Shirika la FCS: Tunapongeza usimamiaji na kuheshimu misingi ya Demokrasia Nchini chini ya Rais Samia

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la The Foundation For Civil Society (FCS), Francis Kiwanga amesema Shirika hilo linajivunia miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuheshimu na kusimamia misingi ya Demokrasia.

Kiwaga amesema kuwa FCS inajivunia uongozi wa Rais Samia unaoheshimu misingi ya Demokrasia na uhuru wa watu, ambapo amebainisha kuwa FCS itaendelea kuwa daraja kati ya watu na Serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
photo_2024-03-07_13-04-01.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS anayemaliza muda wake wa uongozi Francis Kiwanga akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi nyaraka za Ofisi na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi hiyo Justice Rutenge.
photo_2024-03-07_13-04-01 (2).jpg

Mwenyekiti wa Bodi ya FCS, DKt. Ally Laay, (kulia) akizungumza alipokuwa akielezea mchakato mzima wa kumpata Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS, Justice Rutenge.
"Kwetu sisi tunaona ni taasisi inayopigania misingi ya utawala bora, tunahitaji kuendeleza juhudi za kupambania maendeleo ya watu, na hili ni suala la kujikumbusha kila siku," amesema Kiwanga.

Kiwanga ameyasema hayo wakati akikabidhi akikabidhi ofisi kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya, Justice Rutenge, Jijini Dar es Salaam ambaye anatarajiwa kuanza majukumu yake rasmi rasmi Mei, 2024.

Kiwaga amesema licha ya kuwa anamaliza muda wake ameahidi kuendeleza ushiriano na Shirika hilo na atakuwa balozi kwa kutoa mchango wake pindi atakapohitajika.

Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya FCS, DKt. Ally Laay, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake kwa kuwa mchapakazi, mwadilifu na kusimamia majukumu yake kwa weledi na kuiheshimisha FCS.

Pia, amesema ana imani kubwa na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge anayetarajiwa kuanza rasmi majukumu yake Mei Mosi, 2024.

"Bwana Rutenge ameshinda kwa kishindo kikubwa licha ya kuwepo ushindani mkubwa katika mchakato mzima wa kumpata Mkurugenzi Mtendaji mpya, bodi imemwamini kuwa atafanya kazi vizuri na kuendelea alipoishia Kiwanga kutokana na sifa alizo nazo na ni kijana," amesema Laay.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge, ameahidi kufanya kazi kwa weledi kulingana na taaluma na ujuzi alio nao kwa maslahi mapana ya jamii na Serikali kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom