Shilingi ya Tanzania kuipiku dollar ya Marekani

Shilingi ya Tanzania kuipiku dollar ya Marekani

Haiwezekani mkuu, ni sawa na kusema tuongeze upana wa mipaka ya nchi hadi KENYA yote , Uganda yote Rwanda na Burundi tuite Tanzania!
hizi nchi zina wenyewe sio mali yetu, hata hizi currency zimeanzishwa na wenyewe, Kazi ya Benki kuu ni hiyo kuongeza au kupunguza value ya pesa. Tambua BOT si mali ya watanzania. Ni mali ya Illuminatti/Jesuits wa Vatican, Hao jamaa wanaimiliki hadi Federal Reserve bank ya USA za zingine zote Duniani...
Wrong Ideology,Uelewa wako mdogo kuhusu masuala ya uchumi na Fedha
 
Haiwezekani mkuu, ni sawa na kusema tuongeze upana wa mipaka ya nchi hadi KENYA yote , Uganda yote Rwanda na Burundi tuite Tanzania!
hizi nchi zina wenyewe sio mali yetu, hata hizi currency zimeanzishwa na wenyewe, Kazi ya Benki kuu ni hiyo kuongeza au kupunguza value ya pesa. Tambua BOT si mali ya watanzania. Ni mali ya Illuminatti/Jesuits wa Vatican, Hao jamaa wanaimiliki hadi Federal Reserve bank ya USA za zingine zote Duniani...
Mbona Zambia waliweza?

Sent From Mhenga Aliyesema Hasomeshi Wazazi
 
Wewe ni mpumbavu. Unajibu swali langu kwani nimekuuliza wewe? Wtu kama wewe msioelewa kaa mbali na mimi. Sijakuliza wewe na hujui hata nini nilitaka kuendelea na mwuliza swali. Ondoa uharibifu wako hapa. Fueyewwwwww.
Mkuu mbona unamkasirikia?

Kutumia uchumi wa karatasi ni jambo baya kabisa ambapo nchi zimeingizwa mkenge na hao Illuminatti, wao wannunua mali halisi kama Gold na Silver wao wanatupatia karatasi. Uchumi mzuri ni ule wa mali kwa mali. sio mali kwa makaratsi, eti yameandikwa Fedha halali.
 
Kuimarisha sarafu si kitu kizuri mara zote.

Tafadhali rejea post namba 16 katika uzi huu huu hapo nyuma kidogo.

Sent from my Kimulimuli

Nakubaliana na wewe kabisa kuhusu thamani ya pesa na uchumi wa kibiashara na pia si vizuri kuwa na sarafu dhaifu kama hamjitosherezi kimahitaji na mnategemea import of goods and services.

Kama thamani ya pesa iko chini ni nzuri kwa exporting business lakini pia hicho cha ku-export muwe nacho (product au services), lakini pia usisahau inflation ambayo inaumiza mahitaji/matumizi ya ndani kama tunavyoona sasa sababu sarafu yetu siyo imara na tunategemea kwa kiasi kikubwa imports of goods and services.

Hivyo kubadilisha siyo mbaya sana sababu hata Ghana cedis waliweza na economy prospects in Ghana iko vizuri.
 
Tunaweza kuamua kubadilisha fedha zetu tunavyotaka wakati wowote. Lakini haitusaidii lolote kufanya hivyo kama uchumi wetu haujakua inavyotakiwa. Kadiri tunavyouza bidhaa na huduma nyingi nje ya nchi ndivyo kadiri shilingi yetu inavyopata thamani kubwa. Suluhisho pekee ni kukuza shughuli za uzalishaji kweny kilimo ambapo ndipo Watanzania wengi wamejikita. Mazao ya kilimo yasindikwe tuyauze nje kwa thamani kubwa zaidi. Vijana wote wapatiwe shughuli za uzalishaji (kwenye kilimo, uvuvi, ufugaji, uchimbaji madini na kazi za viwandani) na sio kuwapa mitaji ya kufanya umachinga wakiuza bidhaa za nchi nyingine na kuinua uchumi wa nchi hizo. Ni mpaka pale falsafa ya 'hapa kazi' itakapoweza kuwapa vijana wote kazi ya uzalishaji ndipo maendeleo ya kweli yatakapokuja.

Sent from my SM-J120H using JamiiForums mobile app
Maoni yangu mauzo ya fedha za dhahabu zingekuwa zinakaa nchini dhahir shilingi ingekuwa na thamani

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
never kwa vitu gan tunavyo uza kimataifa

Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
 
Wanajamvi haswa wachumi nilikuwa naomba kuuliza, hivi kwa mfano Tanzania ikiamua kufuta pesa zake zote na kuanzisha currency mpya labda tukaiita KIDAKA, sasa tukaamua kwamba dola moja iwe sawa na KIDAKA mbili, je inawezekana? na kama haiwezekani ni kwanini? kwani nani anasimaia uanzishwaji wa currency mbona watu wana currency wanaziita kikwao kama kwacha, reale au yen? je wakati zinaanza zilikuwa chini hivyo hivyo? Dah ebu WACHUMI nisaidieni
Ni Kitu hakiwezekan kaka ukapandisha thaman ya hela yako kwa style hiyo uliyo ifikiria.

Kuwa na hela yenye thaman ina pimwa na AMERICAN DOLLARS na kunafactors nyingi sn ya kupandisha HELA yako thaman.

Nakupa hii moja wapo tu Inayoikabili NCHI yetu EXPORTS AND IMPORTS

MFANO:
EXPORTS VALUE yako.....$ 1 BILLION
IMPORTS VALUE yako.....$ 5 BILLION
sasa hapo kaka unaweza tu kuamua kama ulivyo fikiria maan.... tutahitaji kununua DOLLA ya ziada ili kucover mapungufu.... na yapo mambo mengi na yanayo husiana na thaman ya pesa yako.

Zimwi likujualo......
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuhusu thamani ya pesa na uchumi wa kibiashara na pia si vizuri kuwa na sarafu dhaifu kama hamjitosherezi kimahitaji na mnategemea import of goods and services.

Kama thamani ya pesa iko chini ni nzuri kwa exporting business lakini pia hicho cha ku-export muwe nacho (product au services), lakini pia usisahau inflation ambayo inaumiza mahitaji/matumizi ya ndani kama tunavyoona sasa sababu sarafu yetu siyo imara na tunategemea kwa kiasi kikubwa imports of goods and services.

Hivyo kubadilisha siyo mbaya sana sababu hata Ghana cedis waliweza na economy prospects in Ghana iko vizuri.
Haya mambo yapo complex sana.

Kanuni ya msingi ya kuelewa ni hii.

Pesa ni makaratasi tu.Unaweza kuipandisha au kuishusha thamani (kwa maana ya kuondoa sifuri kadhaa au kuifanya iwe inabadilishwa kwa uwiano wa moja kwa dola nyingi), lakini kama hujapandisha production na balance of trade, kupandisha thamani pesa hivyo hakuna maana.

Ni sawa na Idi Amin alivyotaka kupandisha uchumi wa Uganda kwa kuamrisha Benki Kuu ichapishe hela nyingi, matokeo yake akapata "unintended consequence" ya inflation.

Kwa hiyo, kama tunataka kuendeleza uchumi, tuangalie zaidi uzalishaji na balance of trade kuliko kutaka ku manipulate currency.

Unaweza kuongea habari za kupanga thamani ya pesa kama una uzalishaji mzuri na una cha ku export, kama anavyofanya China. Kabla ya hapo cha umuhimu kabisa ni uzalishaji.

Tukizalisha vitu vingi vyenye thamani kubwa vinavyonunuliwa na watu wengi thamani ya pesa itapanda yenyewe.

Na, tukipandisha thamani ye pesa yetu bila uzalishaji wa kutosha, hata hicho kidogo tunachozalisha kitakosa mnunuzi huko nje.
 
Inawezekana.

Ila kinachokuza uchumi ni uzalishaji. Si thamani ya hela.

Tukienda soko la dunia mafuta yanauzwa kwa dola za Kimarekani. Wajapani wanapinunua mafuta kutoka Saudi Arabia wananunua kwa dola za Kimarekani. Hawatumii Japanese Yen au Saudi Riyals.

Dola ya Kimarekani ndiyo hela inayotumika sana katika biashara ya kimataifa.

Sasa kama leo dola moja ni Sh 2500, kesho dola moja iwe nusu Kidaka, basi hiyo Kidaka moja itakuwa inabadilishwa kwa shilingi elfu tano za zamani tu.

Zaidi, kuwa na hela yenye thamani kubwa si automatically kuwa na uchumi mzuri.

China kwa miaka mingi wamejitahidi sana hela yao isipande thamani.

Ndiyo. Nchi inaweza kujitahidi hela yao isipande thamani. Tena wamefanya hivyo mpaka Marekani wamelalamika sana kwamba Wachina wanaishusha hela yao thamani makusudi. Waziri wa Fedha wa Obama Timothy Geithner alilisema hili. Donald Trump amekuwa akilisema hili miaka mingi sana na mpaka leo analisema.

Kwa vipi nchi itake hela yake isipande thamani?

Hela ya nchi ikipanda thamani, kuuza bidhaa za nchi hiyo nje inakuwa vigumu sana. Nitakupa mfano.

Ki hamburger cha Marekani ni rahisi sana kufika $2 Marekani. $2 Marekani kutoa kununua hamburger, na $2 nyingine kutoa kununua juisi ukapata lunch ya kujibana actually umekula mlo cheap sana hapo. Kwa wastani unaweza kula lunch ya $6 na kama unataka kutanua unaweza kufikisha hata $30. Sasa fanya hesabu za mtu wa kawaida bongo ki humburger karibu sh 5,000 na kijuice karibu sh 5,000 nyingine. Hiyo hapo ni very cheap lunch ushaondoa sh 10,000. Comparison nikiendeleza unakuta $6 ni karibu sh 15,000 na $30 ni karibu sh 75,000

Ndiyo maana McDonalds ya Marekani haiwezi kuanzisha franchise Dar na kuuza vitu kwa bei za Kimarekani. Hawatafanya biashara kwa sababu dola ina nguvu sana.

China wanakataa kupandisha Yuan kwa sababu China ni a giant exporter. Moja ya sababu unaona kila kitu ni "Made in China" ni kwa sababu Dola moja ni 6.78 Yuan. Wakiipandisha sana thamani Yuan iwe karibu aubiizidi dollar, watashusha exports uchumi utadorora.

Wao kuuza vitu nje kwa urahisi ni muhimu kuliko thamani ya hela yao kuwa kubwa sana.

Kwa hiyo, kuwa na hela yenye thamani sana kunaweza kuharibu uchumi.

Kinachopandisha uchumi si thamani ya hela, ni uzalishaji na kuuza vitu nje.

Nchi inaweza kuwa na hela ambayo haina thamani sana ikawa na uchumi mzuri kuliko nchi yenye hela yenye thamani sana.

Ila, tatizo letu ni kwamba, tuna hela isiyo na thamani, halafu hatuna uzalishaji wa ku export kwa sana. Hii wanaita "the worst of both worlds". Tunapigwa kwa kuwa na hela isiyo na thamani, halafu tunapigwa tena kwa kukosa uzalishaji.

Tungepigwa kumoja tu kwa kuwa na hela isiyo na thamani wakati upande wa uzalishaji tuko fiti, tungeweza ku revenge kwa kutumia hela isiyo na thamani kuongeza exports kama wanavyofanya China. Mpaka tufanye kuwa na hela isiyo na thamani kutusaidia kiuchumi.

Lakini hatufanyi hivyo. Nchi ambayo ina hela isiyo na thamani halafu haina uzalishaji mzuri, inapata matatizo sana inapoagiza vitu kutoka nje. Kwa sababu hela yake haina thamani. Ikienda kununua dola dola zinakuwa za bei ya juu sana. Ikienda kununua mafuta mafuta yanakuwa ya bei ya juu sana. Na kwa vike haina uzalishaji sana, ikitegemea imports, uchumi unashuka.

Geithner Hints at Harder Line on China Trade

Exclusive: Trump calls Chinese 'grand champions' of currency manipulation

Sent from my Kimulimuli
Kula Like mkuu
 
kwa dhahabu

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
yeye ana fanya biashara ya vitu vingapi pili dhahab zenyewe thaman yake sisi kama wa tz hatujui alafu tatu mashine zenyewe za kusafshia mpaka kwao kuwapita mpaka tuwe na uwezo wakutengeneza mashine za kuzalishia maligaf sisi wenyewe una nunua trekta kwao alafu unataka kuwa pita kifedha wao tengeneza na wew uanze kuuza ndipo ufikilie hayo unayo fikiria in short tz inahitaji viwanda vingi sana

Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
 
Haya mambo yapo complex sana.

Kanuni ya msingi ya kuelewa ni hii.

Pesa ni makaratasi tu.Unaweza kuipandisha au kuishusha thamani (kwa maana ya kuondoa sifuri kadhaa au kuifanya iwe inabadilishwa kwa uwiano wa moja kwa dola nyingi), lakini kama hujapandisha production na balance of trade, kupandisha thamani pesa hakuna maana.

Ni sawa na Idi Amin alivyotaka kupandisha uchumi wa Uganda kwa kuamrisha Benki Kuu ichapishe hela nyingi, matokeo yake akapata "unintended consequence" ya inflation.

Kwa hiyo, kama tunataka kuendeleza uchumi, tuangalie zaidi uzalishaji na balance of trade kuliko kutaka ku manipulate currency.

Unaweza kuongea habari za kupanga thamani ya pesa kama una uzalishaji mzuri na una cha ku export, kama anavyofanya China. Kabla ya hapo cha umuhimu kabisa ni uzalishaji.

Tukizalisha vitu vingi vyenye thamani kubwa vinavyonunuliwa na watu wengi thamani ya pesa itapanda yenyewe.

Na, tukipandisha thamani ye pesa yetu bila uzalishaji wa kutosha, hata hicho kidogo tunachozalisha kitakosa mnunuzi huko nje.

Hapo kwenye blue nakubaliana na wewe kabisa kwa asilimia 100%. Na kuna sababu nyingi sana za kusabisha inflation kuwa kubwa kwa nchi ila cha muhimu kudhibiti inflation kupanda.

Hapo kwenye red mkuu si kweli sababu goods au services haziwezi kupandisha thamani ya pesa na haijawahi kutokea kwenye uchumi huu wa sasa.
 
Wanajamvi haswa wachumi nilikuwa naomba kuuliza, hivi kwa mfano Tanzania ikiamua kufuta pesa zake zote na kuanzisha currency mpya labda tukaiita KIDAKA, sasa tukaamua kwamba dola moja iwe sawa na KIDAKA mbili, je inawezekana? na kama haiwezekani ni kwanini? kwani nani anasimaia uanzishwaji wa currency mbona watu wana currency wanaziita kikwao kama kwacha, reale au yen? je wakati zinaanza zilikuwa chini hivyo hivyo? Dah ebu WACHUMI nisaidieni
Watu kama wewe mnatakiwa mkamatwe
 
duuu nimesoma uchumi partial lakini hiii yakupunguza 0 ndo naisikia leo embu tufafanulie labda kuna point kubwa
 
Kuibiwa kwa rasilimali nchini kumepelekea shilingi kushuka thamani, rushwa na uchaguzi usiokuwa huru..

Nakumbuka dola moja ilikuwa kwa shilingi mia tano, sasa dola moja ni 2200 nakumbuka rial ya Oman ilikuwa 2000 kwa rial moja, sasa ni 5600.
Nadhani wasomi watueleze zaidi kwa nini kila siku shilingi kupungua thamani, au kule bot wanaajiriwa vilaza watoto wa mjomba wasio jua kazi zao? Bank ndio inayo endesha nchi nasio rais

Mkuu, kwa taarifa tu, 1$ = 2240 Tshs as of jana tarehe 13/7/2017
 
Haiwezekani mkuu, ni sawa na kusema tuongeze upana wa mipaka ya nchi hadi KENYA yote , Uganda yote Rwanda na Burundi tuite Tanzania!
hizi nchi zina wenyewe sio mali yetu, hata hizi currency zimeanzishwa na wenyewe, Kazi ya Benki kuu ni hiyo kuongeza au kupunguza value ya pesa. Tambua BOT si mali ya watanzania. Ni mali ya Illuminatti/Jesuits wa Vatican, Hao jamaa wanaimiliki hadi Federal Reserve bank ya USA za zingine zote Duniani...
HVI HIZI HABARI ZA ILLUMINAT/JESUIT WA VATICAN HUWA MNAZITOA WAPI?
 
Masuala ya uchumi na fedha wanayajua wachaga, ninyi mlioenda shule mmekaria kutudanganya tu na theory zenu zisizofanya kazi[/QUOTE

Swali tu dogo, Dola ya marekeni inafanya vema,je huko kuna wachaga uliowasema???,
Kupanda na kushuka kwa thamani ya pesa hutegemea zaidi upatikanaji na Uhitaji wa pesa zako, Ili wahitaji wa pesa zako( Pesa za nchi yako) basi zalisha mali na uwambie wageni wanunue vitu vya pesa ya nchi yako tu hapo uhitaji wa pesa utapanda na thamani yake pia itapanda.

Hi ni sawa tu na biashara ya wachaga ukitaka bei ya sukari ipande ficha iwe inapatikana kidogo then wahitaji wakiwa wengi wenyewe watakua wanapandishana bei ya kununulia.
 
Back
Top Bottom