Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 76,249
- 108,221
Nishareport hii post. Tuko pamoja kiongozi.
Ushapaisha penati mwamba...
Nishareport hii post. Tuko pamoja kiongozi.
Waambie wakubwa watufungulie Jf au kama hutaki tuanze na majaribio ya kureport hii post maana tumechoka ma VPNWakuu,
Salamu nyingi kwenu, wanachama (wana JF) na wageni wote mnaotembelea JamiiForums! Tunayo furaha kubwa kuendelea kuwa nanyi katika jukwaa hili muhimu ambalo limekuwa kitovu cha fikra, maarifa, na uhuru wa kutoa maoni kwa staha.
Ili kuendelea kufurahia mijadala yenye tija na kuhakikisha kila mmoja wetu anakuwa katika mazingira salama, tunapenda kuwakumbusha mambo machache ya msingi:
Tunawashukuru kwa dhati kwa ushirikiano mnaoendelea kuuonyesha kila siku. Mchango wenu katika kuripoti machapisho yanayokiuka taratibu ndio unaoifanya JamiiForums iendelee kuwa sehemu safi, yenye amani, na inayoaminika na kila mtu. Usinukuu andiko na ku-tag moderators, unachelewesha maamuzi; saidia kwa kuripoti ujumbe husika.
- Matumizi ya Kitufe cha 'REPORT': Tunawaomba muwe mabalozi wazuri kwa kutumia kitufe cha 'REPORT' (Ripoti) kilichopo kwenye kila chapisho pale mnapokutana na maudhui yasiyofaa, lugha ya udhalilishaji, au ukiukwaji wowote wa kanuni za jukwaa. Hii ndiyo njia ya haraka na salama zaidi ya kutupa taarifa ili tuchukue hatua.
- Mchakato Wetu wa Usimamizi: Pindi mnaporipoti chapisho, bandiko husika linaondoka automatically na timu yetu ya wasimamizi (moderators) hupitia maudhui husika kwa umakini na weledi mkubwa. Kulingana na miongozo ya jukwaa letu, tunaweza kuchukua hatua za kurekebisha (edit) au kuondoa kabisa (remove) maudhui hayo. Wale wanaoonekana wamevunja taratibu kupitiliza, wataonywa au kufungiwa kwa muda. Lengo letu kuu siku zote ni kulinda heshima na hadhi ya jukwaa letu kwa manufaa ya wote.
Jukwaa hili ni letu sote, na kuliweka salama ni jukumu letu sote. Tuendelee kushirikiana na kuhamasishana kujenga mijadala yenye afya na kuheshimiana bila kujali tofauti zetu za kimawazo.
Pamoja tunaweza kudumisha ubora wa JamiiForums!
Wasalaam,
Hadi Melo mwenyewe ameona acheke tu😂😂Nishareport hii post. Tuko pamoja kiongozi.
Umenisaidia, mie namkubali mkaka m1 hapo yupo km Halfcast, afu km ana tatizo la macho (sina hakika) ana vitu vyangu kabisa yule kakaMaxence Melo sema nawaelewa hao warembo hapo ofisini😎😎 haswa huyo bonge bonge😍😍🤌🤌... Wadau msini report 😑😑
Kabisa km mie, ni kwenda nao sambamba.Max weka jukwaa la malalamiko na lia lia FC 😹😹😹
Wengine wanaanzaga shengesha wenyewe. Yakiwazidia wanaanza kujiliza huko HQ.. Mimi adui nnayemmudu siwaachii mods ni bampa to bampa..!!
Nimebonyeza hapo sijaona kitu
Life ban itakuwepo endapo kutakuwa na “gross violation of our community engagement guidelines”. Zisome hapa - JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala
Nimecheka sana.LHata wakongwe kama mimi ninapokuta natukanwa na kijana anayeweza kuwa mjukuu wangu nikamsihi kuwa awe mstaarabu lakini akazidi matusi basi huwa namwonyesha kuwa nilianza kutukanwa kabla hajazaliwa hivyo nina akiba kubwa sana ya matusi pia.
Anza kwa kuwashughulikia kwa kusaidia kuondoa posts zao wewe.Ndugu Maxence Melo kuna wale wanaotukana matusi ya nguoni na kutoa lugha za kuudhi wanaposhindwa hoja katika kutetea vyama vyao vya siasa.
Naomba muwashughulikie ipasavyo memba hao kwa maslahi mapana ya jukwaa hili pendwa.
Asante