Shindano bubu la Tsh.10,000,000/=

Shindano bubu la Tsh.10,000,000/=

kwanza utajuaje kuwa nimetumia 1000
Kabla ya kupewa hiyo milioni 10. Lazima uelezee mchakato wa uzalishaji au mzunguko wa hicho ulichokifanya mpaka kukupa zaidi ya hiyo laki Shem.
 
Yani bila kuweka hiyo buku Kwa kanji Sina hakika kama Kuna pengine otherwise uwatafute wale jamaa walioanza na nyoya Moja la kuku saiv wanamiliki kuku 20,000.
Maweee !.
Kwanini teknolojia kwa Mhindi na sio nje yake !?..
 
Hiyo buku mimi nanunua vocha dakika kama zote. Nampigia Masalu Jacob anikopeshe 20k, binti kiziwi nampanga fresh 30k naipata toka kwake, MIN-me akinipa 30k, hiyo iliyobaki leo dada anajazia tayari laki mnipe hiyo 10m nitoe 1m wagawane kesi kwisha. Na hata wiki haitasha.
Haaaaaaaaahaaaaaaaaa !..
Hii unaweza kuifanya kwa kujirudia au kuiendeleza ikawa bora kweli !?.. Huoni utakuwa na wewe kama wale jamaa wa "Network Marketing" kweli!?..
 
Wakati naua 4m4 Mzee wangu alituita na bro na kutupatia laki moja tuizalishe iwe laki mbili kwa kufanya biashara NDANI ya week moja,
Tukajumua machungwa ya elfu90 na kupeleka sokoni tuuze kwa jumla, oyaa biashara sio lelemama siku ya3 tuliyakimbia machungwa yetu.
 
Wakati naua 4m4 Mzee wangu alituita na bro na kutupatia laki moja tuizalishe iwe laki mbili kwa kufanya biashara NDANI ya week moja,
Tukajumua machungwa ya elfu90 na kupeleka sokoni tuuze kwa jumla, oyaa biashara sio lelemama siku ya3 tuliyakimbia machungwa yetu.
Pole sana. Ila upo mwanzo kutokana na mazingira yako kabisa na ukaweza. Niamini.
 
Mkuu hakuna business utaifanya Kwa buku izalishe 100k Kwa week isipokuwa Kwa kanji Tena Bado ni wewe-25%/75%-kanji.
Ndio uniambie hiyo biashara sasa unayoweza ifanya Shem!?. Usilalamike.
 
Haaaaaaaaahaaaaaaaaa !..
Hii unaweza kuifanya kwa kujirudia au kuiendeleza ikawa bora kweli !?.. Huoni utakuwa na wewe kama wale jamaa wa "Network Marketing" kweli!?..
kikubwa laki ipatikane tokana na buku
 
Toa mchanganuo
1. Elfu kumi nanunua sabuni za dr S dazani moja sh 5,000/=na dawa ya meno ya angola nusu dazani sh 5,000/= natembeza mtaani kwa miguu na silipi nauli nauza sabuni moja 1,000/= na dawa ya meno nauza 2,000/= ili zimalizike haraka nauza dawa ya meno 3,000/= nakuongeza na sabuni ya kuogea yenye kutibu magonjwa ya ngozi kama chunusi na fanasi bure. Nikiamaliza ntakuwa na 24,000/=
Siku ya pili nachukua sabuni dazani mbili kwa 10,000/= na dawa ya meno dazani moja kwa 10,000/= naongeza na lotioni za buku buku nne
Natembeza mtaani kwa masaa 8 mpaka jioni nakuwa na 52,000/=
Siku ya tatu na nunua mzigo mara dufu nalipa nauli naenda pembezoni mwa miji au vijijini kama boko au mapinga huko ndani ndani nawauzia vipodozi na dawa za ngozi hapo mpaka jioni narudi na zaidi ya laki.
Siku ya nne nanunua mzigo wa laki nachanganya na vipodozi vikali vya kuwa mweupe naenda vijiji vya mkoa wa pwani kama ikwiriri au msanga chole uzaramoni huko mzigo wa laki narudi nazaidi ya laki mbili.
Siku ya tano naongeza bidhaa, nanunua mzigo wa laki mbili hapo namix vipodozi, chaja za simu, saa na kofia naenda kilwa huko wanavuna ufuta kuna msimu wa pesa nauli yake 20,000/= nauza siku mbili narudi na laki tano. Siku ya saba napumzika nafanya ibada nafua nalala na jioni naenda kucheki mechi

2. Wiki ya pili narudia mchakato nikilenga sehemu wanakopokea hela za ufuta hapo mtaji utapanda mpaka 1,000,000/=
3. Wiki ya tatu nanunua mzigo wa laki tano, na laki tano inayobaki nachongesha kibanda cha biashara
4. Wiki ya nne nikimaliza mzigo wa laki tano nikapata 1m natoa lakitano nalipiasehemu ya kuweka kibandana laki tano inayobaki nanunua mzigo narudi chaka wanakovuna ufuta.
5. Nafungua biashara ya vipodozi na nguo kwenye kibanda changu au laki tano ya kibanda na laki tano ya kulipia sehemu ya kuweka kibanda naweza paa frem ya 1m nikaanzisha duka maeneo changamfu kama mbagala au bunju hivyo hapo ntaangalia chaguo rahisi. Kisha namweka kijana genZ auze
6. Faida nayopata kwenye umachinga nakuwa nairudisha dukani humo
7. Duka likikuwa naligawa yawe mawili, yaani duka la nguo na duka la vipodozi.
8. Maduka yakifika thamani ya 3m natoa 1m kila duka naanza kununua mazao kama ufuta au korosho au mpunga na kuuza ghalani
9. Mtaji wa mazao ukikua kufikia 10m nasajili kampuni ya kununua mazao na nakuza mtaji mpaka ufike 100m
10. Ukifika 100m nafungua chama ha ushirika nanunua uwanja na kujenga ghala la kuhifadhia nafaka zangu na za wakulima na wafanya biashara wengine na kuuza mnadani
11. Mtaji ukifika 200m nanunua mashine za kukoboa mpunga na kumamua alizeti na kuzifunga maghalani na uwapa vijana wazisimamie
12. Ikifika 500m nafungua min supermaket na baadhi ya bidhaa za viwanda vidogo navyozalisha kama mchele na mafuta ya alizeti nauza humo
13. Nikifikisha billion moja naongeza petrol station na biashara ya usafirishaji kwa kuanza na malori nabus za tata
14. Nikifika billion 2 naongeza biashara za mazao kwenda nje ya nchi kama kupeleka korosho uchina na veitnam
15. Nikifikisha billion 5, nawekeza kwenye gesi na viwanda vya chuma
16. Nikifikisha billion 10 nawekeza kwenye real estate, namiliki mijumba kuanzia kkoo, masaki, mbezi beach, mbweni na kigamboni napangisha raia.
17. Ikifika b20 najenga hotel za nyota tano kwenye majiji kama Dsm, Dom, Mwanza, Arusha na Mbeya

Kama kuna sehemu hapajaeleweka uliza swali
 
Back
Top Bottom