Shillingi ya Tanzania Yazidi Kuporomoka Thamani

mkuu ni kweli moja ya sababu sababu ukiuza nje wananunua kwa dola kwa hiyo tatizo letu tunaimport kwa kununua vitu nje kwa dola ndio maana dola imekua expensive sana na mbaya zaidi kuna baadhi ya mahoteli yanauza chakula kwa dola na kutoa huduma nyingine kwa diola na sisi hatuzalishi serikali ingekua na akili ingeimarisha nishati ya umeme na mafuta kwanza ili tuweze kuwa na viwanda vya kutosha kuzalisha na kutoa huduma kwa jamii kama vile bidhaa na ajira vinginevyo kila kukicha uchumi utazidi kuporomoka maana mgao nao umeshika kasi!
Niliwahi kusikia wachumi wanasema eti sababu mojawapo ya huo mporomoko ni kwamba: hatuuzi bidhaa zetu (i.e pamba, kahawa, katani, madini) njeya nchi kwa wingi kama tunavyonunua bidhaa toka nje......sijui km kuna ukweli ktk hilo!
 
Hizo graph zinaonyesha thamani ya euro against dollar, utaona kuwa euro ilikuwa inapada thamani mpaka mwezi mei awmbapo ilikuwa maximum,ikaanza kudondoka june mpaka sasa ni kama 1.43 against a dollar,mwezi mei(graph ya kwanza) ilikuwa almost 1.48,ila inaonyesha kuwa euro inajitahidi tena ku-rally towards kiwango cha may(may be due to greece bailout).
Graph ya pili inaonyesha uwekezaji wa Euro in long/short term basis,angalia orange na blue zinavyoshuka,against non-commercial value(kijani),graph ya pili inaonyesha jinsi Zitto alivyokuwa akiiambia serikali kuhusu kununua euro bonds badala ya gold,ambayo leo nilipoangalia markets imepanda kama 0.63 pts at the closing bell.
Perfomance ya dollar nayo inasemekana itakuwa strong especially baada ya serikali ya US ku-release mafuta kutoka kwenye reserves zake kwa ajili ya sikukuu ya uhuru wao ili kupunguza bei ya mafuta huku,hii itapunguza exports za mafuta na kungangalisha thamani ya dollar kidogo.
Kwa sisi wabeba mabox ni habari nzuri kwani tukiweka vijisenti vyetu kwenye tembo card,tutapata kafaida kadogo,ila kwa wafanyakazi wanaolipwa madafu,itakuwa kazi kidogo.
Mkuu lakini umejibu kidogo saana kuhusiana na kwanini shilingi yetu iko vile. Hivi mpango wa Euro Bond ulikuwaje? Maana maelezo yako naona yanatofautiana na hasa ninachofaham nini serikali ilitaka kufanya kuhusiana na euro bond. Ya Zitto sijayasikia naomba unifahamishe.
Kwanza ni kichekesho kama kuna madai ya kununua Euro Bond kwa sababu serikali yenyewe haina pesa. Kwahiyo ninachofaham serikali ilitaka kuraise pesa kwa kutumia Euro Bond kabla ya mtikisiko wa Uchumi. Mpango huo uliathiriwa maana masharti yangekuwa magumu na hivyo interest rate zingekuwa kubwa. Na bond ile ilikuwa inatakiwa itumike kwenye miundombinu.
Kwa gold kuna unafuu kwa sababu inapatikana nchini kama kweli tunapesa na demand yake inazidi kupata na pia inaweza kununulika kwa local currency hivyo haitaweza kuharibu urari wetu kwenyefedha za kigeni.
Tuendelee na majibu yetu kwa hali tete ya Tshs
 
Nadhani mada ni kuhusu kushuka kwa value ya Tsh wiki iliyopita,this can be explained by the forex market trend kama ilivyoonyeshwa kwenye hizo graphs.
Kuhusu kununua,hiyo nadhani nimekosea,nilikuwa namaanisha ku-issue 500USD Euro Bond.
Kuhusu Zitto,
Tanzania: Reintroduce Local Gold Reserve, Team Tells Bot (Mining.com) : BullionTalk.com
 
Asante mkuu kwa mchango wako.

Sasa kushuka kwa thamani ya Shillingi kuna uhusiano gani na mfumuko wa bei? Najua ukienda kwenye maduka mengi sasa hivi naq hasa yanayouza vitu amabavyo ni imported unakuta vitu vimepanda bei ukiwauliza wanakwambia bei ya dola imepanda hivyo wanalazimika kuongeza bei ili wapate thamani halisi ya pesa walizotumia kununua hizo bidhaa. Je ili lina ukweli wowote au watu wanajaribu kutumia nafasi hiyo kutengeneza super profit? Je kushuka thamani kwa shilingi kutakuwa na athari gani kwenye bei ya mafuta locally?

Tiba
 
Bei ya mafuta imeshuka kwenye soko ,kwa hiyo kutakuwa na effect ndogo,almost negligible....ila ni ukweli for the past two wks thamani ya dola imeongezeka,na kama ulivyoona kwenye hizo graphs,dola moja no almost 1.43 euros.
1600x1.43=2088euros.
 
Natabiri mimi Pesa ya Tanzania baada ya miaka mitano ijayo pesa yetu itakuwa kama pesa ya Congo,na Zimbabwe Makaratasi yasiyokuwa na thamani yoyote ile.

Mzizimkavu Congo ipi unazungumzia? Congo DRC...Dola moja ni sawa na faranga 900.Kuona wanabeba pesa mingi ni kwamba wao noti kubwa ni 500 so ukiwa faranga laki moja u can imagine.....labda kama congo ingine brazavile...compare na kwetu dola moja ni sawa na 1598 saa hii.
 
Asante mkuu kwa mchango wako.

Sasa kushuka kwa thamani ya Shillingi kuna uhusiano gani na mfumuko wa bei? Najua ukienda kwenye maduka mengi sasa hivi naq hasa yanayouza vitu amabavyo ni imported unakuta vitu vimepanda bei ukiwauliza wanakwambia bei ya dola imepanda hivyo wanalazimika kuongeza bei ili wapate thamani halisi ya pesa walizotumia kununua hizo bidhaa. Je ili lina ukweli wowote au watu wanajaribu kutumia nafasi hiyo kutengeneza super profit? Je kushuka thamani kwa shilingi kutakuwa na athari gani kwenye bei ya mafuta locally?

Tiba

Tiba,

Sarafu ya nchi ina thamani kutoka na mahitaji ya kutumika sarafu husika nchini. Kwahivyo, kama sarafu ya nchi ikiwa haihina mahitaji thamani ya sarafu hushuka. Quantity theory money inasema thamani ya sarafu inasababishwa na vitu viwili kwanza mfumuko wa bei nchi na kiwango cha sarafu katika mzunguko wa pesa. Tanzania shilling inashuka kutokana na kukosekana na mahitaji ya sarafu nchini, mfumuko wa bei na ufisadi.

A. Kukosekana kwa mahitaji ya sarafu nchini:

Kusema ule ukweli hili swala serikali inaonekana either imelinyamazia kimya au kuna vigogo wanafaidika nalo (hasa kwenye sekta ya nyumba mfano Dar wapangishaji hudai dollar kama malipo ya pango, au baadhi ya shule Dar nazo pia hudai ada kwa dollar). Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya sarafu ya nje nchini sarafu ya tanzania inashuka thamani. Hilo linachangia kwa kiwango kikubwa kukuwa kwa mahitaji ya sarafu za nje nchini na pia kushuka kwa thamani ya Tanzanian shillings. Ukiatazama volatility ya currency (mtiririko wa sarafu) utanyambua kwamba sarafu yetu haina stability kwani ikishuka dollar nayo inashuka, dollar ikiwa strong nayo inakuwa strong na hivyo basi utaona kuwa sarafu yetu haina thamani kama mtoto yatima inaenda popote sarafu ya kimataifa inapoelekea.

B. Mfumuko wa bei:
Mfumuko wa bei wa nchi yetu unachangiwa na mambo mawili, cost push inflation inayotokana na mfumuko wa bei ya mafuta duniani, European sovereign debt crisis, na maumivu ya mtikisiko wa sekta ya benki. Mfumuko wa bei ya mafuta duniani unaosababishwa na speculators (kwasababu Financial Times- April walitamka wazi bei halisi ya mafuta Crude Brent Oil haizidi hata $70 kwa pipa) ambao wanaipaisha bei ya mafuta kutokana na machafuko ya mashariki ya mbali (middle east). Machafuko haya hao speculators huwa wanacheza kamari ya kubadilishana bidhaa wakihofia machafuko hayo yanaweza kusababisha uhaba wa mafuta katika soko la dunia. Mategemeo ya nchi za kimagharibi yameanza kufifia kwani walitegemea hali ya amani itarejea mashariki ya mbali lakini bado haijawa shwari hasa Libya. Ndio ya kwamba International Energy Agency (IEA) walifungua reserves zao kujaribu kushusha bei ya mafuta (kwa lengo hasa kuwafaidisha marekani kwani siku za mapumziko ziko mbeleni). Pia uamuzi wa kufungua mafuta ya akiba ulikuja baada ya nchi za Opec kushindwa kufikia muafaka wa kuongeza uzalishaji wa mafuta katika soko la dunia (OPEC). Kwa ufupi bei ya mafuta imeanza kushuka kwa kasi sasa ila wanauchumi hawategemei itadumu kwani mahitaji ya mafuta yako palepale. Mfumuko wa bei ya mafuta umechangia kwa kiwango kikubwa mfumuko wa bei nchini na kufanya maisha ya watanzania kuwa bei ya juu.

Pia mfumuko wa bei umesababishwa pia kwa kukua kwa gharama za uzalishaji nchini kutokana na kukosekana na nishati ya umeme nchini. waziri wa nishati wakati akicheza makida makida gharama za uzalishaji zimekuwa zikiongezeka kuchangia mfumuko wa bei kwa kiwango kikubwa. Jambo hili linaweza kutatulika kama utapatikana umeme wa uhakika nchini.

Pia mfumuko wa bei umechangiwa na kuongezeka kwa purchasing power ya watanzania (demand pull). Serikali ya mkapa walijitahidi na kufanikiwa kupunguza mfumuko wa bei unaotokana na demand pull. Kama umerudia kumbukumbu zako mishahara ya mtanzania wakati wa mkapa ilikuwa haipandi ovyo na hivyo kusaidia kwa kiwango cha aina fulani kushuka kwa kasi ya mfumuko wa bei. Serikali ya Kikwete imekuwa ikiongeza mishahara kila kukicha na kuchangia kuongezeka kwa kiwango cha purchasing power ya mtanzania. Hivyo basi, kumeongeza gharama za maisha ya kufumua mfumuko wa bei nchini. Kuongezeka kwa gharama za uzalishaji, uwezo wa mtanzania kununua kumechangia kukuza mfumuko wa bei na hivyo kusababisha thamani ya shillingi kuporomoka.

Mtikisiko wa madeni ya nchi hasa kwa nchi za ulaya pia umechangia kuwapo na mabadiliko yasitabirika ya sarafu katika ulimwengu (Volatility). Hilo linatokana na hofu ya kuvunjika kwa Umoja wa nchi za ulaya, contagion effect ya greece hasa kwa nchi za spain, Italy, Ireland na Portugal. Pia debt risk exposure kwa benki za US, UK na Hongo Kong na China. Kutokana na hilo utagundua sarafu za Asia zimekuwa zikipanda thamani sana kuliko za ulaya kutoka na wasiwasi uliopo sasa hasa kutokana na kile kinachoendelea Ugiriki na Ulaya nzima. Kwetu hatujasalimika kwani sarafu yetu imeunganishwa na US dollar (currency peg) na basi utagundua sarafu yetu leo imeamka hivi kesho imeamka vile.

Pia kuporomoka kwa sekta ya viwanda na kupungua kwa mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya nchi na kudorora kwa bei za malighafi za kilimo kama katani, kahawa nk. kumechangia kwa kiwango kikubwa kuwapo kwa uhaba wa sarafu nchini. Sekta ya viwanda imekufa kabisa kiasi kwamba nchi yetu imekuwa ikitegemea bidhaa za nje badala za nchini hadi vyakula na kupelekea kuwapo na mfumuko wa bei nchini. na uhaba sarafu za kigeni.

C. Ufisadi:
Ufisadi una mchango wa kiasi kikubwa kuporomoka kwa sarafu nchini. Niliwahi kusema nyuma kwamba ukitaka kujua thamani sarafu imeshuka kwa kiasi kikubwa chukua taarifa za sarafu BOT (Refer to their website). Ukiziweka katika Excel ukatengeneza graph utaona trend ya thamani ya shillingi iliporomoka kwa kiasi kikubwa miaka ya 2005-2006. Miaka hii ndio majanga ya ufisadi kama EPA yaliitikisa nchi, BOT twin tower, na madudu mengineyo. Hii trend ya kuporomoka sarafu ya nchi miaka hii wakati kulikuwa hakuna mtikisiko wa kiuchumi duniani wala mfumuko wa bei ya mafuta unapelekea kupata jibu moja la kwamba sarafu ya nchi thamani yake ilikuwa inaporomoka kutokana na watu kuwa wananunua dollar, pound kwa kiwango kikubwa ili either wasafirishe nje ya nchi (capital flight). Waliokuwa wakifanya ufisadi walikuwa either wakinunua dollar kwa wingi nchini au wakizisafirisha kwa kutumia njia ya fedha nje ya nchi.

BOT inafanya nini?
Binafsi naona BOT hawana wanalolifanya kuokoa shillingi kwasababu kwa tamko la Benno ndulu (nimekata tamaa kumuita professor ameniangusha sana) naona wamekuwa wanajaribu kutafuta sababu za kuhalalisha sarafu kwanini inashuka badala ya kushukulikia hilo jambo.

