Shilingi ya Tanzania yazidi kuporomoka

Shilingi ya Tanzania yazidi kuporomoka

Acha upumbavu wako wewe. Shiling hata siku moja haiwezi kuwa kipimo cha uchumi kukua au lah. Kuuza nje bidhaa nyingi siyo kwamba basi uchumi wako ndo ushakua. Acheni kukariri micro and macro economics. Kama ndo hicho kipimo Zimbabwe ingekuwa ndo nchi ya mwisho kwa uchumi duniani. Na Kuwait ndo ingekuwa ya kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
we kahaba unawashwa
 
viwanda havijaanza kutema bidhaa za kuuza nje. but hela yetu itapanda thamani wadeni wetu wakianza kulipa
 
kwanini GDP yetu inaonekana inakuwa while mitaani na biashara nyingi zimezorota sana. huu ni kutokana na maono yangu maana nadhani watu wamekuwa wanaangalia sana kwenye ECONOMIC GROWTH kuliko ECONOMIC DEVELOPMENT. economic growth ni kuangalia ukuaji wa uchumi kwa kuangalia sector zinazojumlisha consumption, investment, goverment saving export and import

GDP = CONSUMPTION + INVESTMENT +GOVERMENT SPENDING + (EXPORT -IMPORT)

Hii CONSUMPTION ni manunuzi ya watu binafsi: investment....ni total of investment ambazo zimefanyika ndani ya mwaka husika wa kupima hii GDP, Goverment spending( hii ni mapato ya serikali toa matumizi):
export- import ( thamani ya vitu tunavyouza nje kutoa thamani ya vitu tunavyoagiza)

sasa tuanze kuangalia baada ya 2015 nadhani mh Raisi alifanya kazi nzuri sana

1)alianza na nia ya kubana matumizi na alisema matumizi yote ya serikali ni lazima yapate ruhusa yake (na hapa ndipo hela yetu kubwa ilipokuwa inapotea kwa safari zisizo na kichwa wala miguu, miradi mingi ambayo hela ilipotea sana)

2)aliadhimia kwa kusema hatachukua misaada nje na lazima tujitegemee kwa kuanza kulipa kodi (kodi ya majengo kuamishiwa TRA, makusanyo ya kodi lazima yasimamiwe vizuri, kutumia mashine za EFD,

3)ukusanyaji mzuri wa faini za makosa ya barabarani, faini za mahakamani nk

4) matumizi mazuri ya fedha za serikali katika miradi yote kwa kuhakikisha serikali kuu inajua hela zinaenda wapi na nani anapokea hizo hela na matumizi yake

katika hayo machache hapo juu nadhani nataka niongelee upoteaji wa hela nyingi ni kuwa hela nyingi zilizokuwa zinapatikana katika njia za rushwa na madili zilianza kupotea, kusimamia ukusanyaji mzuri wa kodi, kulipunguza madili ya watu kuwaibia serikali kwa sababu watu wengi kuanza kuzitumia hizo mashine na makusanyo ya kodi kuongezeka sana

sasa ukiangalia vyote hapo juu ukiweka katika calculations za GDP lazima ziwe na good effect kwa uchumi wetu...

consumption
haya matumizi ya watu binafsi yamepungua sana na hata ukiangalia CPI zitakuwa zimeshuka kutokana na watu kununua vitu wanavyovihitaji na kutochezea tena hela kama zamani, maana hela zilikuwa nyingi
lakini ukiangalia kiundani matumizi ya vitu vilivyoacha kununuliwa si vingi sana...kama mtu alikuwa anatumia 50000tsh kwa siku bar anapunguza anatumia 25000tsh
kama alikuwa anakula kilo 10 nyama kwa wiki basi matumizi yamebadilika kwa kilo 10 kwa wiki 2 au tatu na kuanza kumatumizi ya vitu vingine pia,mchicha,spinach, nk
conclusion:kupungua kwa manunuzi binafsi kwa asilimia kidogo

investment
ukiangalia katika kipindi kifupi utaona kuwa serikali imefanya miradi mbalimbali ambayo ndio inainua hiyo value ya investment,na miradi hii mingi imefanywa au inafanywa na usimamizi mzuri wa serikali kwa ukaribu mzuri zaidi so matokeo yake yataonekana.
conclusion: kuongezeka kwa investment kwa asilimia kubwa kidogo

government spending

hapa tunaangalia mapato ya serikali kutoa matumizi....serikali imeongeza sana mapato kupitia kodi zilizokuwa zinapotea, makusanyo ya kodi kuwa makubwa sana,faini za makosa mengi kufika serikali moja kwa moja bila kupigwa sana
serikali kubana matumizi yake mfano wakala wa majengo kuanza kujenga sana bila kutoa tender, wafanyakazi hewa,

