Shinyanga: Achinjwa kwa deni la sh 400,000

MKAZI wa Majengo Sokola, katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Gongo Charles (30), ameuawa kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa kumdai Sh. 400,000.

Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu, Charles Kwilasa, tukio la kuuawa mwanawe limetokea Agosti 4, mwaka huu, usiku.

“Majira ya saa mbili usiku tulipomaliza kula chakula familia nzima tukaingia kulala akiwamo marehemu, kumbe kijana wangu baadaye alitoka nje na baada ya kufika saa tano akaja kwenye dirisha la nyuma kumgongea mdogo wake,” alisema.

Kwilasa alisema, mdogo wake wakati anamfungulia kaka yake alikuwa na watu wawili na alipoingia ndani walianza kudaiana pesa.

Aliwanukuu wakisema; “tupe sasa hela zetu tuondoke”. Alisema kwa kuwa hakuwa na chochote aliingia chumbani kwenda kumwomba mdogo wake ambaye naye alimweleza hana kiasi chochote bali kiasi alichokuwa nacho tayari amenunua mchele.

Mzazi huyo aliendelea kusimulia kuwa vurugu zilianzia hapo wakati yeye hakujua kinachoendelea, lakini baada ya kusikia mwanawe akilia ndipo alipofungua mlango wake na kutoka nje na alikutana watu wawili wakitoka nje haraka.

Aliendelea kusimulia kuwa kabla ya kuwafuatilia alifika mdogo wake na kumweleza kuwa kaka yake amepigwa na kucharangwa mapanga na watu wawili.

Kwa mujibu wa maelezo ya mzazi huyo wauaji baada ya kukosa kiasi wanachotaka na kabla ya kutekeleza mauaji hayo walimtaka marehemu akaombe kiasi hicho kwa baba yake.

Alisema hata hivyo, alikataa na kuwaahidi kuwa angewalipa baadaye ndipo watu hao walipopandwa na hasira na kumfanyia ukatili huo.

Mdogo wa marehemu, Derick Charles, akizungumza na gazeti hili nyumbani kwao, alidai kuwa majira ya saa tano usiku aligongewa dirisha na kaka yake na alipokwenda kufungua mlango alirudi kulala, lakini baada ya muda mfupi kaka yake alimfuata chumbani na kumwomba kiasi cha Sh. 400,000 ili awakabidhi watu wawili aliofika nao ndani kwa madai kuwa wanamdai.

“Mimi nilimwambia kaka kwa sasa sina hela bali nimezinunua mchele kwa ajili ya kuuza kwenye kibanda changu baada ya kumweleza hivyo alirudi sebuleni na kulala.”

Alisema alimwambia kaka yake ambaye kwa sasa ni marehemu azime taa na kufunga mlango, lakini hakumjibu chochote.

Muda mfupi baadaye alisema akasikia kelele za kuomba msaada na alipotoka chumbani alikuta akiwa ashafariki kwa kuchinjwa na kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake,” alisema Derick.

Derick alisema baada ya kushuhudia mauaji hayo wauaji walitokomea kusikiojulikana na aliamua kutoka nje ili kumweleza baba yake jinsi tukio lilivyotokea.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, George Kyando, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wanaendelea na msako ili kuwabaini watu waliofanya unyama huo.

Ippmedia
Binaadamu wamekua zaidi ya wanyama, sijui ni umaskini au ni kitu gani, unatoa uhai wa mtu kwa ajili ya pesa?
 
Muda mfupi baadaye alisema akasikia kelele za kuomba msaada na alipotoka chumbani alikuta akiwa ashafariki kwa kuchinjwa na kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake,” alisema Derick.
Halafu utawasikia wajinga kua watu wa kaskazini wanauana sana...shy inaongoza kwa mauaji ya wazee,waganga,uchawi,visasi
 
Shetani anakuletea uhitaji wa hela uliyokopesha Kama ndy tegemeo pekee la maisha
Anakufany umuone uliyemkopa kuwa yeye ndyo anafanya ufike mahali umkufuru muumba wako.
Anajaza chuki kwa moyo final unafanya vtu visivyo eleweka Mana ili kupata hiko kitu lazma mkopeshwaji awe na Hali nzuri

Watu wanasahau Hilo baadae ndy hyo Hali inatokea

So sad
Wakopaji huwa mnazingua Sana , mtu anakusaidia alaf unaniona Fala , ni rahsi kuwahukumu wale majamaa Ila ni kitu cha kujifunza pia Kwa wale wadaiwa sugu , somtime natoa bigup Kwa banks kuwafilisi
 
Muda mfupi baadaye alisema akasikia kelele za kuomba msaada na alipotoka chumbani alikuta akiwa ashafariki kwa kuchinjwa na kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake,” alisema Derick.
Hata Mimi naendelea kushangaa na Kama Ni kweli ndugu yake na familia yake watakuwa wazembe sana,vinginevyo polisi waanze na hao ndugu kuwachunguza.
 