Nini kifanyike:
A. Ununuzi wa dhahabu:
Namuunga mkono Zitto kabwe pendekezo lake la kununua dhahabu kwani katika soko la sasa na matatizo ya madeni. bei ya dhahabu imekuwa ikipanda mno. Hili jambo litachangia kuifanya sarafu iwe na thamani kwani italinganishwa na kiwango cha dhahabu nchi inayo katika reserves. Ni vema BOT wapunguze reserve za dollar kwani dollar inashuka thamani na forecast zinaonyesha uchumi wa marekani haukui ilivyokuwa inategemewa. Pia matatizo ya madeni ya nchi yamesababisha kushuka thamani za sarafu ya Euro na sterling pound. Ni vema tupunguze ukubwa reserves za foreign currencies na kuongeza kiwango cha dhahabu nchini.

b. Kupunguza matumizi ya foreign currency nchini:
Dollarisation inabidi kutomezwa venginevyo thamani ya shillingi nchini itaendelea kuporomoka.

c. Kutokomeza ufisadi:
Kutasaidia kupunguza mahitaji ya fedha za kigeni na kupelekea sarafu yetu kuimarika.

d. Tax reduction:
Kupunguza kodi katika sekta ya mafuta kutapunguza mfumuko wa bei na kupunguza gharama za uzalishaji.

e. Umeme wa uhakika utasaidia kuongeza uhai wa sarafu na kupunguza gharama za maisha nchini.

f. Kujaribu kutokuongeza mshahara badala yake wapunguze kodi ya makato ya mshahara. Hilo litasaidia kupunguza purchasing power ya mtanzania nchini.

Natumai nimekufunua kidogo Mkuu.

Nilikuwapo!!!
 
Nadhani mada ni kuhusu kushuka kwa value ya Tsh wiki iliyopita,this can be explained by the forex market trend kama ilivyoonyeshwa kwenye hizo graphs.
Kuhusu kununua,hiyo nadhani nimekosea,nilikuwa namaanisha ku-issue 500USD Euro Bond.
Kuhusu Zitto,
Tanzania: Reintroduce Local Gold Reserve, Team Tells Bot (Mining.com) : BullionTalk.com
Nashukuru angalau sasa tunaweza kujadili mada iliyopo mbele yetu. Ukweli katika graph yako ile explanations ya Euro ilikuwa irrelevant. Why? Kwasababu uchumi wetu upo dolarised na hizo exchange rates za Euro na Pound zinakuwa driven na value ya dollar kwa Tanzania. Yaani ukishafaham dollar value yake ni ipi against Tshs then utaelewa value ya currency nyingine. Otherwise graphs zako zina complicate simple explanation ya tatizo letu.
Ukweli hatuzalishi bidhaa za kuuza nje na pia matumizi yetu kwa bidhaa za nje yameongezeka saana. Kama utakumbuka baada ya migogoro ya mashariki ya Kati kuanza Spain waliamua kupunguza spidi za magari kwenye highways kutoka 120km/hr to 110. Lengo hasa likiwa kusave fedha yao ya kigeni kwenye kununua mafuta ambayo yaliongezeka kasi kwa hali ya juu saana. Baada ya bei kupungua wamerejesha ile spidi kwenye highways. Wao wanasema kitendo cha kufanya hivyo kwa muda wa miezi mitatu kimesave kiasi cha zaidi ya $300mil. Kuanzia hapo, unaweza kufikiria namna foleni zinavyofilisi uchumi wetu, uagizaji wa vyakula ambavyo tungeweza kuzalisha toka nje unavyotumaliza na bado rushwa.
Kwahiyo, utaona kwamba licha ya madai ya ongezeko la thamani ya dollar shilingi yetu imepungua saana. Ushahidi wa currency nyingine zinazofanya unaweza kuthibitisha ni kwa kiasi gani Tanzania yetu imeshindwa kuweka misingi ya kueleweka kwenye matumizi ya fedha za kigeni. Kuendelea kufanyabiashara zetu,, nchini kwetu kwa pesa za wageni hili nalo ni tatizo kubwa saana. Tunawaogopa mno wawekezaji!!!
 
Mzizimkavu Congo ipi unazungumzia? Congo DRC...Dola moja ni sawa na faranga 900.Kuona wanabeba pesa mingi ni kwamba wao noti kubwa ni 500 so ukiwa faranga laki moja u can imagine.....labda kama congo ingine brazavile...compare na kwetu dola moja ni sawa na 1598 saa hii.
Tahadhari nyingine katika mjadala huu ni kwamba; kuwa na strong exchange rates hakumaanishi uchumi wa nchi husika ni mzuri. Kwahiyo kuna factor nyingine zinapaswa kuzingatiwa.
 
Bei ya mafuta imeshuka kwenye soko ,kwa hiyo kutakuwa na effect ndogo,almost negligible....ila ni ukweli for the past two wks thamani ya dola imeongezeka,na kama ulivyoona kwenye hizo graphs,dola moja no almost 1.43 euros.
1600x1.43=2088euros.
Kaka naona unarefer Euro peke yake na kwa saana. Ni bora basi utengeneze basket of major currencies ndio iwe kielelezo. Uchumi wa hiyo currency sasa hivi ni very fragile. Well kutoka kwenye peak mafuta mwezi April, 2011 achana na ile ya kabla ya mtikisiko wa dunia, mafuta yalikuwa yanauzwa dollar 127 na wiki iliyopita kwenye closing bell ilikuwa roughly 105. Hiyo ni change ya 17%. Lakini ukitumia indicative rates za BOT against US dollar utaona dollar ili-appreciate kutoka 1509 kwenda 1568 ambayo ni 3%. Kwahiyo net effect, assume mambo mengine constant, Utaona implictly mafuta yalitakiwa yawe yamepungua kwa asilimia angalau 15% toka kwenye peak. Yaani kama watu walilipa 2000 angalau sasa hivi tunatarajia yawe kwenye 1700-1800. Lakini ukiondoka na ilo punguzo la kodi ya serikali, utaona mafuta yanatakiwa yawe nafuu zaidi.
 
