Sumbawanga: Radi yasababisha kifo cha mtu mmoja na ng'ombe 27

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,775
Sumbawanga: Mwanaume mmja amepoteza maisha papo hapo Kwa kupigwa na Radi wakati akilima na kusababisha kifo chake na Ng'ombe 2 alikuwa akiwatumia kulimia huko Kijiji Cha Muze.

Aidha katika tukio jingine Ng'ombe 25 wamepoteza maisha kwenye Kijiji Cha Tamasenga Kwa kupigwa na Radi.

--
Kufuatia Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha Maafa Wananchi wilayani sumbawanga Mkoani Rukwa wametakiwa kuchukua tahadhari za kiusalama ikiwa ni pamoja na kusimamisha Shughuli za Kilimo Pindi Mvua zinaponyesha.

Hayo yamejiri Mara baada ya Mvua kubwa iliyoambatana na Radi Kusababisha Maafa katika vijiji viwili tofauti wilayani humo ambapo Kijana mmoja aitwaye Edward Ibrahim Silungu mwenye Umri wa Miaka 32 katika Kijiji Cha Muze na Ng'ombe wawili aliokuwa akilimia Shambani kwake walipotezamaisha kwa kupigwa na radi, huku Katika kijiji cha Tamasenga Manispaa ya Sumbawanga Ng’ombe 25 wakifariki kwa kupigwa na radi

Akieleza Kuhusu tukio Hilo Shuhuda Ambaye ni Baba Mzazi wa Kijana huyo Ibrahim Silingu amesema kuwa walikuwa Shambani wakiendelea na Shughuli za Kilimo ndipo Mvua ilianza kunyesha Kisha baada ya Muda zilisikika Ngurumo zikiambatana na Radi na kusababisha Kijana wake kupigwa na Radi yeye pamoja na Ng'ombe wake wawili Wakati akiendelea na zoezi la Kulima Shambani kwake.

Akitoa Salamu za pole Kwa niaba ya Serikali Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe . Ally Chirukile ametoa wito Kwa wananchi kuchukua tafadhali katika kipindi hiki Cha Mvua kubwa ikiwa ni pamoja na Kuacha kufanya shughuli za Kilimo Kwa Kutumia Ng'ombe Wakati Mvua ikiendelea kunyesha.

Aidha amewataka wananchi wanaokaa sehemu za Mabonde kuhakikisha wanahamia sehemu amambazo ni Salama na kuzingatia utunzaji wa Mazingira inayosaidia miundombinu ishirabikike Wakati wa Mvua kubwa.

Chanzo: Wasafi

My Take
Hii ni Ajali ya kawaida msije husisha na mambo yenu ya kishirikina.

Poleni sana mliokumbwa na Madhila haya.
 
hii umeme ni mbaya sana,
huko nyuma kijijini nikiwa na bibi yangu tunatoka mashineni kusaga unga, tumekaribia nyumbani kabisa, ghafla dalili ya mvua ikawa imetanda hatari hadi giza yaani, radi za ngurumo na zile za flash za kuwaka zilikua kali na hatari mno.....

Ghafla bana mbele yetu ni kama fimbo yenye moto mkali ilivurumushwa kwa kasi ya 5G, ikakatiza mbele yetu jirani yetu mimi na bibi yangu ikaenda kupasua na kuuchanjachanja mti mkubwa ulokua mbele yetu nilivibrate kama kiswaswadu nikimng'ang'ania bibi yangu...

I.R.P Mwendazake huko sumbawanga
 
Hiyo radi iliyoua ng'ombe 25 usiku nilisikia mngurumo wake nikadhani ni kombora la Israel limepotea njia badala ya kuwatwanga Hamas limeangukia Sumbawanga!
 
Sumbawanga: Mwanaume mmja amepoteza maisha papo hapo Kwa kupigwa na Radi wakati akilima na kusababisha kifo chake na Ng'ombe 2 alikuwa akiwatumia kulimia huko Kijiji Cha Muze.

Aidha katika tukio jingine Ng'ombe 25 wamepoteza maisha kwenye Kijiji Cha Tamasenga Kwa kupigwa na Radi.

--
Kufuatia Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha Maafa Wananchi wilayani sumbawanga Mkoani Rukwa wametakiwa kuchukua tahadhari za kiusalama ikiwa ni pamoja na kusimamisha Shughuli za Kilimo Pindi Mvua zinaponyesha.

Hayo yamejiri Mara baada ya Mvua kubwa iliyoambatana na Radi Kusababisha Maafa katika vijiji viwili tofauti wilayani humo ambapo Kijana mmoja aitwaye Edward Ibrahim Silungu mwenye Umri wa Miaka 32 katika Kijiji Cha Muze na Ng'ombe wawili aliokuwa akilimia Shambani kwake walipotezamaisha kwa kupigwa na radi, huku Katika kijiji cha Tamasenga Manispaa ya Sumbawanga Ng’ombe 25 wakifariki kwa kupigwa na radi

Akieleza Kuhusu tukio Hilo Shuhuda Ambaye ni Baba Mzazi wa Kijana huyo Ibrahim Silingu amesema kuwa walikuwa Shambani wakiendelea na Shughuli za Kilimo ndipo Mvua ilianza kunyesha Kisha baada ya Muda zilisikika Ngurumo zikiambatana na Radi na kusababisha Kijana wake kupigwa na Radi yeye pamoja na Ng'ombe wake wawili Wakati akiendelea na zoezi la Kulima Shambani kwake.

Akitoa Salamu za pole Kwa niaba ya Serikali Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe . Ally Chirukile ametoa wito Kwa wananchi kuchukua tafadhali katika kipindi hiki Cha Mvua kubwa ikiwa ni pamoja na Kuacha kufanya shughuli za Kilimo Kwa Kutumia Ng'ombe Wakati Mvua ikiendelea kunyesha.

Aidha amewataka wananchi wanaokaa sehemu za Mabonde kuhakikisha wanahamia sehemu amambazo ni Salama na kuzingatia utunzaji wa Mazingira inayosaidia miundombinu ishirabikike Wakati wa Mvua kubwa.

Chanzo: Wasafi

My Take
Hii ni Ajali ya kawaida msije husisha na mambo yenu ya kishirikina.

Poleni sana mliokumbwa na Madhila haya.
Huko yasemekana radi yaweza piga mchana wa jua kali ikamchagua imtakaye na ikachagua ng'ombe walionenepa ikaacha waliokonda!
 
Back
Top Bottom