Shirika halijajibu Hoja za Mkaguzi ya kuwa linajiendesha kwa Hasara, limeona liandae futari kwenye hoteli ya kifahari

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Kwenye mitandao ya kijamii miongoni mwa mashirika yaliyotajwa kujiendesha Kwa Hasara ni shirika la TTCL mpaka imefika hatua inashauliwa yakuwa lianchane na biashara ya kuuza line libakie kusimamia barua za sanduku la posta na mkongo wa Taifa.

Kabla halijajibu Hoja Kwa Nini linajiendesha Kwa Hasara linaandaa FUTARI NA MGENI RASMI NI WAZIRI WA HABARI, fedha za kuandaa futari zimetoka wapi?mnaendelea kututia hasara hivi kama mti husio zaa UNAAMBIWA ungolewe shambani hauna tija,wewe uzalishi unakulaje?

Sisi WANANCHI tuliopo huku Aliko aliyekuwa anaongoza shirika ilo tupo mbioni kumfukuza haiwezekani tuongozwe. Na mkuu wa mkoa aliyearibu shirika la Umma nyie mnandaa futari?na picha mnapiga mnavyosonsomora aise?
Fikirieni mara mbili!.
20230413_045846.jpg
20230413_045842.jpg
20230413_045838.jpg
20230413_045835.jpg

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye (Mb) amekuwa Mgeni Rasmi katika Futari iliyoandaliwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam Tarehe 12 Aprili, 2023.
 
Kwenye mitandao ya kijamii miongoni mwa mashirika yaliyotajwa kujiendesha Kwa Hasara ni shirika la TTCL mpaka imefika hatua inashauliwa yakuwa lianchane na biashara ya kuuza line libakie kusimamia barua za sanduku la posta na mkongo wa Taifa...
Pamoja na Uzi wako ila rekebisha hapo ulipotaja kusimama sanduku la barua.

TTCL haihusiki nasanduku (box) za barua, mkongo ni SAWA.

Acha mhemko!
 
Kwenye mitandao ya kijamii miongoni mwa mashirika yaliyotajwa kujiendesha Kwa Hasara ni shirika la TTCL mpaka imefika hatua inashauliwa yakuwa lianchane na biashara ya kuuza line libakie kusimamia barua za sanduku la posta na mkongo wa Taifa...
Mnaomtetea Nape ndo mjifunze hapo namna uwezo wake wa reasoning

Shirika lina hasara babkubwa. Wewe unaalikwa iftar ya mamilion ya shilingi iliyoandaliwa na shirika linalopumulia gesi kisha unaenda.

Waziri anayejitambua angrjjukiza hawa hiyo pesa wanaitoa wapi na kwa nini isitumike kuanza kupunguza hasara wanayopitia.

Seems Nape ni sehemu ya hasara ya TTCL. Serikali ichunguze na iwe kipimo cha utendaji wake kwa kuangalia uimara wa taasisi zilizo chini yake
 
Ndio tujue kuwa nchi ipo autopilot. Kwamba ni ukweli usiopingika kuwa hatuna mkuu wa * mwenye weledi wala maarifa ya kuliongoza *, sad truth wallah!!

Huyo Nape ni reflection ya uongozi ulioshindwa, anachofanya ni kudhihirisha kuwa taifa limefeli kimfumo, na hata mamlaka zilizomteua hazina uwezo wa kupambanua, na ndio maana halisi ya kula kwa urefu wa kamba.
 
umemaliza !!! , kwenye nchi yenye viongozi wenye akili wangemfukuza huyo jamaa, ni TZ hapo tu ndio waziri anawajibu jeuri wananchi
 
Yote tunayoyasema hapa kama dharau kwa wananchi walifanya mahesabu na kupata Majibu kuwa kutakuwa na malalamiko then Mh. Waziri akaulizwa vp itakuwaje? Then Mh. Waziri akawahakikishia kuwa wapo salama shughuli liendelee.

Yaani mtoto wako amerudishwa nyumbani kisa wewe mzazi hujalipa ADA alafu wewe mzazi unafanya birthday ya nguvu....tafsiri yake ni nini?
 
Back
Top Bottom