Short course ya Siasa miezi mitatu.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,890
SHORT COURSE YA SIASA MIEZI MITATU.

Anaandika, Robert Heriel
Mkufunzi

Najua kila mtanzania ni mwanasiasa lakini wengi wenu mnataka muwe certified. Mambo ya makaratasi au sio. Kumiliki gamba ndio Mpango mzima, asije akakudanganya mtu Cheti cha Siasa ni zaidi ya Cheti cha upolopesa.

Acha nikupe faida ya kumiliki Cheti cha Siasa ambacho nitakupatia Baada ya mafunzo nitakayokupa ndani ya miezi mitatu. Kwa gharama nafuu. Usijesema Taikon nataka kukuingiza mjini na ndevu, kukulia Pesa yako kindezindezi hapana.

Sikiza! Cheti cha Siasa kinafaida zifuatazo;
1. Ukienda kuchumbia Ukweni ukikitoa Cheti cha Siasa unapewa MKE Bure.
Mahari hautoi, Ukweni wanaamini kuwa binti Yao Ipo siku atakuwa First Lady.

2. Ukienda Bank unaweza kuombea mkopo alafu Cheti cha Siasa kikawa mdhamana wako. Alafu Mikopo yenyewe unachukua Pesa ndefu kichizi. Mamilioni ya Pesa utakosa pakuyaweka. Hutaki Pesa wewe?
Alafu maafisa Mikopo muda wa kukudai watakudai Kwa adabu kwelikweli utadhani wao ndio wenye Deni.

3. Cheti cha Siasa kitakufanya uwe juu ya sheria yaani wewe Polisi watakutetemekea wakiona Gamba, Jela haitakuwa kwaajili yako. ukae Jela Cheti kikiwa wapi. Cheti cha Siasa ni bima ya kiteknolojia kukabiliana na mambo hatari Kam hayo. Mimi napendaga kukiita Hirizi ya Simba Junior.
Watafungwa wengine lakini sio Wewe. Uliona wapi wenye Vyeti vya Siasa wakafungwa nawe.

4. Cheti cha Siasa kitakufanya uitwe muhesimiwa hata kama hauna heshima yoyote.
Wangapi nimewapa hivyo Vyeti Hawana lolote lakini wanaitwa wahesimiwa, wanatetemekewa na kusujudiwa. Wewe si haupendi dharau? Si unapenda utukufu, basi njoo nikupe Cheti cha Siasa.

Lakini Taikon wewe hayo mafunzo ulisomea wapi? Nani kakupa mamlaka ya kutoa hivyo Vyeti?
Sasa unaniuliza tena, wewe unataka majibu ya Maswali hayo au unataka Cheti cha Siasa?

Kozi outline nitaitoa humuhumu ili wanaopenda kujiunga wajiunge,
Wakufunzi wa kozi hii tupo Saba nchi nzima, moduli ni zilezile tuu.

Kuhusu gharama ya mafunzo itakuwa NI gharama za kisiasa kama mafunzo yenyewe yalivyo.

Moja ya kozi muhimu zitakazofundishwa ni pamoja na;
1. Verbal intelligence and language Code
2. Public acquisition
3. The Checkers Vs Chess in Politics

Acha nipumzike SASA
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ndo nn
 
Watoa nyuzi zenye nature hii ndio wanafanya riport ya CAG ichelewe kufanyiwa kazi
 
Back
Top Bottom