Shilingi ya Tanzania yazidi kuporomoka

Shilingi ya Tanzania yazidi kuporomoka

Huu ni msimu wa utalii..Peak Season

FOREX (Dollar) zinaingia kwa wingi

Tulitegemea shillingi iwe imara dhidi ya Dolar ya USA..

Sasa kulikoni, shillingi imeporomoka thamani, ni uchumi kukua?

Tanzania yawa nchi ya 5 duniani kwa uchumi unaokuwa kwa kasi. Kenya ya ngapi?
Hizi taarifa zimetolewa na wazungu strategically mkuu hali ya uchumi ni doro kabisa. Alifanikiwa Mkapa tu kuhakikisha uchumi unakuwa imara kwakuwa alikuwa international diplomat ambaye anajua mbinu za wazungu.

Uchumi utakuwaje ikiwa hata tu bia inanunuliwa kwa dola,tunaagiza/import zaidi ya kuuza nje/export hata dola hizo kidogo tulizo nazo tunazirudisha kwa wenyewe poor strategies.

Watu wanazidi kulala njaa huku tunaambiwa uchumi unakuwa. Tumechelewa sana wakati wenzetu wanakimbia sisi ndo tunazinduka usingizini eti tumekuwa tunaibiwa waliosababisha tuibiwe si hawahawa?! too late!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taarifa sahihi ni kutoka BoT kunakosemwa na mkuu wa nchi kuna Phd 17 lakini utendaji wake ameutilia shaka?
Kuna PhD ngapi tanzania? Nyerere hakuwa na Phd lakini alikuwa anajua nini kifanyike uchumi ukue na alikokwama aliachia akili mpya zishughulike.

Mtukufu anaamini wasomi wa vyeti bila kupima uwezo wao kiuhalisia na ndo watakaomkwamisha katika malengo mazuri aliyo nayo kwa nchi hii

Phd za kiafrika si ndo kama za kinalikafu zinazotumika kuyumbisha tu mambo?! So sad kusema tanzania ni fungu la kukosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mheshimiwa nadhani kwa sababu ukuanza kusoma tulichokuwa tunabishana na izzo.basi unaweza usinielewe nilikuwa namaanisha nini ukianza kufuatilia mwanzoni nadhani unaweza kupata picha ya nini nilikuwa naongea na izzo

sasa hao BOT wanaosema uchumi umekuwa kwa 7.2% wanatoa wapi figure zao?nadhani tusibishane kwasababu tunaamini na kuona uchumi si mzuri hao wenye dhaman na uchumi wetu wanasema uchumi unakua
okay katika yote niliyoongea nadhani vipo wazi...kama mimi naona uchumi umekuwa kwasababu ya vitu visivyo na maana kwa maendeleo ya taifa na haviwezi kudumu.
naomba upitie hapa then nije nikupe na wewe matusi yako
Tanzania Overview
IMF Tanzania Economy Review: GDP Growth Strong, Budget Spending Needed - TanzaniaInvest

Ulitoa ulinganisho wa uchumi kipindi cha JK na wakati wa magufuli, uka-conclude kuwa sasa uchumi unakuwa kwa kasi zaidi . NIMEKUJIBU NO. si kweli na data hizo japo umeweka mwenyewe. sasa 7.9 na 7.2 ipi kubwa? mbona hesabu ndogo sana hiyo?
Kuhusu uchumi unakuwa kwenye vitu gani that's immaterial, kwa sababu regardless ni kuwa uchumi unakuwa kwa kasi ndogo kuliko ulivyokuwa unakuwa wakatwa JK, either iwe ni wa makaratasi au vinginevyo.

tusipende kusikiliza sana wanasiasa economic growth na economic development ni vitu viwili tofauti...uchumi wa zimbabwe unaweza kukua na hali yao ni mbaya zaidi

Hali ya mtaani ni mbaya kuliko uchumi wa makaratasi. waulize VODACOM na IPO yao ya 500B imekwendaje, hilo halihitaji data za BOT.
 
kwa leo nataka nitafute data nyingi as possible kuonesha kuwa uchumi unakua lakini nataka nikwambie kuwa uchumi kukua hakumsaidii chochote mwananchi wa kawaida zaidi sana ni kwa ma investor ambao uangalia nchi masikini kama Tanzania lakini uchumi wake unakuwa katika rate nzuri ya 6-7%..hivyo kwa wanaoinvest hela nyingi ni opportunity kwao kuja kufanya biashara maana kwa nchi inayoendelea mara nyingi opportunity ni nyingi
ila kwa mwananchi kama mimi na wewe ukuaji huu wa uchumi hautusaidii sana kama ECONOMIC DEVELOPMENT ambazo hizi zinatugusa moja kwa moja ndani kwetu na familia zetu na jamii zetu hazikui

hapo chini ni data za quarter moja kulinganisha na mwaka uliopita: katika quarter hii inaonesha kabisa kuporomoka kwa sector mbalimbali lakini ukiangalia uwekezaji ndani ya sector hizo ndio itaamua imepungua kwa asilimia ngapi

mfano kama construction sector ukubwa wake ni 1b ikiongezeka kwa 1% ....lakini kama finance and banking sector total value ni 100m ikipungua kwa 10% itakuwa imepunguza 10m... utakuta value iliyoongezeka ina cover iliyopungua
katika kuangalia ukuaji wa uchumi ni vizuri pia kuangalia total value ya sector nzima

http://www.bot.go.tz/Adverts/PressRelease/Taarifa ya Hali ya Uchumi.pdf

Finally you are making sense., This is opposite of what you were saying before.

