Shilingi ya Tanzania kuipiku dollar ya Marekani

Shilingi ya Tanzania kuipiku dollar ya Marekani

hiram

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2013
Posts
266
Reaction score
393
Wanajamvi haswa wachumi nilikuwa naomba kuuliza, hivi kwa mfano Tanzania ikiamua kufuta pesa zake zote na kuanzisha currency mpya labda tukaiita KIDAKA, sasa tukaamua kwamba dola moja iwe sawa na KIDAKA mbili, je inawezekana? na kama haiwezekani ni kwanini? kwani nani anasimaia uanzishwaji wa currency mbona watu wana currency wanaziita kikwao kama kwacha, reale au yen? je wakati zinaanza zilikuwa chini hivyo hivyo? Dah ebu WACHUMI nisaidieni
 
Haiwezekani mkuu, ni sawa na kusema tuongeze upana wa mipaka ya nchi hadi KENYA yote , Uganda yote Rwanda na Burundi tuite Tanzania!
hizi nchi zina wenyewe sio mali yetu, hata hizi currency zimeanzishwa na wenyewe, Kazi ya Benki kuu ni hiyo kuongeza au kupunguza value ya pesa. Tambua BOT si mali ya watanzania. Ni mali ya Illuminatti/Jesuits wa Vatican, Hao jamaa wanaimiliki hadi Federal Reserve bank ya USA za zingine zote Duniani...
 
yes hilo linawezekana,Zambia wamelifanya hili wamefuta yale 000 zote na thamani ya kwacha ni zaidi ya ths.yetu,political will na kuwa seriously na uchumi wetu hili tunaliweza,hakikisha tunajitahidi kuuza zaidi ya tunachoagiza,tujitegemee kwa bajeti yetu,na masuala haya ya fedha nchi nyingi zinaoanisha sarafu yao kwa zingine mfano,Namibian dollar kwa ZAR,Lesotho loti kwa ZAR,Swaziland lilangeni kwa ZAR,kwa hiyo ukitembelea hizi nchi unaweza kutumia ZAR ndani ya nchi hizo.
 
Haiwezekani mkuu, ni sawa na kusema tuongeze upana wa mipaka ya nchi hadi KENYA yote , Uganda yote Rwanda na Burundi tuite Tanzania!
hizi nchi zina wenyewe sio mali yetu, hata hizi currency zimeanzishwa na wenyewe, Kazi ya Benki kuu ni hiyo kuongeza au kupunguza value ya pesa. Tambua BOT si mali ya watanzania. Ni mali ya Illuminatti/Jesuits wa Vatican, Hao jamaa wanaimiliki hadi Federal Reserve bank ya USA za zingine zote Duniani...
Aisee, please tell us more kaka!

Ni kwanini Tshs iko chini?
 
Its virtually impossible. Ukisoma kanuni ya Purchasing Power Parity inazungumzia kuhusu mambo ya exchange rates.
Yani Iwapo inagharimu Tsh elfu moja kununua mkate wa boflo hapa Tanzania na wakati inagharimu dola moja kununua mkate wa boflo nchini Marekani, the exchange rate will be $1= Tsh 1,000. Ofcourse kuna assumptions zake kama vile no transportation costs, na pia no taxation. But purchasing power parity (PPP) Ni msingi mzuri wa kukokotolea exchange rates.
Vipo vitu vingine vinavyoathiri exchange rate kama vile demand na supply ya currency (fedha husika). Mfano iwapo Tanzania tuna mahitaji makubwa sana ya dola kwa ajili ya kununulia bidhaa nje ya nchi, hii ina maanisha lazima shilingi itashuka thamani unless the govt pumps more dollars to Bureau De change to keep up with the demand ya dollar.
Otherwise hicho unachozungumzia ndicho China wanachotuhumiwa na Marekani kukifanya yani they have kept their currency artificially low ili kufanya iwe cheaper ku export bidhaa za kutoka China na iwe gharama kuimport bidhaa kutoka nchi nyingine kwenda China!
 
Kuna tofauti kubwa kati ya thamani ya fedha na nguvu ya sarafu katika soko.

Kwenye uchumi so long as fedha yako haina nguvu ya kimanunuzi katika soko la dunia au unanunua kwa wenzako kuliko unavyowauzia basi hata kama ungepunguza masifuri au kuyaongeza kwenye tarakimu ya fedha yako bado inakuwa haina maana.

Nikukumbushe tu kuwa fedha ya japani inabadilishwa kama sawa na shilingi ya Kenya kwa fedha yetu hapa nchini.

Sasa usidhani kuwa Japani ni nchi yenye uchumi mdogo au fedha yake haina thamani kwa kuwa inalingana na ya Kenya katika exchange rate.

Marekani na Mchina wanagombana kila siku katika hilo.

Kwamba Mchina ameporomosha thamani ya fedha yake kwa makusudi ili iwe na nguvu katika manunuzi na inaihenyesha Dollar ya Marekani kweli kweli.

Hata kama tungefuta masifuri yote kwenye fedha yetu elfu 10 ikabaki kusomeka sh 10 bado kama hatuuzi vingi zaidi ya tunavyonunua ni kazi bure tu.

Sent by Bilionea ASIGWA mutu ya hela Mingi
 
Haiwezekani mkuu, ni sawa na kusema tuongeze upana wa mipaka ya nchi hadi KENYA yote , Uganda yote Rwanda na Burundi tuite Tanzania!
hizi nchi zina wenyewe sio mali yetu, hata hizi currency zimeanzishwa na wenyewe, Kazi ya Benki kuu ni hiyo kuongeza au kupunguza value ya pesa. Tambua BOT si mali ya watanzania. Ni mali ya Illuminatti/Jesuits wa Vatican, Hao jamaa wanaimiliki hadi Federal Reserve bank ya USA za zingine zote Duniani...
🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁
 
Kuibiwa kwa rasilimali nchini kumepelekea shilingi kushuka thamani, rushwa na uchaguzi usiokuwa huru..

Nakumbuka dola moja ilikuwa kwa shilingi mia tano, sasa dola moja ni 2200 nakumbuka rial ya Oman ilikuwa 2000 kwa rial moja, sasa ni 5600.
Nadhani wasomi watueleze zaidi kwa nini kila siku shilingi kupungua thamani, au kule bot wanaajiriwa vilaza watoto wa mjomba wasio jua kazi zao? Bank ndio inayo endesha nchi nasio rais
 
Hiki kitu hufanyika pale nchi inapokuwa katika khar mbaya ya kiuchumi(economy crisis)
Nchi inaweza kuomba kutumia currency ya nchi nyingine ili kujiimalisha..mfano ni zimbabwe...inatumia usd na gharama za maisha ziko juu kama ulaya..
 
Tunaweza kuamua kubadilisha fedha zetu tunavyotaka wakati wowote. Lakini haitusaidii lolote kufanya hivyo kama uchumi wetu haujakua inavyotakiwa. Kadiri tunavyouza bidhaa na huduma nyingi nje ya nchi ndivyo kadiri shilingi yetu inavyopata thamani kubwa. Suluhisho pekee ni kukuza shughuli za uzalishaji kweny kilimo ambapo ndipo Watanzania wengi wamejikita. Mazao ya kilimo yasindikwe tuyauze nje kwa thamani kubwa zaidi. Vijana wote wapatiwe shughuli za uzalishaji (kwenye kilimo, uvuvi, ufugaji, uchimbaji madini na kazi za viwandani) na sio kuwapa mitaji ya kufanya umachinga wakiuza bidhaa za nchi nyingine na kuinua uchumi wa nchi hizo. Ni mpaka pale falsafa ya 'hapa kazi' itakapoweza kuwapa vijana wote kazi ya uzalishaji ndipo maendeleo ya kweli yatakapokuja.

Sent from my SM-J120H using JamiiForums mobile app
 
Kuna tofauti kubwa kati ya thamani ya fedha na nguvu ya sarafu katika soko.

Kwenye uchumi so long as fedha yako haina nguvu ya kimanunuzi katika soko la dunia au unanunua kwa wenzako kuliko unavyowauzia basi hata kama ungepunguza masifuri au kuyaongeza kwenye tarakimu ya fedha yako bado inakuwa haina maana.

Nikukumbushe tu kuwa fedha ya japani inabadilishwa kama sawa na shilingi ya Kenya kwa fedha yetu hapa nchini.

Sasa usidhani kuwa Japani ni nchi yenye uchumi mdogo au fedha yake haina thamani kwa kuwa inalingana na ya Kenya katika exchange rate.

Marekani na Mchina wanagombana kila siku katika hilo.

Kwamba Mchina ameporomosha thamani ya fedha yake kwa makusudi ili iwe na nguvu katika manunuzi na inaihenyesha Dollar ya Marekani kweli kweli.

Hata kama tungefuta masifuri yote kwenye fedha yetu elfu 10 ikabaki kusomeka sh 10 bado kama hatuuzi vingi zaidi ya tunavyonunua ni kazi bure tu.

Sent by Bilionea ASIGWA mutu ya hela Mingi
Uchumbuzi wako una mkanganyiko!

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Tambua BOT si mali ya watanzania. Ni mali ya Illuminatti/Jesuits wa Vatican, Hao jamaa wanaimiliki hadi Federal Reserve bank ya USA za zingine zote Duniani...
Mkuu unaweza kufafanua vizuri haya, japo tupate mwanga.
 
Aisee, please tell us more kaka!

Ni kwanini Tshs iko chini?
Thamani ya Tsh iko chini si kwa mapenzi yetu, ila ni kwa mapenzi ya wenye hizi nchi kupitia Central Bank (BOT) wanafanya manipulation kwenye uchumi wa nchi ili political agenda zao zikubalike na nchi. Mfano Tanzania tungeruhusu uhuru wa vyombo vy a habari na kuruhusu uhuru wa jinsia yaani ushoga na usagaji basi value ya pesa ingeongezeka. Zimbawe Mugabe alifuata matakwa ya wananchi kuwanyang'anya wazungu mashamba kilichofuata ni kuiporomosha thamani pesa ya Zimbabwe. Katika uchumi wanadai kuwa thamani ya dollar inategemea na demand ya dollar yenyewe sokoni lakini ukija kwenye reality haina ukweli wowote na value ya currency husika. Hawa Illuminatti wakikupenda wanaweza kukufanya kuwa super rich kama walivyoziwezesha nchi za Asia pacific kama China, Singapore nk ili kuipunguzia strengh USA kupitia NAFTA kuhamisha workforce USA na Canada kuipeleka China.
Hata biashara ya Masoko ya Fedha iliyopo kwenye masoko ya kimataifa yanakuwa controlled na wenye mifumo yao ya fedha ya Online. yaani wanachofanya ni kuangalia jinsi watu walivyo pump Pesa kwenye uchumi then wana punguza thamani ili watu msiwe matajiri sana. Ndo maana hawa jamaa walimuua Gaddaffi kwa vile Gaddafi yeye pesa yake alikuwa anainunulia Gold na madini mengine ya thamani ili Utajiri wa nchi uwe dhahiri, kuliko kutegemea paper money ambapo dakika yoyote Illuminatti waliamua kui disvalue unajikuta huna kitu.
 
Wanajamvi haswa wachumi nilikuwa naomba kuuliza, hivi kwa mfano Tanzania ikiamua kufuta pesa zake zote na kuanzisha currency mpya labda tukaiita KIDAKA, sasa tukaamua kwamba dola moja iwe sawa na KIDAKA mbili, je inawezekana? na kama haiwezekani ni kwanini? kwani nani anasimaia uanzishwaji wa currency mbona watu wana currency wanaziita kikwao kama kwacha, reale au yen? je wakati zinaanza zilikuwa chini hivyo hivyo? Dah ebu WACHUMI nisaidieni
Inawezekana.

Ila kinachokuza uchumi ni uzalishaji. Si thamani ya hela.

Tukienda soko la dunia mafuta yanauzwa kwa dola za Kimarekani. Wajapani wanaponunua mafuta kutoka Saudi Arabia wananunua kwa dola za Kimarekani. Hawatumii Japanese Yen au Saudi Riyals.

Dola ya Kimarekani ndiyo hela inayotumika sana katika biashara ya kimataifa.

Sasa kama leo dola moja ni Sh 2500, kesho dola moja iwe nusu Kidaka, basi hiyo Kidaka moja itakuwa inabadilishwa kwa shilingi elfu tano za zamani tu.

Zaidi, kuwa na hela yenye thamani kubwa si automatically kuwa na uchumi mzuri.

China kwa miaka mingi wamejitahidi sana hela yao isipande thamani.

Ndiyo. Nchi inaweza kujitahidi hela yao isipande thamani. Tena wamefanya hivyo mpaka Marekani wamelalamika sana kwamba Wachina wanaishusha hela yao thamani makusudi. Waziri wa Fedha wa Obama Timothy Geithner alilisema hili. Donald Trump amekuwa akilisema hili miaka mingi sana na mpaka leo analisema.

Kwa vipi nchi itake hela yake isipande thamani?

Hela ya nchi ikipanda thamani, kuuza bidhaa za nchi hiyo nje inakuwa vigumu sana. Nitakupa mfano.

Ki hamburger cha Marekani ni rahisi sana kufika $2 Marekani. $2 Marekani kutoa kununua hamburger, na $2 nyingine kutoa kununua juisi ukapata lunch ya kujibana actually umekula mlo cheap sana hapo. Kwa wastani unaweza kula lunch ya $6 na kama unataka kutanua unaweza kufikisha hata $30. Sasa fanya hesabu za mtu wa kawaida bongo ki humburger karibu sh 5,000 na kijuice karibu sh 5,000 nyingine. Hiyo hapo ni very cheap lunch ushaondoa sh 10,000. Comparison nikiendeleza unakuta $6 ni karibu sh 15,000 na $30 ni karibu sh 75,000

Ndiyo maana McDonalds ya Marekani haiwezi kuanzisha franchise Dar na kuuza vitu kwa bei za Kimarekani. Hawatafanya biashara kwa sababu dola ina nguvu sana.

China wanakataa kupandisha Yuan kwa sababu China ni a giant exporter. Moja ya sababu unaona kila kitu ni "Made in China" ni kwa sababu Dola moja ni 6.78 Yuan. Wakiipandisha sana thamani Yuan iwe karibu aubiizidi dollar, watashusha exports uchumi utadorora.

Wao kuuza vitu nje kwa urahisi ni muhimu kuliko thamani ya hela yao kuwa kubwa sana.

Kwa hiyo, kuwa na hela yenye thamani sana kunaweza kuharibu uchumi.

Kinachopandisha uchumi si thamani ya hela, ni uzalishaji na kuuza vitu nje.

Nchi inaweza kuwa na hela ambayo haina thamani sana ikawa na uchumi mzuri kuliko nchi yenye hela yenye thamani sana.

Ila, tatizo letu ni kwamba, tuna hela isiyo na thamani, halafu hatuna uzalishaji wa ku export kwa sana. Hii wanaita "the worst of both worlds". Tunapigwa kwa kuwa na hela isiyo na thamani, halafu tunapigwa tena kwa kukosa uzalishaji.

Tungepigwa kumoja tu kwa kuwa na hela isiyo na thamani wakati upande wa uzalishaji tuko fiti, tungeweza ku revenge kwa kutumia hela isiyo na thamani kuongeza exports kama wanavyofanya China. Mpaka tufanye kuwa na hela isiyo na thamani kutusaidia kiuchumi.

Lakini hatufanyi hivyo. Nchi ambayo ina hela isiyo na thamani halafu haina uzalishaji mzuri, inapata matatizo sana inapoagiza vitu kutoka nje. Kwa sababu hela yake haina thamani. Ikienda kununua dola dola zinakuwa za bei ya juu sana. Ikienda kununua mafuta mafuta yanakuwa ya bei ya juu sana. Na kwa vike haina uzalishaji sana, ikitegemea imports, uchumi unashuka.

Geithner Hints at Harder Line on China Trade

Exclusive: Trump calls Chinese 'grand champions' of currency manipulation

Sent from my Kimulimuli
 
Kwanza cha kujiuliza ni nini kinasababisha fedha kupanda thamani au kushuka yenyewe.

Pili nini kinasababisha taifa kupitia benki yake ipandishe au kushusha thamani ya sarafu yake dhidi ya sarafu za nchi nyingine.

Nikianza na swali la kwanza kanununi ni ileile kadri unavyohitaji sarafu za nje ndivyo thamani yake inapanda kwako.

Mfano leo hii mahitaji ya dolla nchini kwetu yakipungua inamaana thamani ya dolla itashuka dhidi ya shilingi ndio kwanini tuinunue bei kubwa ili hali hatuihitaji?

Uzarishaji wa ndani japo hili linajenga zaidi hilo la juu, kama tunadharisha na kujitoshereza kwa bidhaa mfano za viwandani kwa bei nafuu inamaana bidhaa toka nje zitakosa soko huku kwetu watalazimika kushusha thamani ya pesa yao kama ushindani wa kibiashara dhidi ya bidhaa zetu na automatically sarafu yetu itakuwa imepanda thamani. Na hili nadhani linajibu swali la pili pia.

Nini kitatokea kama Tanzania itapandisha thamani ya sarafu yake ilingane na dola? Uchumi utaanguka, sababu viwanda vyote lvitakufa, kwanini vife sababu bidhaa toka nje itakuwa nafuu mno mara 2000 ya sasa, yaani bidhaa unayonunua 100, 000 hapa utaipata kwa tsh 50 tu nje ya hapa nani atanunua ya hapa? Unaweza kuagiza nyama china mpaka hapa na bado ikawa nafuu sana kuliko nyama inayouzwa buchani temeke kwanini ununue temeke? Hakuna biashara itafanyika hapa hence uchumi wa ndani utakufa kabisa,

Lkn pia sahau kuuza nje ya nchi bidhaa yoyote.

