Habari wapendwa katika bwana,naomba kuwasilisha hoja
Kwa mwezi wa pili tarehe 27/02/2018 serikali kupitia ofisi ya rais -TAMISEMI ilitangaza ajira za walimu takribani 45,000. Ambapo waombaji walitakiwa kuomba kwa njia ya mtandao.
Watu walipewa siku 18 kuwasilisha maombi yao ,ambapo jumla ya waombaji 91,000 walijitokeza kuwania nafasi hizi,ambapo ikiwa ofisi ya rais-TAMISEMI ingewataka waombaoji kutuma maombi yao kwa njia ya posta ,tuchukulie kila bahasha kwa mfumo wa EMS kulingana na wingi wa viambato kila bahasha ingalighalimu kiasi kisichopungua 11,500 x waombaji 91,000 = 1,046,500,000/= hivyo shirika letu la posta lingepata kiasi hicho cha fedha kwa muda Wa Sikh 18 tu.
Kwa hali hii naiomba serikali yangu kuwa makini katika kukusanya mapato ili kuhakikisha mashirika yetu ya umma yanapiga hatua hivyo kuweza kusonga mbele kimaendeleo.
Ushauri wangu ni kuwa serikali ihimize nyaraka zote za serikali zitumwe kwa njia ya posta ili kuliinua shirika letu kiuchumi
Lakini nashauri wizara ya OR-TAMISEMI na wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kufanikisha hili jambo
Ahsanteni.
Sent using
Jamii Forums mobile app