Shinyanga: Mkulima, Mfugaji wafariki kwa Kupigwa na Radi wakati wakisuluhishwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
WATU wawili wakazi wa Kitongoji cha Salawe A, Kijiji cha Salawe, Kata ya Ubagwe, Halmashauri ya Ushetu, Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi nyumbani kwa mwenyekiti akiwasuluhisha mgogoro uliokuwa ukiwakabili.

Tukio hilo limetokea nyumbani kwa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Daniel Malunde, wakati akisuluhisha kesi ya mifugo ya mfugaji Shija Machelewa (57) kuingia shambani kwa mkulima Petro Augustino (62) na kula mazao yake.

Wakati mifugo hiyo ikila mazao ya mkulima huyo, aliyekuwa akiichunga alikuwa ameelekea bondeni kutafuta maji ya kunywa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi (ACP) Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema baada ya uchunguzi, miili hiyo ilikabidhiwa kwa ndugu. Hakuna mtu aliyeshikiliwa kutokana na tukio hilo.
 
Kumbe na shinyanga Hilo la radi lipo?
Sumbawanga na kigoma ndo Mambo yao hayo.
Hiyo radi kuna mawili, either katumiwa Mwenyekiti imechapa hao wapuuzi wawili wasio na kinga. Au hao wapuuzi wawili wametumiana wenyewe kwa wenyewe. Ndiyo michezo yao hiyo, huko radi zimeshachapa watu mpaka mahakamani live live na hakimu kumaliza kesi hapo hapo.
 
Back
Top Bottom