MKAZI wa Majengo Sokola, katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Gongo Charles (30), ameuawa kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa kumdai Sh. 400,000.

Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu, Charles Kwilasa, tukio la kuuawa mwanawe limetokea Agosti 4, mwaka huu, usiku.

“Majira ya saa mbili usiku tulipomaliza kula chakula familia nzima tukaingia kulala akiwamo marehemu, kumbe kijana wangu baadaye alitoka nje na baada ya kufika saa tano akaja kwenye dirisha la nyuma kumgongea mdogo wake,” alisema.

Kwilasa alisema, mdogo wake wakati anamfungulia kaka yake alikuwa na watu wawili na alipoingia ndani walianza kudaiana pesa.

Aliwanukuu wakisema; “tupe sasa hela zetu tuondoke”. Alisema kwa kuwa hakuwa na chochote aliingia chumbani kwenda kumwomba mdogo wake ambaye naye alimweleza hana kiasi chochote bali kiasi alichokuwa nacho tayari amenunua mchele.

Mzazi huyo aliendelea kusimulia kuwa vurugu zilianzia hapo wakati yeye hakujua kinachoendelea, lakini baada ya kusikia mwanawe akilia ndipo alipofungua mlango wake na kutoka nje na alikutana watu wawili wakitoka nje haraka.

Aliendelea kusimulia kuwa kabla ya kuwafuatilia alifika mdogo wake na kumweleza kuwa kaka yake amepigwa na kucharangwa mapanga na watu wawili.

Kwa mujibu wa maelezo ya mzazi huyo wauaji baada ya kukosa kiasi wanachotaka na kabla ya kutekeleza mauaji hayo walimtaka marehemu akaombe kiasi hicho kwa baba yake.

Alisema hata hivyo, alikataa na kuwaahidi kuwa angewalipa baadaye ndipo watu hao walipopandwa na hasira na kumfanyia ukatili huo.

Mdogo wa marehemu, Derick Charles, akizungumza na gazeti hili nyumbani kwao, alidai kuwa majira ya saa tano usiku aligongewa dirisha na kaka yake na alipokwenda kufungua mlango alirudi kulala, lakini baada ya muda mfupi kaka yake alimfuata chumbani na kumwomba kiasi cha Sh. 400,000 ili awakabidhi watu wawili aliofika nao ndani kwa madai kuwa wanamdai.

“Mimi nilimwambia kaka kwa sasa sina hela bali nimezinunua mchele kwa ajili ya kuuza kwenye kibanda changu baada ya kumweleza hivyo alirudi sebuleni na kulala.”

Alisema alimwambia kaka yake ambaye kwa sasa ni marehemu azime taa na kufunga mlango, lakini hakumjibu chochote.

Muda mfupi baadaye alisema akasikia kelele za kuomba msaada na alipotoka chumbani alikuta akiwa ashafariki kwa kuchinjwa na kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake,” alisema Derick.

Derick alisema baada ya kushuhudia mauaji hayo wauaji walitokomea kusikiojulikana na aliamua kutoka nje ili kumweleza baba yake jinsi tukio lilivyotokea.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, George Kyando, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wanaendelea na msako ili kuwabaini watu waliofanya unyama huo.

Ippmedia
Huyo baba alijuaje kama hao wauaji walimtaka aende kuomba pesa kwake yeye? Maana yeye hakuwepo na wala mdogo mtu hakuwepo wakati mauaji yanatokea, kwa maelezo ya mdogo mtu, yeye alisikia kelele na kukuta kaka yake ameshafariki tayari, maana alivyogongewa na kumjibu hana alirudi kulala hadi aliposikia kelele. Babata mtu nae alitoka baada ya kusikia kelele. Sasa imekuwaje?
 
Lakini kila kitu ni kwa agreement yawezekana agreement zao mtu kufa asipo lipa kwa wakati napo huwez jua
 
Laki 4 si pesa ya kuhonga pisi kali unaua mtu kwa ajili ya Laki 4 ya kitanzania?
Kweli umasikini bado upo kwa kasi ya 5G.
 