SEKTA karibu ZOTE zinaporomoka.

Hence, in agreement with my previous conlusion. HUYU bwana mfupi anaharibu.
 
Lakini ripoti zao za kupika toka Lumumba zinaeleza uchumi unakua kwa kasi.
Acha upumbavu wako wewe. Shiling hata siku moja haiwezi kuwa kipimo cha uchumi kukua au lah. Kuuza nje bidhaa nyingi siyo kwamba basi uchumi wako ndo ushakua. Acheni kukariri micro and macro economics. Kama ndo hicho kipimo Zimbabwe ingekuwa ndo nchi ya mwisho kwa uchumi duniani. Na Kuwait ndo ingekuwa ya kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ningekuwa na uwezo ningewanunulia pc raia wote tz wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea ,baadae nawapatia kifurushi cha mwaka ili wajiunge jamii forum wapate vitu vizuri .naskitika napata mimi tu mambo mazuri haya kutoka jamii na wenzangu wachache .
 
Ulitoa ulinganisho wa uchumi kipindi cha JK na wakati wa magufuli, uka-conclude kuwa sasa uchumi unakuwa kwa kasi zaidi . NIMEKUJIBU NO. si kweli na data hizo japo umeweka mwenyewe. sasa 7.9 na 7.2 ipi kubwa? mbona hesabu ndogo sana hiyo?
Kuhusu uchumi unakuwa kwenye vitu gani that's immaterial, kwa sababu regardless ni kuwa uchumi unakuwa kwa kasi ndogo kuliko ulivyokuwa unakuwa wakatwa JK, either iwe ni wa makaratasi au vinginevyo.

Hali ya mtaani ni mbaya kuliko uchumi wa makaratasi. waulize VODACOM na IPO yao ya 500B imekwendaje, hilo halihitaji data za BOT.
hali ya mtaani sio economic growth ni economic development
 
Finally you are making sense., This is opposite of what you were saying before.

SEKTA karibu ZOTE zinaporomoka.

Hence, in agreement with my previous conlusion. HUYU bwana mfupi anaharibu.
mkubwa ndio maana nimekwambia ungesoma nilichoondika mwanzo....huyu jamaa nilikuwa namuelekeza kuhusu uchumi wetu unaposemekana unakua ....INAWEZEKANA unatokea au wame calculate kutoka kwa vile vitu nilivyo viweka mwanzo
kwasababu wengi wetu hatuangaliagi VOLUME au total VALUE ya sector fulani bali tunaangalia percentage fall/increased

NOTE: Matumizi kuongezeka nadhani sababu kubwa zaidi ni ELIMU BURE..

sibishani na wewe kuwa huyu jamaa mfupi haeleweki na nadhani wanaojua uchumi wana mdanganya kuhusu kuweza ku control uchumi wetu kwa wepesi zaidi
 
Acha upumbavu wako wewe. Shiling hata siku moja haiwezi kuwa kipimo cha uchumi kukua au lah. Kuuza nje bidhaa nyingi siyo kwamba basi uchumi wako ndo ushakua. Acheni kukariri micro and macro economics. Kama ndo hicho kipimo Zimbabwe ingekuwa ndo nchi ya mwisho kwa uchumi duniani. Na Kuwait ndo ingekuwa ya kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app

Wewe ndo mpumbavu kama unafikiri currency ya nchi haiwezi kutukima kama kipimo cha kukua au kudorora kwa uchumi!! Hivi kwa nini kila siku Mabenki including BOT huwa wanatoa taarifa ya THAMANI ya Shilingi yetu kulinganisha na DOLLAR?
Nimeshasema angalia jirani zetu Kenya na Shillingi yao ilivyo imara dhidi ya Dollar halafu ulinganishe UCHUMI wa Kenya na Tanzania. Ni ujinga na uzuzu kudai kuwa Fedha haiwezi kuwa kipimo cha uchumi wa Taifa lolote. Unaweza kutuambia hapa ni kwanini fedha zote duniani lazima zilinganishwe na Dollar ya Marekani???Kwa kifupi ni kwamba tunatumia Dollar kwa viel Marekani ni the strongest country ecomically and politically.

Kama unataka kujua fedha inahusiana na kukua au kudorora kwa Uchumi angalia Uganda enzi za Nduli Idd Amin ambapo ilifikia mtu kwenda sokoni kununua nyanya anabeba magunia ya noti!!Kwanini? Kama Uchumi UNAKUA MBONA BAJETI YA 2016/17 Bajeti imetoshleza chini ya 40%?? Hiyo pesa inayoingia kutokana na Uchumi kukua iko wapi kwenye Bajeti ya Serikali na kwenye mzunguko wa fedha mtaani na kwa Mwananchi mmoja na mmoja?????