conclusion: mapato juu sana na matumizi kupungua sana..hapa ndipo unapoona ile (MAPATO - matumizi) kuanza kuwa na effect ndogo

export - import
kutokana na kupotea kwa hela mifukoni kwa watu wengi, matumizi ya kununua nguo dubai,magari kila mwaka yamepungua sana,kununua meza italy,tiles italy,makabati england yale mambo yameisha sana ...so tumepunguza sana manunuzi ya hela zakigeni ambazo zilikuwa dili kuna kipindi kila mtu ana dola mtaani kitu ambacho kilikuwa kina affect sana control ya thamani ya hela yetu,mahitaji ya dola yalikuwa juu sana na bei juu
conclusion:.kupungua kwa manunuzi ya nje imepunguza sana (import value) na sasa kuona ile Net export imeongezeka sana maana value ya export ipo pale pale na import imepungua so export -import =value kubwa

sasa ukijumlisha vyote hivi katika GDP = c+i+g+(x-i)...lazima ongezeko liwepo ila ukiangalia ECONOMIC DEVELOPMENT ambapo hapa sasa tunaanza kuangalia maendeleo/uchumi wa mtu mmoja mmoja, elimu, health services, employment hapo ndio tuna kinzana na economic growth yetu iliyopatikana kwa kuangalia jumla na normally inawahusu sana makampuni,serikali na mashirika mbali mbali
ila ukianza kuangalia ECONOMIC DEVELOPMENT ya watu binafsi kina sisi.....hayo yaliyosemwa kama kukua kwa uchumi hauonekani mitaani kwetu tandale,manzese,singida,moshi vijijini,butiama huko,mbeya vijijini,songwe, na vijiji vyote
Ume eleza vizuri sana lakini kwann shilling ina shuka hilo huja jibu

Do you have confidence ?
 
Duniani kuna taasisi mbili ndio zinawajibika na mambo ya kifedha na uchumi ambazo ni WORLD BANK na IMF na kwa hapa Tanganyika ni BOT sasa swala la Phd ni swala la vyeti tu mimi swali langu kwa mleta mada ni vigezo gani ametumia vya kiuchumi kujua kuwa shilingi yetu imeporomoka?
Na wewe huoni? Smartphone mnazotumia za nini? Au makompyuta mnayotumia ya nini ikiwa hata hamjui kuwa shilingi ya Tanzania inaporomoka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lako ni kuwa hujawahi kushika Dollar ukapeleka Bureau De change kubadilisha upate Shs

Kwa hiyo ili kujua shillingi imeporomoka wewe mpaka uulize mtu?

Angalia Trend ya exchange rate, Mwaka uliopita, Mwezi uliopita, wiki iliyopita....eee utajua tu

na hii ipo wazi... Kila benki inaweka exchange rate ubaoni siku hiyo

Au Nenda benki yeyote au Bureau De change yeyote uliza Trend ya shillingi
Mwambie huyo. Mpaka m*****li amtangazie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MM nipo kwenye industry ya mambo ya kifedha so siitaji kwenda Bureau kupata info Tatizo hapa mnachanganya vitu
1 Uchumi 2 Uimara wa sarafu 3 maendeleo kushuka na kupanda kwa thamani ya fedha ktk soko ni jambo ;la kawaida sana na Exchange rate hata siku moja huwezi kukuta inapimwa kwenye uchumi kwani ndio maana unaweza kuona Japan pamoja na uchumi wake unaibadilisha kwa shilingi ngapi?
Tanganyika tullishafikia Exchange rate ya 2500 dhidi ya dola 1 na ukuwaji wa uchumi wetu ulikuwa ni 7.9% kwa mwaka na mpaka sasa ni 7.2% na kuifanya Tanganyika kuwa nchi ya pili Africa huku ya kwanza ikiwa na ukuaji wa 8.1% je sasa Exchange rate ni shiling ngapi?? na ilishakuwa shiling ngapi huko nyuma ?
Samahani ukizungumzia fedha ya Shilingi ni matumizi harari kwa Zanzibar na Tanganyika. Kwa iyo usiweke Tanganyika peke yake Sema Tanzania.
 
Uchumi unakuwa

Duh,

Shillingi 2230 ndio Dollar moja ya USA

mpaka tufike November, Shillingi itakuwa 2400 Kwa Dollar moja

Hivi ndio Viashiria vya uchumi kukua, Tz ya Vi wonder
 
Back
Top Bottom