Huyo baba alijuaje kama hao wauaji walimtaka aende kuomba pesa kwake yeye? Maana yeye hakuwepo na wala mdogo mtu hakuwepo wakati mauaji yanatokea, kwa maelezo ya mdogo mtu, yeye alisikia kelele na kukuta kaka yake ameshafariki tayari, maana alivyogongewa na kumjibu hana alirudi kulala hadi aliposikia kelele. Babata mtu nae alitoka baada ya kusikia kelele. Sasa imekuwaje?
Maelezo ya mzee na ya huyo mdogo wa marehemu yanatofautiana kidogo.

Maelezo ya mzee ni kama huyo mdogo mtu aliwaona hao watu wawili wakati akimfungulia mlango kaka yake, lakini mdogo mtu anasema yeye alifungua mlango na kurudi Kulala yaani hakuwaona.
 
Hata Mimi naendelea kushangaa na Kama Ni kweli ndugu yake na familia yake watakuwa wazembe sana,vinginevyo polisi waanze na hao ndugu kuwachunguza.
Hata mimi nimeshangaa kuwa walishindwa kutuliza jahazi mapema kabla hayajatokea
 
Jamaa mpumbavu unalalaje chumbani huku ndugu yako yuko sebuleni amezongwa fala sana.. akamatwe kwa uchunguzi
MKAZI wa Majengo Sokola, katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Gongo Charles (30), ameuawa kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa kumdai Sh. 400,000.

Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu, Charles Kwilasa, tukio la kuuawa mwanawe limetokea Agosti 4, mwaka huu, usiku.

“Majira ya saa mbili usiku tulipomaliza kula chakula familia nzima tukaingia kulala akiwamo marehemu, kumbe kijana wangu baadaye alitoka nje na baada ya kufika saa tano akaja kwenye dirisha la nyuma kumgongea mdogo wake,” alisema.

Kwilasa alisema, mdogo wake wakati anamfungulia kaka yake alikuwa na watu wawili na alipoingia ndani walianza kudaiana pesa.

Aliwanukuu wakisema; “tupe sasa hela zetu tuondoke”. Alisema kwa kuwa hakuwa na chochote aliingia chumbani kwenda kumwomba mdogo wake ambaye naye alimweleza hana kiasi chochote bali kiasi alichokuwa nacho tayari amenunua mchele.

Mzazi huyo aliendelea kusimulia kuwa vurugu zilianzia hapo wakati yeye hakujua kinachoendelea, lakini baada ya kusikia mwanawe akilia ndipo alipofungua mlango wake na kutoka nje na alikutana watu wawili wakitoka nje haraka.

Aliendelea kusimulia kuwa kabla ya kuwafuatilia alifika mdogo wake na kumweleza kuwa kaka yake amepigwa na kucharangwa mapanga na watu wawili.

Kwa mujibu wa maelezo ya mzazi huyo wauaji baada ya kukosa kiasi wanachotaka na kabla ya kutekeleza mauaji hayo walimtaka marehemu akaombe kiasi hicho kwa baba yake.

Alisema hata hivyo, alikataa na kuwaahidi kuwa angewalipa baadaye ndipo watu hao walipopandwa na hasira na kumfanyia ukatili huo.

Mdogo wa marehemu, Derick Charles, akizungumza na gazeti hili nyumbani kwao, alidai kuwa majira ya saa tano usiku aligongewa dirisha na kaka yake na alipokwenda kufungua mlango alirudi kulala, lakini baada ya muda mfupi kaka yake alimfuata chumbani na kumwomba kiasi cha Sh. 400,000 ili awakabidhi watu wawili aliofika nao ndani kwa madai kuwa wanamdai.

“Mimi nilimwambia kaka kwa sasa sina hela bali nimezinunua mchele kwa ajili ya kuuza kwenye kibanda changu baada ya kumweleza hivyo alirudi sebuleni na kulala.”

Alisema alimwambia kaka yake ambaye kwa sasa ni marehemu azime taa na kufunga mlango, lakini hakumjibu chochote.

Muda mfupi baadaye alisema akasikia kelele za kuomba msaada na alipotoka chumbani alikuta akiwa ashafariki kwa kuchinjwa na kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake,” alisema Derick.

Derick alisema baada ya kushuhudia mauaji hayo wauaji walitokomea kusikiojulikana na aliamua kutoka nje ili kumweleza baba yake jinsi tukio lilivyotokea.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, George Kyando, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wanaendelea na msako ili kuwabaini watu waliofanya unyama huo.

