Shillingi ya Tanzania Yazidi Kuporomoka Thamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shillingi ya Tanzania Yazidi Kuporomoka Thamani

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Tiba, Jun 25, 2011.

 1. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Wadau,

  Jana nilijaribu kufuatilia thamani ya pesa yetu dhidi ya pesa za kigeni na nilichogundua ni kwamba shilingi inapoteza thamani yake kwa kasi ya ajabu. Wiki tatu zilizopita on average kwa mfano USD 1 = Tshs 1,490 lakini kwa exchange rate za jana 1 USD = Tshs. 1,600 on average. Kwa upande wa Euro, Euro 1 = 2,180 on average lakini jana 1 Euro = 2,270.

  Hivi kuna anayeweza kutupa maelezo ya kitaalamu ni kwanini pesa yetu inashuka thamani kwa kasi ya namna hiyo? Je wenzetu wa BOT wanachukua hatua gani kukabiliana na hali hii?

  Tiba
   
 2. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Niliwahi kusikia wachumi wanasema eti sababu mojawapo ya huo mporomoko ni kwamba: hatuuzi bidhaa zetu (i.e pamba, kahawa, katani, madini) njeya nchi kwa wingi kama tunavyonunua bidhaa toka nje......sijui km kuna ukweli ktk hilo!
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ndulu amesema tuuze nje na uchumi utapanda
   
 4. K

  KAMALELA JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Kaka mbona bado naitaendelea kushuka thamani, kwasasa tunaagiza Fuel kwa wingi sana kwa matumizi ya jenereta majumbani mwetu na maofisini ambapo kama kungekuwa na umeme hiyo demand ya kupeleka pesa za kigeni nje isingekuwa kubwa kiivyo, ninachokiona mimi kwasasa ni ukosefu wa sera na usimamizi mzuri wa kukuza uchumi wetu. kumbuka rais akisafiri inatumika pesa ya kigeni, wale wabunge walikwenda kubembeleza pesa za BAE wanatumia pesa za kigeni.


  Tupige magoti tuombe Mungu.... awape hekima viongozi wetu hawa!
   
 5. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tuexport rushwa pato la kigeni litaongezeka
   
 6. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Ngoja tusubiri wataalamu wa haya mambo waamke waje watueleze kwa kina hapa. Hizo theory za demand and supply wakati mwingine tuzisingizia tu!!!

  Tiba
   
 7. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Huyu Ndulu mwaka jana au juzi alipata tuzo gani sijui kwa kuisadia pesa yetu isishuke thamani sana, sasa hizo mbinu alizotumia wakati huo mbona hazitumii tena mwaka huu? Hii hali inatisha sana. Soon tutaanza kutembea na makapu ya pesa kama rafiki zetu Zimbabwe maana wallet zitakuwa haziwezi kutosha tena.

  Tiba
   
 8. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Jamani mbavu zangu!!!!!! Yes we are good at it and may be we should start exporting.......LOL

  Tiba
   
 9. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Ninaweza kukubaliana na wewe kwani kukosekana kwa umeme wa uhakika ni tatizo na mwiba mkali kwenye uchumi wetu lakini viongozi wetu ili hawalioni hata kidogo. Na wala halipewi kipaumbele kwani kwenye bajeti ya juzi zimetengwa pesa kiduchu kwa ajili ya mradi wa megawati 160 tu. Waziri wetu Ngeleja kazi ni kuonekana kwenye nyumba za starehe usiku akiwa na vimwana hana muda wa kufikiria ni jinsi gani tuepuke ili tatizo la umeme.

  Kwetu kuna usemi kwamba "Mungu mbela, naiwe agawe otaileo" which literary means that you should invest your own efforts while at the same time praying and asking God's help. Tusitarajie kwamba sala tu zitatusaidia kuwafanya viongozi wetu waelewe na kuanza kuwatumikia wananchi kama inavyopashwa. Tunapashwa kupiga hatua mbele zaidi kuwaondoa madarakani walafi na wazembe hawa!!!!

  Anyway, Mungu ibariki Tanzania.

  Tiba
   
 10. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 280
  Wakuu hii kitu inatisha,ila kuhusu euro naona kama kuna mchakachuo.
  Thamani ya dola imepanda,especially against the Euro na wanajitahidi kui mess up yuan kidizaini....nilifanikiwa kuona interview ya Geithner,kwenye CNBC leo......we need to brace ourselves.

  [​IMG] One-sided sentiment extremes in Euro/US Dollar options risk reversals have coincided with a noteworthy EURUSD bottom and call for further strength. Our risk reversal percentiles showed that FX Options traders had grown the most aggressively bearish the EURUSD in the past quarter. Such sentiment extremes have come on important price bottoms and tops in recent years, and this particular instance is so far no exception.
  Source:DailyFx.com
   
 11. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu hebu tutafisirie kwa lugha rahisi, hizo graph zinatwambia nini?

  Natanguliza shukrani.

  Tiba
   
 12. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 280
  Hizo graph zinaonyesha thamani ya euro against dollar, utaona kuwa euro ilikuwa inapada thamani mpaka mwezi mei ambapo ilikuwa maximum,ikaanza kudondoka june mpaka sasa ni kama 1.43 against a dollar,mwezi mei(graph ya kwanza) ilikuwa almost 1.48,ila inaonyesha kuwa euro inajitahidi tena ku-rally towards kiwango cha may(may be due to greece bailout).
  Graph ya pili inaonyesha uwekezaji wa Euro in long/short term basis,angalia orange na blue zinavyoshuka,against non-commercial value(kijani),graph ya pili inaonyesha jinsi Zitto alivyokuwa akiiambia serikali kuhusu kununua euro bonds badala ya gold,ambayo leo nilipoangalia markets imepanda kama 0.63 pts at the closing bell.
  Perfomance ya dollar nayo inasemekana itakuwa strong especially baada ya serikali ya US ku-release mafuta kutoka kwenye reserves zake kwa ajili ya sikukuu ya uhuru wao ili kupunguza bei ya mafuta huku,hii itapunguza exports za mafuta na kungangalisha thamani ya dollar kidogo.
  Kwa sisi wabeba mabox ni habari nzuri kwani tukiweka vijisenti vyetu kwenye tembo card,tutapata kafaida kadogo,ila kwa wafanyakazi wanaolipwa madafu,itakuwa kazi kidogo.
   
 13. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu asante kwa ufafanuzi. Nakutakia ubebaji mabox mwema!!!!!

  Tiba
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Natabiri mimi Pesa ya Tanzania baada ya miaka mitano ijayo pesa yetu itakuwa kama pesa ya Congo,na Zimbabwe Makaratasi yasiyokuwa na thamani yoyote ile.
   
 15. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu
   
 16. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kwa mwenendo huu, benki kuu ni lazima ichapishei noti za shilingi 50,000 na shlingi 100,000 mwaka huu.

  Kuanzia mwaka ujao hadi 2015 zitakuwepo noti za shs. 500,000 na 1,000,000
   
 17. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 280
  Tutafanya jambo la maana kama tutapunguza matumizi ya mafuta kwa njia mbili,kupnguza wingi wa matumizi,na at the same time kuongeza ufanisi (efficiency) kwenye uzalishaji.
  Pia ingekuwa ni vizuri sana tukitaifisha migodi yote ya dhahabu.
   
 18. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu, miaka mitano mingi kama tukienda kwa trend hii ya sasa. Hali inatisha!!!

  Tiba
   
 19. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu tutapunguzaje matumizi ya mafuta na kuongeza ufanisi wakati sasa mgao ni 24 hours kwa siku? Hivi Ngeleja anasubiri nini kujiuzulu? Wanazidi kudidimiza uchumi wa nchi kwa mtindo huu.

  Tiba

  Tiba
   
 20. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu, huko ndiko tunakoelekea!!!!

  Tiba
   
Loading...