Watu 18 wakutwa na kipindupindu Shinyanga

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amesema watu 18 kati ya 41 ambao walikabiliwa na tatizo la kuhara na kutapika, wamebainika kuwa na ugonjwa wa kipindupindu mkoani humo.

Desemba 28 mwaka Jana, Mkoa wa Shinyanga katika Kata ya Kagongwa wilayani Kahama, kulitokea vifo vya watu watano ambao walikabiliwa na ugonjwa wa kuhara na kutapika, na kusababisha Mkoa kuunda timu ya wataalamu kufuatilia tatizo hilo.

Mndeme akizungumza leo Januari 09, 2024 na Waandishi wa habari mkoani amesema vifo vya watu hao watano haikubainika moja kwa moja kwamba walikufa kwa kipindupindu.

Amesema katika wagonjwa wengine 41 ambao na wao walikuwa wakikabiliwa na ugonjwa huo wa kuhara na kutapika, baada ya kupata vipimo, 18 walibainika kuwa na kipindupindu na walipatiwa matibabu,hadi sasa wamesalia wagonjwa 5 wakiendelea na matibabu.

"Wagonjwa hawa 18 ambao wamebainika kuwa na kipindupindu, 15 wanatoka Kahama, wawili wanatoka katika Manispaa ya Shinyanga na mmoja mmoja kutoka Kishapu, natoa wito kwa wananchi wazingatie masuala ya usafi hasa kipindi hiki cha msimu wa mvua," amesema Mndeme.

Aidha, ametoa tahadhari kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuwa ili kukabiliana na ugonjwa huowanatakiwa waepuke kutumia maji yasiyochemshwa, kula matunda bila kuyaosha, kula chakula baridi, matumizi hafifu ya vyoo na kutofanya usafi wa mazingira muda wote.
 
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amesema watu 18 kati ya 41 ambao walikabiliwa na tatizo la kuhara na kutapika, wamebainika kuwa na ugonjwa wa kipindupindu mkoani humo...
Nasisitiza wasikate magogo mepesi kandokando ya barabara na vichakani,ila kwenye mashimo yaliyochimbwa rasmi nakuandaliwa kwa ajili hiyo😎
 
Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza, Dr. Sebastian Pima amesema Watu 7 wamebainika kuugua Ugonjwa wa Kipindupindu Jijini Mwanza na wengine 18 wakiendelea na uchunguzi juu ya Afya zao kutokana na kuishi au kukutana na Wagonjwa.

Pima amesema “Tulipokea Watu wawili wakiwa na dalili za Kipindupindu kutoka Mkoa wa Simiyu, wakiwa njiani kurudi walipata dalili za kuharisha na kutapika wakaenda kwenye Kituo cha Afya walivyopimwa wakakutwa na Kipindupindu”.

Ameongeza "Baada ya visa hivyo, hadi sasa tumepata jumla Wagonjwa 7, wawili tumewaruhusu. Kwenye kituo chetu cha matibabu tumebaki na Wagonjwa 5 ambao wanaendelea vizuri na matibabu.
 
Back
Top Bottom