Ippmedia
 
Shinyanga hapana wamezidi kwa mauaji kuliko sehemu yoyote Tanzania hata uzalilishaji pia na ubakaji ni huko shinyanga.
Nadhani sababu ni wamechelewa sana kuelimika na ni washamba bado.
Musoma Mara, Shinyanga, Kumezidi hiyo mikoa, ikifuatiwa na Arusha alafu Mbeya.
Sijasikia Lindi au Tanga wakifanya haya.
 
Kuna mikoa ni ya hovyo sana.
Matukio ya hovyo namna hii huwezi kuyasikia mkoa wa Lindi.
Matukio ya hovyo Lindi ni nadra sana
Si ndiyo hata mimi nimekomment hapa hivyo kumbe mawazo yetu yanafanana, tatizo ni dini na elimu hawana.
 
MKAZI wa Majengo Sokola, katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Gongo Charles (30), ameuawa kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa kumdai Sh. 400,000.

Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu, Charles Kwilasa, tukio la kuuawa mwanawe limetokea Agosti 4, mwaka huu, usiku.

“Majira ya saa mbili usiku tulipomaliza kula chakula familia nzima tukaingia kulala akiwamo marehemu, kumbe kijana wangu baadaye alitoka nje na baada ya kufika saa tano akaja kwenye dirisha la nyuma kumgongea mdogo wake,” alisema.

Kwilasa alisema, mdogo wake wakati anamfungulia kaka yake alikuwa na watu wawili na alipoingia ndani walianza kudaiana pesa.

Aliwanukuu wakisema; “tupe sasa hela zetu tuondoke”. Alisema kwa kuwa hakuwa na chochote aliingia chumbani kwenda kumwomba mdogo wake ambaye naye alimweleza hana kiasi chochote bali kiasi alichokuwa nacho tayari amenunua mchele.

Mzazi huyo aliendelea kusimulia kuwa vurugu zilianzia hapo wakati yeye hakujua kinachoendelea, lakini baada ya kusikia mwanawe akilia ndipo alipofungua mlango wake na kutoka nje na alikutana watu wawili wakitoka nje haraka.

Aliendelea kusimulia kuwa kabla ya kuwafuatilia alifika mdogo wake na kumweleza kuwa kaka yake amepigwa na kucharangwa mapanga na watu wawili.

Kwa mujibu wa maelezo ya mzazi huyo wauaji baada ya kukosa kiasi wanachotaka na kabla ya kutekeleza mauaji hayo walimtaka marehemu akaombe kiasi hicho kwa baba yake.

Alisema hata hivyo, alikataa na kuwaahidi kuwa angewalipa baadaye ndipo watu hao walipopandwa na hasira na kumfanyia ukatili huo.

Mdogo wa marehemu, Derick Charles, akizungumza na gazeti hili nyumbani kwao, alidai kuwa majira ya saa tano usiku aligongewa dirisha na kaka yake na alipokwenda kufungua mlango alirudi kulala, lakini baada ya muda mfupi kaka yake alimfuata chumbani na kumwomba kiasi cha Sh. 400,000 ili awakabidhi watu wawili aliofika nao ndani kwa madai kuwa wanamdai.

“Mimi nilimwambia kaka kwa sasa sina hela bali nimezinunua mchele kwa ajili ya kuuza kwenye kibanda changu baada ya kumweleza hivyo alirudi sebuleni na kulala.”

Alisema alimwambia kaka yake ambaye kwa sasa ni marehemu azime taa na kufunga mlango, lakini hakumjibu chochote.

Muda mfupi baadaye alisema akasikia kelele za kuomba msaada na alipotoka chumbani alikuta akiwa ashafariki kwa kuchinjwa na kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake,” alisema Derick.

Derick alisema baada ya kushuhudia mauaji hayo wauaji walitokomea kusikiojulikana na aliamua kutoka nje ili kumweleza baba yake jinsi tukio lilivyotokea.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, George Kyando, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wanaendelea na msako ili kuwabaini watu waliofanya unyama huo.

Ippmedia
Ujinga ukifunga ndoa na umaskini haya ndiyo matokeo ambapo tofauti ya binadamu na mnyama iko wazi.
 
Muda mfupi baadaye alisema akasikia kelele za kuomba msaada na alipotoka chumbani alikuta akiwa ashafariki kwa kuchinjwa na kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake,” alisema Derick.

kahama kuna madini mengi na uzi wangu wa madini niliyoona machimboni nazani tumepata picha.

karibu kwenye watu wamadini
 
Back
Top Bottom