Sijui nimekata kiu ya swali? Japo sijatulia kueleza in details na mifano hai.



Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
 
Mfano mwingine ni nchi ya Nigeria kulipa madeni ya nchi yote inayodaiwa, walifanikiwa kulipa madeni hayo kutokana na utajiri wa mafuta lakini kilichofuata ni kuleta mgogoro wa mafuta, yaani nchi inazalisha mafuta ya kutosha lakini magari yanapanga foleni kujaza gas, na mgogoro wa Vita ya wenyewe kwa wenyewe na magaidi wa Boko haram pamoja na jimbo la Biafra kutaka kujitenga. Lengo ni kuhakikisha nchi inaingia kwenye bad political state ambayo mwisho wa siku hakuna ahueni ya maisha kwa wananchi.

Hata madini yetu yangekuwa yanapitia BOT ili hesabu ya mauzo ya nje yaani Foreign Export igekuwa inaonyesha gharama ya mauzo, wachambuzi wanasema labda ingefanya thamani ya shillingi iwe juu dhidi ya dollar, lakini hata hilo likifanyika halitawezesha shillingi yetu kupanda. Hakuna nchi rahisi kuishi kama tanzania. kwa vile ina hali ya hewa mtu yeyote hata masikini anaweza kuishi hata kama hana pesa za kununua nguo, na hata masikini anaweza kuishi kwa kulima kwa vile mvua na ardhi ipo, ndo maana bado dollar haijawa mbaya sana, na watanzania hata ukiishusha thamani ya shillingi tuna mifumo ya kienyeji ya kuishi pasipo kuwa tegemea hao illuminatti, hatuhitaji import ya chakula, tunalima wenyewe nk.

Kupitia Central bank Illuminatti wanachapa hizi currency na kuzikopesha nchi kwa kusign bond ya masharti nafuu, na madeni hayo huwa hayalipiki na kuzifanya serikali ziendelee kukopa na kukopa. Marekani yenyewe pamoja na utajiri wake wote inadaiwa na hawa Illuminatti 16Trl. Dollar pesa nyingi ambazo hazilipiki, Na deni hili linawarudia wananchi kwa kulipa kodi nk. japo pesa hizi zimepatikana kwa ku print tu, hii ni siri ya Illuminatti amabyo hawataki watu wajue.

Ndo maana napenda sana Magufuli anavyokusanya kodi lakini asiishie kutaka sifa ya kulipa madeni, yeye awakope sana afu kilipa kidooooogo, Ili tuwaingize mkenge hawa illuminatti.
 
Wachumi mtufafanulie taratibu tuelewe? Kwa mini sh ya Kenya INA nguvu kuliko ya tz?
 
Wachumi mtufafanulie taratibu tuelewe? Kwa mini sh ya Kenya INA nguvu kuliko ya tz?
Kwa sababu Wakenya wanaweza kujitegemea zaidi ya Watanzania na hawahitaji kununua vitu vya nje na misaada ya nje kama Watanzania.

Hii inaitwa "balance of trade". Wakenya wanazalisha ndani zaidi yetu. Urari wao wa kuuza nje kutoka ndani na kuagiza ndani kutoka nje ni mzuri kuliko wetu. Nimeweka link ya balance of trade mwisho wa post hii.

Thamani ya fedha inaendana na uzalishaji na uwezo wa kujitegemea.

Rais Kenyatta amejigamba kwamba bajeti ya Kenya haijatumia hela yoyote ya msaada kutoka nje.

Magufuli hajafikia kusema hivyo.

Unavyohitaji vitu vya nje zaidi ndivyo unavyozidi kuhitaji hela za nje zaidi, ndivyo unavyozinunua zaidi. Unavyozinunua zaidi kwa kutumia shilingi yako, ndivyo unavyozipandisha thamani zaidi kulinganisha na hela zako kwa kanuni za kiuchumi za supply, demand and price.

Thamani ya shilingi pia ilianza kushuka kwa kasi baada ya vita vya Kagera na matatizo ya kiuchumi ysliyofuatia vita hiyo.

Kenya haijawahi kupigana vita.

Soma

How does the balance of trade impact currency exchange rates?

Sent from my Kimulimuli
 
Back
Top Bottom