CCM na Magufuli mnataka kuwalaghai Watanzania kuwa Uchumi unakuwa ilhali kiuhalisia uchumi unaporomoka kwa kasi ya ajabu!!!
Kama Rais hana nidhamu ya matumizi ya fedha lazima Thamani ya shilingi ishuke. Anachofanya Magufuii hakina tofauti na kile alichokuwa akifanya Nduli Idd Amin. Kwamba baada ya WAZIRI WA FEDHA KUMWAMBIA IDDI AMIN KUWA Banki Kuu haina fedha AMINI AKAMWAMBIA ACHAPISHE NOTE KWA WINGI!!!!
Magufuli anapojifungia Ikulu na Mtoto wa Shangazi yake au Dada yake na kubadilisha matumizi ya Fedha bila kibali cha Bunge kulingana na Bajeti unategemea nini???
 
Nimekuelewa
 
Kuna hohe hahe kiuchumi na kiakili wanajaribu kusema eti kuna maendeleo

eti shillingi kushuka sio sababu]

Hohe hahe wanasema mara ooh, umesoma wapi shilingi imedorora...duh

Vilaz...a hoyeee
 
Acha upumbavu wako wewe. Shiling hata siku moja haiwezi kuwa kipimo cha uchumi kukua au lah. Kuuza nje bidhaa nyingi siyo kwamba basi uchumi wako ndo ushakua. Acheni kukariri micro and macro economics. Kama ndo hicho kipimo Zimbabwe ingekuwa ndo nchi ya mwisho kwa uchumi duniani. Na Kuwait ndo ingekuwa ya kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app

Stupid comment

So uchumi kukua ni nini sasa

Unapinga hoja ya mtu bila kuweka hoja yako?

Craxy Lumumba's without proper argument
 
Wewe ndo mpumbavu kama unafikiri currency ya nchi haiwezi kutukima kama kipimo cha kukua au kudorora kwa uchumi!! Hivi kwa nini kila siku Mabenki including BOT huwa wanatoa taarifa ya THAMANI ya Shilingi yetu kulinganisha na DOLLAR?
Nimeshasema angalia jirani zetu Kenya na Shillingi yao ilivyo imara dhidi ya Dollar halafu ulinganishe UCHUMI wa Kenya na Tanzania. Ni ujinga na uzuzu kudai kuwa Fedha haiwezi kuwa kipimo cha uchumi wa Taifa lolote. Unaweza kutuambia hapa ni kwanini fedha zote duniani lazima zilinganishwe na Dollar ya Marekani???Kwa kifupi ni kwamba tunatumia Dollar kwa viel Marekani ni the strongest country ecomically and politically.

Kama unataka kujua fedha inahusiana na kukua au kudorora kwa Uchumi angalia Uganda enzi za Nduli Idd Amin ambapo ilifikia mtu kwenda sokoni kununua nyanya anabeba magunia ya noti!!Kwanini? Kama Uchumi UNAKUA MBONA BAJETI YA 2016/17 Bajeti imetoshleza chini ya 40%?? Hiyo pesa inayoingia kutokana na Uchumi kukua iko wapi kwenye Bajeti ya Serikali na kwenye mzunguko wa fedha mtaani na kwa Mwananchi mmoja na mmoja?????

CCM na Magufuli mnataka kuwalaghai Watanzania kuwa Uchumi unakuwa ilhali kiuhalisia uchumi unaporomoka kwa kasi ya ajabu!!!
Kama Rais hana nidhamu ya matumizi ya fedha lazima Thamani ya shilingi ishuke. Anachofanya Magufuii hakina tofauti na kile alichokuwa akifanya Nduli Idd Amin. Kwamba baada ya WAZIRI WA FEDHA KUMWAMBIA IDDI AMIN KUWA Banki Kuu haina fedha AMINI AKAMWAMBIA ACHAPISHE NOTE KWA WINGI!!!!
Magufuli anapojifungia Ikulu na Mtoto wa Shangazi yake au Dada yake na kubadilisha matumizi ya Fedha bila kibali cha Bunge kulingana na Bajeti unategemea nini???
Kama ukiwa unasema kwamba pesa ndio kigezo cha kukuwa kwa uchumi angalia pesa ya Pounds vs Dollars. Maana pounds ni kubwa inamaana waingereza wapo juu kupita Marekani.
 
Au pesa ya China na ya Japan [emoji557] [emoji552] ni ndogo sana ukilinganisha na Saud arabia. Unataka kusema uchumi wa Saudi Arabia unapita China na Japan [emoji557] [emoji552]
 
Kwa trend hii ya kushuka kwa uchumi na kuhamika kwa dola Ipo siku utakuwa na billions of tsh lakini itakuwa ngumu kununua japo noah toka japan karibuni wana jf tujadili hoja hapo juu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisema hadharani utaitwa mchochezi mamlaka toka juu itawatuma polisi wakukamate baadae utapimwa mkojo
 
Back
Top Bottom