Asante mkuu kwa mchango wako.

Sasa kushuka kwa thamani ya Shillingi kuna uhusiano gani na mfumuko wa bei? Najua ukienda kwenye maduka mengi sasa hivi naq hasa yanayouza vitu amabavyo ni imported unakuta vitu vimepanda bei ukiwauliza wanakwambia bei ya dola imepanda hivyo wanalazimika kuongeza bei ili wapate thamani halisi ya pesa walizotumia kununua hizo bidhaa. Je ili lina ukweli wowote au watu wanajaribu kutumia nafasi hiyo kutengeneza super profit? Je kushuka thamani kwa shilingi kutakuwa na athari gani kwenye bei ya mafuta locally?

Tiba
Ndugu yangu kinachotokea simply kwamba, ili waagize bidhaa zilezile kwa supplier yuleyule inamaana watahitaji Tshs nyingi zaidi kwa dola zilezile. Kwahiyo, ili na wao waje wauze kwa faida itabidi wawachaji watu bei kubwa na kwa kuwa wanauza kwa Tshs inamaana watu watalipa zaidi.
 
Mkuu, miaka mitano mingi kama tukienda kwa trend hii ya sasa. Hali inatisha!!!

Tiba

Kwa speed hii si ajabu ikifika mwisho mwa mwaka 1 U$ ikawa sawa na T shs 1,800 au hata zaidi. Nadhani demand ya U$ imeongezeka sana kutokana na dollarization ya uchumi wetu. Kwa mfano wenye nyumba wengi sasa hivi hawapokei kodi ya nyumba kwa pesa za madafu kinyume na miaka iliyopita na pia mahotel mengi sasa hivi katika miji mbali mbali ikiwemo Dar, Arusha, Mwanza, Morogoro, Kilimanjaro, Zanzibar n.k. wanakubali malipo kwa kutumia dollar tu ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo malipo katika hotel hizo yaliweza kufanyika katika pesa za madafu. Hali hii imeongeza kwa kiasi kikubwa demand ya U$ na hivyo kuifanya thamani ya shilingi yetu iporomoke katika speed ya kutisha.

Soma hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...x-transactions-in-tanzania-govt-to-act-2.html
 
Tiba,

Sarafu ya nchi ina thamani kutoka na mahitaji ya kutumika sarafu husika nchini. Kwahivyo, kama sarafu ya nchi ikiwa haihina mahitaji thamani ya sarafu hushuka. Quantity theory money inasema thamani ya sarafu inasababishwa na vitu viwili kwanza mfumuko wa bei nchi na kiwango cha sarafu katika mzunguko wa pesa. Tanzania shilling inashuka kutokana na kukosekana na mahitaji ya sarafu nchini, mfumuko wa bei na ufisadi.

A. Kukosekana kwa mahitaji ya sarafu nchini:

Kusema ule ukweli hili swala serikali inaonekana either imelinyamazia kimya au kuna vigogo wanafaidika nalo (hasa kwenye sekta ya nyumba mfano Dar wapangishaji hudai dollar kama malipo ya pango, au baadhi ya shule Dar nazo pia hudai ada kwa dollar). Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya sarafu ya nje nchini sarafu ya tanzania inashuka thamani. Hilo linachangia kwa kiwango kikubwa kukuwa kwa mahitaji ya sarafu za nje nchini na pia kushuka kwa thamani ya Tanzanian shillings. Ukiatazama volatility ya currency (mtiririko wa sarafu) utanyambua kwamba sarafu yetu haina stability kwani ikishuka dollar nayo inashuka, dollar ikiwa strong nayo inakuwa strong na hivyo basi utaona kuwa sarafu yetu haina thamani kama mtoto yatima inaenda popote sarafu ya kimataifa inapoelekea.

B. Mfumuko wa bei:
Mfumuko wa bei wa nchi yetu unachangiwa na mambo mawili, cost push inflation inayotokana na mfumuko wa bei ya mafuta duniani, European sovereign debt crisis, na maumivu ya mtikisiko wa sekta ya benki. Mfumuko wa bei ya mafuta duniani unaosababishwa na speculators (kwasababu Financial Times- April walitamka wazi bei halisi ya mafuta Crude Brent Oil haizidi hata $70 kwa pipa) ambao wanaipaisha bei ya mafuta kutokana na machafuko ya mashariki ya mbali (middle east). Machafuko haya hao speculators huwa wanacheza kamari ya kubadilishana bidhaa wakihofia machafuko hayo yanaweza kusababisha uhaba wa mafuta katika soko la dunia. Mategemeo ya nchi za kimagharibi yameanza kufifia kwani walitegemea hali ya amani itarejea mashariki ya mbali lakini bado haijawa shwari hasa Libya. Ndio ya kwamba International Energy Agency (IEA) walifungua reserves zao kujaribu kushusha bei ya mafuta (kwa lengo hasa kuwafaidisha marekani kwani siku za mapumziko ziko mbeleni). Pia uamuzi wa kufungua mafuta ya akiba ulikuja baada ya nchi za Opec kushindwa kufikia muafaka wa kuongeza uzalishaji wa mafuta katika soko la dunia (OPEC). Kwa ufupi bei ya mafuta imeanza kushuka kwa kasi sasa ila wanauchumi hawategemei itadumu kwani mahitaji ya mafuta yako palepale. Mfumuko wa bei ya mafuta umechangia kwa kiwango kikubwa mfumuko wa bei nchini na kufanya maisha ya watanzania kuwa bei ya juu.

Pia mfumuko wa bei umesababishwa pia kwa kukua kwa gharama za uzalishaji nchini kutokana na kukosekana na nishati ya umeme nchini. waziri wa nishati wakati akicheza makida makida gharama za uzalishaji zimekuwa zikiongezeka kuchangia mfumuko wa bei kwa kiwango kikubwa. Jambo hili linaweza kutatulika kama utapatikana umeme wa uhakika nchini.

Pia mfumuko wa bei umechangiwa na kuongezeka kwa purchasing power ya watanzania (demand pull). Serikali ya mkapa walijitahidi na kufanikiwa kupunguza mfumuko wa bei unaotokana na demand pull. Kama umerudia kumbukumbu zako mishahara ya mtanzania wakati wa mkapa ilikuwa haipandi ovyo na hivyo kusaidia kwa kiwango cha aina fulani kushuka kwa kasi ya mfumuko wa bei. Serikali ya Kikwete imekuwa ikiongeza mishahara kila kukicha na kuchangia kuongezeka kwa kiwango cha purchasing power ya mtanzania. Hivyo basi, kumeongeza gharama za maisha ya kufumua mfumuko wa bei nchini. Kuongezeka kwa gharama za uzalishaji, uwezo wa mtanzania kununua kumechangia kukuza mfumuko wa bei na hivyo kusababisha thamani ya shillingi kuporomoka.

Mtikisiko wa madeni ya nchi hasa kwa nchi za ulaya pia umechangia kuwapo na mabadiliko yasitabirika ya sarafu katika ulimwengu (Volatility). Hilo linatokana na hofu ya kuvunjika kwa Umoja wa nchi za ulaya, contagion effect ya greece hasa kwa nchi za spain, Italy, Ireland na Portugal. Pia debt risk exposure kwa benki za US, UK na Hongo Kong na China. Kutokana na hilo utagundua sarafu za Asia zimekuwa zikipanda thamani sana kuliko za ulaya kutoka na wasiwasi uliopo sasa hasa kutokana na kile kinachoendelea Ugiriki na Ulaya nzima. Kwetu hatujasalimika kwani sarafu yetu imeunganishwa na US dollar (currency peg) na basi utagundua sarafu yetu leo imeamka hivi kesho imeamka vile.

Pia kuporomoka kwa sekta ya viwanda na kupungua kwa mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya nchi na kudorora kwa bei za malighafi za kilimo kama katani, kahawa nk. kumechangia kwa kiwango kikubwa kuwapo kwa uhaba wa sarafu nchini. Sekta ya viwanda imekufa kabisa kiasi kwamba nchi yetu imekuwa ikitegemea bidhaa za nje badala za nchini hadi vyakula na kupelekea kuwapo na mfumuko wa bei nchini. na uhaba sarafu za kigeni.

C. Ufisadi:
Ufisadi una mchango wa kiasi kikubwa kuporomoka kwa sarafu nchini. Niliwahi kusema nyuma kwamba ukitaka kujua thamani sarafu imeshuka kwa kiasi kikubwa chukua taarifa za sarafu BOT (Refer to their website). Ukiziweka katika Excel ukatengeneza graph utaona trend ya thamani ya shillingi iliporomoka kwa kiasi kikubwa miaka ya 2005-2006. Miaka hii ndio majanga ya ufisadi kama EPA yaliitikisa nchi, BOT twin tower, na madudu mengineyo. Hii trend ya kuporomoka sarafu ya nchi miaka hii wakati kulikuwa hakuna mtikisiko wa kiuchumi duniani wala mfumuko wa bei ya mafuta unapelekea kupata jibu moja la kwamba sarafu ya nchi thamani yake ilikuwa inaporomoka kutokana na watu kuwa wananunua dollar, pound kwa kiwango kikubwa ili either wasafirishe nje ya nchi (capital flight). Waliokuwa wakifanya ufisadi walikuwa either wakinunua dollar kwa wingi nchini au wakizisafirisha kwa kutumia njia ya fedha nje ya nchi.

