeni ndiko pekee mahala ambapo hata nyau tu huthubutu kumtazama moja kwa moja mfalme usoni huku mchezo ukichezwa kwa maneno mdomoni, akili kichwani na maspika wakiwa ni refasrii na washika bendera.

Nasema bungeni ndiko mahala ambapo mchezaji wa kulipwa au kepteni kwenye timu asipokaa vizuri hulambwa chenga mara kibao na wachezaji chipukizi; wengine ambao hata majina bado hawa. Ndio!! Bunge ndio uwanja wa siasa penye mazungumzo ya kistaarabu tu (vijembe, kejeli, na mizengwe mahala pake sokoni) huku kukiw ni kwamba kinachotafutwa kwa kiasi kikubwa ni kushawishiana mwelekeo wa mambo, kuridhishana UKWELI ULIPO, na kutatwa matatizo ya jamii iliowatumeni mahala pale.

Hivyo, hali iliojitokeza kati ya viongozi wetu Waziri Mkuu na Mbunge wa Sumbawanga na mwenzake Mbunge wa Arusha, Gdbless Lema, majuzi bungeni Dodoma, lina mengi mazuri ya kutufundisha kadri bunge letu linavyoendelea kuseheni viongozi vijana na wasomi, kuliko kuishia tu kwenye kutuhumiana UTOVU WA LABDA NIDHAMU na hata wengine kuonekana kule kwamba kila kitiririkacho toka vinywani mwao siku zote kibakia na kuendelea kuwa ni UKWELI NA UKWELI MTUPU!!!

Tusisahau pia kwamba siku zote watu tumezingirwa na minada ya kila aina katika maisha tunayoishi. Wakati mnada wa wafanyabiashara wa mitumba ni Mchikichini kwa Makamba Dar, mnada wa nyama ni Vigunguti, Simu za Wizi pale makutano ya barabara za Independence na Makungnya, ya wambeya vijiweni, na mnada wa silaha haramu toka Rwanda ni pale Kijitonyama Breakpoint, kwao wao wanasiasa mnada wao wa kuuza na au kutetea mawazo chini ya misingi inayoeleweka ni bungeni.

Mpaka hapo kwaza nitangulize po ngezi zangu kwa wabunge wa CHADEMA kwa namna ya pekee wanavyochangia kuweka VIWANGO VYA KIMATAIFA KATIKA UENDESHWAJI WA BUNGE LA VYAMA VINGI ambyo kwa bahati mbaya hayakuzoeleka katika nchi yetu ambayo imekwepo chini ya mfumo wa chama kimoja. Pia, kwa namna ya pekee nimpongeze Mhe Godbless Lema kwa utetezi w nguvu anaouleta bungeni dhidi ya madai ya Waziri Mkuu. Wadadisi wa mambo wanahofia kwamba endapo kutabainika kwamba Mhe Pinda alitoa majibu rahisi kwa maswali magumu basi ofisi ya spika itamchukulia hatua gani?? Jamani wabunge wa CHADEMA mko deepu saaana!! Duu, kwa mtaji wa utetezi huo sasa hapa ni patamu mnoooooooo!! Na sasa tunasubiri kweli kweli mwenendo mzima baada ya hapa tuone inavyokwenda.

Kweli sasa bunge letu si kama enzi zao Marehemu Amran Mayagila,Komanya, Joseph Rwegasira au Fredrick Msuya ambako mbunge kazi yake ilikua ni kuingia pale mjengoni na kuanza kuchapa usingizi waka mjadala ukiendelea huku akitajwa tu jina na spika wa wakati huo, Marehemu Chifu Adam Safi kumuuliza maoni yake juu ya mjadala unaoendelea, mara utasikia mtu mzima kaibuka ndotoni na udenda ukichuruzika, na kusilibia tu jibu lolote lile kama vile 'MHESHIMIWA SPIKA NAUNGA MKONO HOJA ASILIMIA KWA MIA KAMA ILIVYOSEMWA NA MVUNGUMZAJI ALIYETANGULIA'.

