Shilingi Bilioni 3 Kudhamini Jezi za Timu ya Taifa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

SHILINGI BILIONI 3 KUDHAMINI JEZI ZA TIMU ZA TAIFA; DKT. NDUMBARO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuendelea kuwatumia wawekezaji wa ndani kutengeneza jezi za mpira wa miguu wa timu za Taifa.

Dkt. Ndumbaro ametoa pongezi hizo Septamba 11, 2023 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Udhamini wa Jezi za Timu za mpira wa miguu za Taifa kati ya TFF na Sandaland Fashion Wear Ltd wa thamani ya Shilingi Bilioni 3 kwa muda wa miaka 5.

"Naipongeza Sandaland kwa kushinda zabuni hii, natoa rai kwenu kuongeza juhudi mfike nje ya mipaka ya Tanzania kwa kupata zabuni za kutengeneza jezi za klabu na timu za Taifa, naamini mtafanya hivyo" amesema Dkt. Ndumbaro.

Ameipongeza TFF kwa kusaini mkataba huo ambao utakua unawapa fedha, na kusisitiza kuwa uongozi wa Rais Walles Karia umefanikisha Tanzania kufuzu AFCON mara 2, timu ya Wanawake chini ya Miaka 17 na timu ya watu wenye ulemavu Tembo Warriors zimefika robo Fainali ya kombe la Dunia, huku Timu ya Wasichana ya Shule ya Sekondari ya Fountain Gate ya Dodoma, kuibuka mabingwa wa mashindano ya soka ya shule za Afrika ya CAF.

Kwa upande wake Rais Karia amesema Mkataba huo utahusisha Timu zote za Taifa za Mpira wa Miguu, ikiwa ni utekekezaji wa maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka wawekezaji wazawa kupewa nafasi zaidi nchini, ambapo amesema wataongeza wadhamini wengi katika maeneo mbalimbali kama ilivyo pia katika Ligi Kuu.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Sandaland Mhe. Yusuph Yenga amesema Kampuni hiyo ina uzoefu wa kutengeneza jezi hapa nchini ambapo tayari wana Mkataba timu ya Simba na kuahidi kuwa jezi hizo zitakuwa na ubora na viwango vya hali ya juu.

WhatsApp Image 2023-09-12 at 01.12.11.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 01.12.12(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 01.12.12.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 01.12.11(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 01.12.11(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 01.12.10.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 01.12.10(1).jpeg
F5w1dQjWcAAq9Hp.jpg
F5w1eF0XAAAKp2W.jpg
 
Sina maana ya kubeza udhamini huu, lakini ifike wakati tutazame mambo kwa hatua kadhaa mbele. Hivi tumeshindwa kabisa kuwavuta wadhamini wakubwa huko kina adidas, nike n.k?

Wanavokuja wale maraisa wa FIFA, sijui watendaji wakubwa wa FIFA, ma CEO huko hatujishughulishi hata kuwauliza A,B,C ambazo ni nzuri nasi tukapata hata pa kuanzia au tunapiga nao picha tu kisha wanaondoka?

Sent from my SM-A536E using JamiiForums mobile app
 
Hamtaki watanzania wenzenu wakue kibiashara ?
 
SHILINGI BILIONI 3 KUDHAMINI JEZI ZA TIMU ZA TAIFA; DKT. NDUMBARO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuendelea kuwatumia wawekezaji wa ndani kutengeneza jezi za mpira wa miguu wa timu za Taifa.

Dkt. Ndumbaro ametoa pongezi hizo Septamba 11, 2023 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Udhamini wa Jezi za Timu za mpira wa miguu za Taifa kati ya TFF na Sandaland Fashion Wear Ltd wa thamani ya Shilingi Bilioni 3 kwa muda wa miaka 5.

"Naipongeza Sandaland kwa kushinda zabuni hii, natoa rai kwenu kuongeza juhudi mfike nje ya mipaka ya Tanzania kwa kupata zabuni za kutengeneza jezi za klabu na timu za Taifa, naamini mtafanya hivyo" amesema Dkt. Ndumbaro.

Ameipongeza TFF kwa kusaini mkataba huo ambao utakua unawapa fedha, na kusisitiza kuwa uongozi wa Rais Walles Karia umefanikisha Tanzania kufuzu AFCON mara 2, timu ya Wanawake chini ya Miaka 17 na timu ya watu wenye ulemavu Tembo Warriors zimefika robo Fainali ya kombe la Dunia, huku Timu ya Wasichana ya Shule ya Sekondari ya Fountain Gate ya Dodoma, kuibuka mabingwa wa mashindano ya soka ya shule za Afrika ya CAF.

Kwa upande wake Rais Karia amesema Mkataba huo utahusisha Timu zote za Taifa za Mpira wa Miguu, ikiwa ni utekekezaji wa maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka wawekezaji wazawa kupewa nafasi zaidi nchini, ambapo amesema wataongeza wadhamini wengi katika maeneo mbalimbali kama ilivyo pia katika Ligi Kuu.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Sandaland Mhe. Yusuph Yenga amesema Kampuni hiyo ina uzoefu wa kutengeneza jezi hapa nchini ambapo tayari wana Mkataba timu ya Simba na kuahidi kuwa jezi hizo zitakuwa na ubora na viwango vya hali ya juu.

View attachment 2746405View attachment 2746406View attachment 2746407View attachment 2746408View attachment 2746409View attachment 2746410View attachment 2746411View attachment 2746412View attachment 2746413
Sawa
 
Sina maana ya kubeza udhamini huu, lakini ifike wakati tutazame mambo kwa hatua kadhaa mbele. Hivi tumeshindwa kabisa kuwavuta wadhamini wakubwa huko kina adidas, nike n.k?

Wanavokuja wale maraisa wa FIFA, sijui watendaji wakubwa wa FIFA, ma CEO huko hatujishughulishi hata kuwauliza A,B,C ambazo ni nzuri nasi tukapata hata pa kuanzia au tunapiga nao picha tu kisha wanaondoka?

Sent from my SM-A536E using JamiiForums mobile app
Mkuu adidas ,au nike original ,bei yake tutaweza kweli ?
 
Huyo aliyesimama upande wa Sandaland akisaini, amekula mawani na Kaunda suit ya kijivu na black isiyoeleweka ni Kaka yake na Sandaland. Ni naibu meya wa jiji la hovyo (DAR)... na mwenyekiti wa Wafanyabiashara kariakoo. Ana pesa chafu na ni TISS mbobevu! Nyuma yake/yao kuna watu wazito na watu wazito hao ni washkaji wao vilevile. Majamaa wana pesa ila mkatili sana!

Anyways!... hizo B3 naona kama kuna upigaji hapo 🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom