sibusiso dlomo
JF-Expert Member
- Apr 23, 2016
- 691
- 386
kwanini GDP yetu inaonekana inakuwa while mitaani na biashara nyingi zimezorota sana. huu ni kutokana na maono yangu maana nadhani watu wamekuwa wanaangalia sana kwenye ECONOMIC GROWTH kuliko ECONOMIC DEVELOPMENT. economic growth ni kuangalia ukuaji wa uchumi kwa kuangalia sector zinazojumlisha consumption, investment, goverment saving export and importKwanza umeniuliza uchumi wa Tanganyika unakua ktk sector gani nimekutajia ambazo ni sector za Mabank,Usafirishaji,Utalii na Madini nikakambia ktk sector hizo zinachukua watu wachache sana so kuona impact mpaka kwa mwananchi wa kawaida Manzese ni vigumu sana nikasema kuwa Dunian sector ambayo ni uti wa mgongo wa ukuaji bora wa uchumi ambao kuanzia tajiri mpaka maskini wa mwisho anaweza kufeel kuwa uchumi unakua ni sector ya Viwanda na Kilimo vitu ambavyo Tanganyika bado japo tunaelekea kwenye viwanda
Jambo jingine unalonishangaza msomi wa uchumi kupinga takwimu wakati wanasema takwimu zinapigwa kwa takwimu sawa na tafiti pia takwimu hizo za ukuaji wa 7.2% wa uchumi wa Tanganyika ajazileta mzaramo au CCM ni WB na IMF taasisi ambazo zina majukumu makubwa juu ya uchumi wa dunia
1 kwanza jukumu la kushauri,kusimamia monetary policy dunian ni lao
so nilazima wafanye tatifi ili waweza kufanya kazi yao kwa weledi
2 Tafiti wanafanya kwa ajiri yao yani kwa matumizi yao si ya Tanzania au nchi yeyote so wanaweza kujidanganya wao?
pia WB na IMF ndio wakopeshaji wakubwa kwa nchi karibu zote dunian so ni tazima wawe na takwimu sahihi juu ya uchumi wa nchi fulani mfano wamekupa takwimu za uongo kuwa uchumi wako unakua wakt si kweli then kesho ukaenda kukopa kwao kuna bank yeyote dunian inaweza kumkopesha mtu ambae hawezi kurudisha mkopo????????
3 Dunia nzima utumia takwimu katika kupanga maendeleo,kuleta huduma,kuongeza au kupunguza kitu ,hata ktk mambo ya kibiashara,uchumi ,hospital,sehemu zote zinaitaji takwimu ktk kuendeleza au kuondoa jambo fulani
na ndo maana kila nchi ina taasisi ya Bureau of Statistics
Sasa kama tunasema takwimu zinapikwa kumbuka WB na IMF wanatoa takwimu za mambo ya kiuchumi na maswala ya kifedha duniani si Tanzania au Africa peke yake je na Ulaya au America na wenyewe wanadanganywa kama tunavyodanganywa sisi kwenye takwimu?
Na kama wangekuwa wanadangaya sijawai kusikia kuna nchi ikilalamika juu ya takwimu hzo hata kama report imetoka na ni mbaya kwa nchi hyo juu ya mambo ya uchumi au fedha sasa najiuliza nchi inawanauchumi wake na wanakubali report hata kama ni mbaya au labda wameambiwa uchumi wao umeshuka sana kwa nini wasipinge na kusema uchumi wetu uko vizri kwa kujikosha kwa wananchi wao??
Hoja ya pili juu ya Exchange rate kwanza unatakiwa kujua kuwa sarafu wa marekani imeimarika dhidi ya sarafu zingine si Tsh peke yake uchumi wa US umeimarika sana ktk robo ya mwisho wa mwaka jana uchumi wa US umekuwa ukikua kwa kiwango cha 0.8% kila miezi 3 huku unemployment rate ikiwa ni 5% kutoka 10% mm nadhani niishie hapo
GDP = CONSUMPTION + INVESTMENT +GOVERMENT SPENDING + (EXPORT -IMPORT)
Hii CONSUMPTION ni manunuzi ya watu binafsi: investment....ni total of investment ambazo zimefanyika ndani ya mwaka husika wa kupima hii GDP, Goverment spending( hii ni mapato ya serikali toa matumizi):
export- import ( thamani ya vitu tunavyouza nje kutoa thamani ya vitu tunavyoagiza)
sasa tuanze kuangalia baada ya 2015 nadhani mh Raisi alifanya kazi nzuri sana
1)alianza na nia ya kubana matumizi na alisema matumizi yote ya serikali ni lazima yapate ruhusa yake (na hapa ndipo hela yetu kubwa ilipokuwa inapotea kwa safari zisizo na kichwa wala miguu, miradi mingi ambayo hela ilipotea sana)
2)aliadhimia kwa kusema hatachukua misaada nje na lazima tujitegemee kwa kuanza kulipa kodi (kodi ya majengo kuamishiwa TRA, makusanyo ya kodi lazima yasimamiwe vizuri, kutumia mashine za EFD,
3)ukusanyaji mzuri wa faini za makosa ya barabarani, faini za mahakamani nk
4) matumizi mazuri ya fedha za serikali katika miradi yote kwa kuhakikisha serikali kuu inajua hela zinaenda wapi na nani anapokea hizo hela na matumizi yake
katika hayo machache hapo juu nadhani nataka niongelee upoteaji wa hela nyingi ni kuwa hela nyingi zilizokuwa zinapatikana katika njia za rushwa na madili zilianza kupotea, kusimamia ukusanyaji mzuri wa kodi, kulipunguza madili ya watu kuwaibia serikali kwa sababu watu wengi kuanza kuzitumia hizo mashine na makusanyo ya kodi kuongezeka sana
sasa ukiangalia vyote hapo juu ukiweka katika calculations za GDP lazima ziwe na good effect kwa uchumi wetu...
consumption
haya matumizi ya watu binafsi yamepungua sana na hata ukiangalia CPI zitakuwa zimeshuka kutokana na watu kununua vitu wanavyovihitaji na kutochezea tena hela kama zamani, maana hela zilikuwa nyingi
lakini ukiangalia kiundani matumizi ya vitu vilivyoacha kununuliwa si vingi sana...kama mtu alikuwa anatumia 50000tsh kwa siku bar anapunguza anatumia 25000tsh
kama alikuwa anakula kilo 10 nyama kwa wiki basi matumizi yamebadilika kwa kilo 10 kwa wiki 2 au tatu na kuanza kumatumizi ya vitu vingine pia,mchicha,spinach, nk
conclusion:kupungua kwa manunuzi binafsi kwa asilimia kidogo
investment
ukiangalia katika kipindi kifupi utaona kuwa serikali imefanya miradi mbalimbali ambayo ndio inainua hiyo value ya investment,na miradi hii mingi imefanywa au inafanywa na usimamizi mzuri wa serikali kwa ukaribu mzuri zaidi so matokeo yake yataonekana.
conclusion: kuongezeka kwa investment kwa asilimia kubwa kidogo
government spending
hapa tunaangalia mapato ya serikali kutoa matumizi....serikali imeongeza sana mapato kupitia kodi zilizokuwa zinapotea, makusanyo ya kodi kuwa makubwa sana,faini za makosa mengi kufika serikali moja kwa moja bila kupigwa sana
serikali kubana matumizi yake mfano wakala wa majengo kuanza kujenga sana bila kutoa tender, wafanyakazi hewa,
conclusion: mapato juu sana na matumizi kupungua sana..hapa ndipo unapoona ile (MAPATO - matumizi) kuanza kuwa na effect ndogo
export - import
kutokana na kupotea kwa hela mifukoni kwa watu wengi, matumizi ya kununua nguo dubai,magari kila mwaka yamepungua sana,kununua meza italy,tiles italy,makabati england yale mambo yameisha sana ...so tumepunguza sana manunuzi ya hela zakigeni ambazo zilikuwa dili kuna kipindi kila mtu ana dola mtaani kitu ambacho kilikuwa kina affect sana control ya thamani ya hela yetu,mahitaji ya dola yalikuwa juu sana na bei juu
conclusion:.kupungua kwa manunuzi ya nje imepunguza sana (import value) na sasa kuona ile Net export imeongezeka sana maana value ya export ipo pale pale na import imepungua so export -import =value kubwa
sasa ukijumlisha vyote hivi katika GDP = c+i+g+(x-i)...lazima ongezeko liwepo ila ukiangalia ECONOMIC DEVELOPMENT ambapo hapa sasa tunaanza kuangalia maendeleo/uchumi wa mtu mmoja mmoja, elimu, health services, employment hapo ndio tuna kinzana na economic growth yetu iliyopatikana kwa kuangalia jumla na normally inawahusu sana makampuni,serikali na mashirika mbali mbali
ila ukianza kuangalia ECONOMIC DEVELOPMENT ya watu binafsi kina sisi.....hayo yaliyosemwa kama kukua kwa uchumi hauonekani mitaani kwetu tandale,manzese,singida,moshi vijijini,butiama huko,mbeya vijijini,songwe, na vijiji vyote