Sasa hivi kweli karibu kila mbuge, hasa wale wa upinzani ni watu ambao ni wadadisi wakubwa na wa kudadavua kweli kila nukta n kituo azungumzapo mtu bungeni na hada huku majukwaani mitaani. Ni watu ambao ni wafuatiliaji wakubwa wa mambo, WENYE NIDHAMU KUBWA KWA 'NGUVU YA HOJA' ILA WATOVU WAKUBWA WA NIDHAMU KWA 'HOJA ZA NGUVU'; hata kama hoja za aina hiyo zinashilishwa mbunge mwenye umri mkubwa kuliko Mrehemu mpendwawetu Mzee Abdalla Fundikira, mwenye usomi zaidi ya Maprofesa Sarungi, Mwakyusa au Mwandosya, au mwenye cheo kikubwa cnini kama Mhe Rostam Aziz - kinachoheshimiwa ni nguvu ya hoja tu!!

Je mnaonaje bungeni tukazingatia zaidi heshima, adabu na unyenyeke mkubwa kwa NGUVU ZA HOJA PEKE YAKE (kwa maslahi ya wale waliotutuma bungeni kuwatetea) kama wajumbe rasmi bungeni, halafu baadaye sana tu kukaanza kuzingatia heshima, adabu na unyenyekevu mkubwa kwa umri wa mtu, elimu yake au cheo pindi tukishatoka nje ya bunge??

Hili ni muhimu sana na lazima liwe hivyo mheshimiwa spika kwa sabu ilikuondoa hatari ya waheshimiwa wabunge kubaguana kiumri, kiusomi, na au ki-vyeo kule mjengoni, ni bora tutambue ya kwamba wangiapo ndani ya bunge la ni kazi moja tu - UWAKILISHI WA WATU WAKE WITHOUT FEAR OF FAVOUR - hivyo dira yake kuu ya kutolea heshima, adabu na unyenyekevu ni NGUVU YA HOJA TUU, ili ubunge wake kama li-taasisi linalotegemewa na wengi sana nje ya bunge liweze kufanya kazi bila vikwazo vingi. Hapo ndipo taasisi za Uwaziri Mkuu na Ubunge wa Jimbo la Arusha au nyingine yoyote itaweza kufanya kazi kwa umurua wake stahiki.

Lakini pindi Ndugu Godbless Lema au Mr Sugu, Halima Mdee au David Kafulila anapokutana Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda aka 'Mtoto wa Mkulima' mwenzangu na mimi hapa basi hapo yale yoote heshima, adabu na unyenyekevu ZIWE MBEEELE KAMA TAI kama ilivyo ada katika jamii yetu ya ki-Tanzania, wazee kutambulika kwa kuwa wametuzaa, kisomo huingatiwa kwakuwa hutuwezesha vizuri zaidi kumudu mazingira yetu tunamoishi na vyeo vithaminiwe hasa wenye dhamana hizo wanapovitumia vizuri zaidi na kwa haki kwetu sote.

Mwisho, heshima, adabu na unyenyekevu zote kwa pamoja ni tamu sana ilioje kwa wanaozipata kila leo na hasa pale ambapo zote hupatikana kwa hiari zaidi!!!
 
Mkuu habari ya siku.

Lakini kwa ushahidi gani watamuondoa? huo wa Marry aah naona hautoshi.

Mkuu what more shall I say, the title is self explanatory that 'Pinda atachomokaje kwa ushahidi kama huu'? I know nothing about the validity of this ushahidi, I am simply telling CDM members to go foward with this evidence and take action based on this evidence, WHY??

1. Mpaka sasa vurugu za Arusha kwa mtu mwenye akili TIMAMU kila kosa linawaangukia chadema, uki-refer same caseiliyotokea HAI
2. Mpaka sasa CDM fans wengi wao wamekuwa dragged na kutofahamu maana ya siasa na wanasiasa wamewabatiza ufalme na ukuu wote, they are blind in such a way HAWAJUI SIASA, wanasiasa kwao ni madaktari!!! what a joke! , wengi ni mazezeta fulani kushoto twende, kulia twende.. nao wanaoenda, anapokuja mtu na ushaidi kama huu then tunataka CDM ijisafishe kwa kuchukua hatua kali juu ya Pinda otherwise, Pinda was right, Makinda was right, na Lema hakuwa sahihi!! sitaki kuamini kuwa Pinda alikuwa sahihi!!