BOT inafanya nini?
Binafsi naona BOT hawana wanalolifanya kuokoa shillingi kwasababu kwa tamko la Benno ndulu (nimekata tamaa kumuita professor ameniangusha sana) naona wamekuwa wanajaribu kutafuta sababu za kuhalalisha sarafu kwanini inashuka badala ya kushukulikia hilo jambo.

Nini kifanyike:
A. Ununuzi wa dhahabu:
Namuunga mkono Zitto kabwe pendekezo lake la kununua dhahabu kwani katika soko la sasa na matatizo ya madeni. bei ya dhahabu imekuwa ikipanda mno. Hili jambo litachangia kuifanya sarafu iwe na thamani kwani italinganishwa na kiwango cha dhahabu nchi inayo katika reserves. Ni vema BOT wapunguze reserve za dollar kwani dollar inashuka thamani na forecast zinaonyesha uchumi wa marekani haukui ilivyokuwa inategemewa. Pia matatizo ya madeni ya nchi yamesababisha kushuka thamani za sarafu ya Euro na sterling pound. Ni vema tupunguze ukubwa reserves za foreign currencies na kuongeza kiwango cha dhahabu nchini.

b. Kupunguza matumizi ya foreign currency nchini:
Dollarisation inabidi kutomezwa venginevyo thamani ya shillingi nchini itaendelea kuporomoka.

c. Kutokomeza ufisadi:
Kutasaidia kupunguza mahitaji ya fedha za kigeni na kupelekea sarafu yetu kuimarika.

d. Tax reduction:
Kupunguza kodi katika sekta ya mafuta kutapunguza mfumuko wa bei na kupunguza gharama za uzalishaji.

e. Umeme wa uhakika utasaidia kuongeza uhai wa sarafu na kupunguza gharama za maisha nchini.

f. Kujaribu kutokuongeza mshahara badala yake wapunguze kodi ya makato ya mshahara. Hilo litasaidia kupunguza purchasing power ya mtanzania nchini.

Natumai nimekufunua kidogo Mkuu.

Nilikuwapo!!!
Mkuu kwenye bold arguments zako zinaonekana hazisemi hasa hizo kodi zikipunguzwa, alternatives ya serikali kwenye mapato ni ipi? Ukipunguza PAYE na nyinginezo kwenye mshahara ni kupunguza mapato kwa serikali, unacover zipi gaps hizo? Obviously utaenda kukopa na siku ya kulipa ni fedha ya kigeni!!!!!
Uchumi wa Kimarekani licha ya kwamba unadeni la takribani Usd trillions lakini kwa sasa hivi umeanza kupumua na ndio maana unaona pesa yao licha ya reserve ya mafuta ili appreciate vilivyo. Hilo la dhahabu kuifanya ndio bases, its ok lakini tukumbuke hakuna guarantee kwamba dhahabu itaendelea kupanda tu moja kwa moja. Huwa kuna turning point.
Lakini mwisho umesema speculators wanacheza kamari? Unamaanisha gamblers??????
 
Mkuu sana Anfaal,
Wazo la kupunguza kodi badala ya kuongeza mishahara is a bullet proof measure ya ku-curb inflation in a sense kwamba wanaweza kuongeza mishahara bila kutuonyesha source ya mapato ambayo watatumia kungeza mshahara (kuchapisha fedha?).Wapunguze kodi hasa kwa wafanyakazi wa ngazi za kati,too much money in people's hands drives inflation.
Kuhusu kupunguza kodi ya mafuta,sidhani kama ni jambo zuri,wajaribu ku supress aggregate demand.Mafuta tanzania yanatumiwa kiholela sana,sioni kwanini jiji kama la Dar watu wanatumia sana mafuta kwenda city,centre..mind you,Dar ina 10% of the population.HOV(High Occupancy Vehicles) zitumike zaidi kusafirisha watu jijini,tukataze magari yanayobeba mtu mmoja kwenda mjini during peak hrs,na magari ya serikali yaonyeshe mfano kwa kukataliowa kuendeshwa jumamosi na jumapil.
Watoze customs kubwa kwa wanaoagiza magari ya zamani na magari yanayotumia mafuta mengi,SUVs,etc na wapunguze au wasamehe customs,hybrid cars (they are getting really popular here in US).
 
Mkuu kwenye bold arguments zako zinaonekana hazisemi hasa hizo kodi zikipunguzwa, alternatives ya serikali kwenye mapato ni ipi? Ukipunguza PAYE na nyinginezo kwenye mshahara ni kupunguza mapato kwa serikali, unacover zipi gaps hizo? Obviously utaenda kukopa na siku ya kulipa ni fedha ya kigeni!!!!!
Uchumi wa Kimarekani licha ya kwamba unadeni la takribani Usd trillions lakini kwa sasa hivi umeanza kupumua na ndio maana unaona pesa yao licha ya reserve ya mafuta ili appreciate vilivyo. Hilo la dhahabu kuifanya ndio bases, its ok lakini tukumbuke hakuna guarantee kwamba dhahabu itaendelea kupanda tu moja kwa moja. Huwa kuna turning point.
Lakini mwisho umesema speculators wanacheza kamari? Unamaanisha gamblers??????
Mkuu,

Kama alivyokwishatamka Kobello kupunguza kodi particularly PAYE kutasaidia kupunguza kiwango cha makato ya mishahara ya wafanyakazi kwa sasa. Unapopunguza kodi mfano kwasasa inakaribia asilimia 29 au 27 wakashusha hadi asilimia 20-25 kutaongeza take home ya mfanyakazi wa kati na kawaida nchini ambao ndio wachangiaji wakubwa katika consumer spending nchini. Serikali kwasasa inaongeza tu mishahara kama daladala na athari ya kuongezeka mshahara ni kuongeza government expenditure which subsequently kunapelekea kuwapo na budget deficit nchini.

Kodi itakapotea kwa wafanyakazi inaweza kufidia na kodi ya madini (hili sitalizungumzia kwa undani kwani mkuu hapa JF tunaelimishana tu na sio kuingia technical). Ila kwa kukusaidia Australia walianzisha kodi kama hiyo ukipata muda itafute. Pia tupunguze misamaha ya kodi nchini kuongeza pato la nchi. Ni wakati muafaka haya makampuni makubwa yaanze kulipa kodi badala ya kuendelea kuwanyonya watanzania.

Vilevile kodi inaweza kuongezwa katika bidhaa za anasa hasa magari ya 4x4, magari ya aghali ili kupunguza msongamano wa mijigari isiyo na maana nchini. Wanaweza pia kuingiza vitu kama congestion charges kwa magari makubwa yanaoenda jijini kama Dar-es-Salaam, Mwanza. Kuongeza mapato ya nchi.

Pia wanaweza kuanzisha kodi ya binafsi ikiwalenda wapangishaji holela waliojaa nchini. Kariakoo wamejenga maghorofa na watu wanapangishwa kwenye nyumba hizo hakuna mtu anayelipa kodi, kuna wapangishaji wa nyumba za kulala, nyumba za kuishi wote hawa wanatakiwa kulipa kodi hawalipi. Kwa njia hiyo utagundua tutaweza kufidia kodi inayopotea katika PAYE kwa kodi hizo zote nilizozitaja hapo juu.

Kuhusu makusanyo dhahabu, dhahabu ni valuable assets katika masoko ya mitaji zinaitwa valuable securities. Ijapokuwa thamani yake huwa na kupanda na kushuka lakini dhahabu iko stable kulinganisha mabadiliko ya thamani ya sarafu. Pia katika ulimwengu uliopo sasa duniani sijaona bado sarafu iliyo na thamani tunayoweza kusema inaweza kuireplace US dollar. Hiyo ni kwasababu Marekani bado ni taifa kubwa kwa uchumi na wanayumba kwa sasa. China ilitarajiwa kuwa taifa mbadala lakini tatizo la housing bubble, inflation, unequal distribution of income, na sababu nyenginezo zinachangia kuweka katika maswali mengi kuliko majibu kuhusu utumiaji renimbi kama sarafu ya amani (safe heaven).

Pound na Euro zina sumu ya madeni, concentrated economy (tofauti na marekani) vitu vinavyoifanya kukosa sifa za kuwa a stable foreign currencies. Dhahabu watu wanaihitaji na itaendelea kutumika hata iweje labda dunia nzima uchumi uanguke kabisa. Kwakuwa mungu ametubariki na dhahabu nchi hivyo ikusanywe kuipandisha thamani sarafu ya shillingi nchini.

Speculators ni wacheza kamari tu tofauti yao ni kwamba uchezaji kamari wao uko katika masoko ya mitaji. Kwa kutumia claims mbali mbali wamekuwa wakichangia kwa kiwango kikubwa kuharibu uchumi wa dunia. Wanaweka bet katika thamani ya asset ambayo haipo na wala haitegemewi kuzalishwa leo wala kesho kama sio kamari hiyo ni nini???

Kuhusu kodi ya mafuta hiyo suala la muda mfupi kukabiliana na msukumo wa bei ya mafuta duniani.

Mchango wangu wa mwisho hapa.
 
Kila siku pesa inashuka thamani na c kusudio la serikali ila ni mipango mibovu ya serikali laiti wangelikuwa na mipango bora tangu miaka 20 iliyopita,viwanda na vitega uchumi vilivyo kuwepo au vilivyo wekwa vingelikuwa mbali badala ya kufa.Ukweli unataka pesa ipande thamani uza bidhaa kamili zaidi nje(finished goods),lakini kutokana na usimamizi mbovu hata sasa pia kukosa uzalendo viwanda na vitega uchumi vingi vishakufa na vilivyopo vinayumba na baadhi vimebinafsishwa kwa makubaliano mabovu yaani 20% kwa 80%.
 
Back
Top Bottom