Ikishindikana hapo, then CDM members wengi ni ticking bomb! hawako tayari kuinyoshea vidole CDM yao kwa makosa yao, swa kabisa na member wa CCM ambao hawaelewi wala kuambiwa baya la CCM, ikifikia hatua hii sisi watazamaji tunasema ' see robots in CCM and those in CDM'!! is wastage of time, kazi ya ukombozi inakuwa kuwaokoa baadhi ya fans wa CDM na baadhi ya fans wa CCM, sitaki ku-conclude kuwa miafrika ndivyo ilivyo, unakaa pembeni na kuchoka kabisa na kusema is this change we need!!! if is this change we need then we have big problem, umenielewa
 
Hata tukiacha hii, Pinda kisaha lidanyanya Bunge mara kadhaa -- moja ni pale alipoliambia kuwa mkataba kati ya serikali na RITES umevunjwa, kumbe bado kama alivyosema Wzaziri wa Mawasiliano Nundu alipokyutana na wafarnyakazi wa TRL wiki iliyopita.

Nundu aliumbuka pale mmoja wa wafanyakazi alimtolea kavu kavu kwamba mbona Pinda alisema mkataba ulivunjwa? Waziri akawa anakenua meno tu na kutizama chini.

Ingawa hizo 'danganya' zingine za pindi hazihusu suyalka hili, lakini linaonyesha jinsi kiongozi huyo mkuu wa shughuli za kiserikali alivyo muongo aliyebobea.

Lakini nafikiri kama kawaida yake, Makinda na Pinda watategemea tu uwingi wa Wabunge wa CCM kwani hawa wengi ni "yes' men.
NI KWELI ALITAMKA MKATABA UMESHAVUNJWA.HUYU NUNDU KAPATA WAPI HABARI HII?HAKUWASILIANA NA PINDA?pINDA ANAWEZA KUDANGANYA KWANI YE NANI ASISEME UWONGO?
 
Ningelikuwa mie, ningetumia ushahidi kidogo sana sana.

Pinda anasema Watanzania watatu walikufa, ukweli ni kuwa alikuwepo Mkenya mmoja na Watanzania wawili.

Pinda anasema kuwa POLISI walitumia nguvu na kurusha RISASI pale walipoona Waandamanaji wanataka kuvamia Kituo cha Polisi. Je ni kweli waliouawa wote walifia karibu na eneo la POLISI?

Mwisho namalizia kuwa, nilipoomba Mwongozo, sikuwa nasema Pinda kadanganya ila ni PM akidanganya, bila kujali ni Pinda, Lowassa au akija PM kutoka Chadema, CUF au kokote kule.

BTW: POLISI si walizuia maandamano kupitia Luninga? Hawakutoa barua kuzuia maandamano. Wana uhakika gani kuwa Chadema walikuwa wakiangalia TV? Kama wao waliandika barua kuomba ruhusa, na wakapewa kwa maandishi, inakuwaje mtu atangaze kwenye TV kuwa maandamano yamevunjwa bila maandishi yeyote?

Ushahidi wa kumtumia CHATANDA, hata mie ningeliuacha kwanza. Sanasana ningekitumia ule wa Msimamizi wa uchaguzi aliwajulisha CCM na PTL kuwa uchaguzi ni kesho na Chadema hawakujulishwa na hivyo kutokufika kwenye uchaguzi, jambo ambalo wao wanalipinga.
 
Atachomokaje? Simple.
Aliposema aliyoyasema, aliyasema akiamini ni ya ukweli kwa mujibu wa taaaaarifa kutoka kwa subordinates wake. He therefore didn't lie. He presented the facts as fed to him by those who are responsible in keeping him informed.
 
Kwa walioko bungeni, au wanaotazama Luninga zao, naomba mtujuze, mambo yanaanza saa ngapi, na nini kinaendelea.
 
Ninamwona Mh. Dr. Wilbrod Slaa akiwa na Magwanda ndani ya mjengo katika jukwaa la wageni .... yaonekana leo kazi ipo
 
Wameanza na maswali ya kawaida. WN OWM Sera, Lukuvi, ametoa sababu za mwaka 47 kwa nini watu hawakujitokeza kwa wingi kupiga kura Oct 31 iliyopita.
 
Kweli tunaomba mlio kwenye luninga tujuzeni mambo ya mjengoni...
 
Mh. Lazaro Nyalandu Naibu waziri wa Viwanda na biashara amemtakia mke wake happy valentine kabla ya kujibu swali la msingi aliloulizwa bungeni
 
Najuta kutosomea kazi ambayo ningekuwa huru kuvunja sheria ya USUPIKA NA UPOLISI NA UWAZIRIO MKUU
 
Leo ni siku ya mbivu na mbichi kujulikana, endapo ukichakachuliwa ushahidi wa Lema CCM itakuwa na hali ngumu kiama! Ni bora wakubali Pinda alipewa wrong infomation.
 
Back
Top Bottom