Shida ya Maji jijini Tanga

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,149
6,989
Nimetembelea katika jiji la Tanga,nimekumbana na tatizo kubwa la maji.Katika kumbukumbu zangu jiji hili,halijawahi kuwa na tatizo la maji.Inasemekana sasa ni wiki ya pili,maji hayatoki katika mabomba ya jiji hilo.
Wakazi wa jiji hili,walisema wanatumia maji ya visima,vilivyopo kwenye misikiti ya jiji hilo,pamoja na maji mvua.
 
Ni kweli. Tanga UWASA inakufa kifo cha mende. Taabu tupu. sehemu zingine ni almost a month with no running water!
 
Aisee poleni mimi hapa ninapoishi maji yapo 24/7 ni hapa hapa Tanga karibu na Tanga Cement
 
Unayosema ni kweli kuhusu tabu ya maji na baadhi ya maeneo inawapasa kuamka usiku kulindia maji, na wakati mwengine hata yakitoka yanakuwa machafu hali inayosababisha magonjwa ya tumbo.
 
Mbona ulishindwa kufika mamlaka ya Maji kuulza hilo jambo ili ulete habar iliyonyooka. Wewe unatembea tu mitaani.
Kufanya nini, kwani wao hawajui kuwa water is not pumped in their pipes. Kilichobaki ni kuomba msaada ngazi za juu. Tanga haikuwa ha shida ya maji , Magufuli will be the answer. Let other engineers try, !
 
Nimetembelea katika jiji la Tanga,nimekumbana na tatizo kubwa la maji.Katika kumbukumbu zangu jiji hili,halijawahi kuwa na tatizo la maji.Inasemekana sasa ni wiki ya pili,maji hayatoki katika mabomba ya jiji hilo.
Wakazi wa jiji hili,walisema wanatumia maji ya visima,vilivyopo kwenye misikiti ya jiji hilo,pamoja na maji mvua.
Jiji limekuwa na ongezeko kubwa la watu tofauti na miaka nyuma , halafu vyanzo vya maji vimebaki vile vile ,
 
Nimefikia Tanga mjini,wenyeji wa hapa wanasema maji yalikuwa yakitoka machafu,yenye tope,baadaye hayakutoka kabisa.
Basi ni shida kwenye baadhi ya maeneo mkuu sio pote, hata hivyo mamlaka zihakikishe zinatatua tatizo maana maji ni muhimu hata kushinda umeme.
Najua changamoto hiyo imetokana na mvua kusababisha kuziba kwa mabomba hasa kutoka huko kwenye vyanzo ambako ni milimani, hata mvua zikinyesha hua maji yanatoka na mchanganyiko wa matope kutoka na kuvurugika huko kwenye vyanzo
 
Jiji limekuwa na ongezeko kubwa la watu tofauti na miaka nyuma , halafu vyanzo vya maji vimebaki vile vile ,
Kwa taarifa nilizopata,jiji hili lilikuwa na visima vikubwa,viko barabara 14,ndio ilikuwa chanzo kikuu cha maji katika jiji hili,kabla ya kutumia maji ya mto.Labda mamlaka zinazohusika warudie kutumia chanzo hiki tena.
 
Tanga UWASA wako kimya bila kueleza sababu ya maji kutoka machafu na maeneo mengine kutopatikana kabisa. Miaka ya nyuma wakati wa mvua maji yalikuwa yanatoka kama kawaida na ni masafi. Kuna tatizo mahali fulani.
 
Kwa taarifa nilizopata,jiji hili lilikuwa na visima vikubwa,viko barabara 14,ndio ilikuwa chanzo kikuu cha maji katika jiji hili,kabla ya kutumia maji ya mto.Labda mamlaka zinazohusika warudie kutumia chanzo hiki tena.
Hivo visima vikubwa 14 wakati vinajengwa Jiji lilikuwa na watu mfano 30,000 ila kwa sasa Jiji lina wakazi labda ya watu 200;000 ... bado hivo visima havitaweza kuwapatia maji wakazi wote kama zamani...
 
Lakini kiasi fulani vingesaidia kupunguza makali ya kukosekana kwa maji.Kwa mfano hivi sasa wenyeji wanasema visima vya umeme vya misikiti ndio vinavyowasaidia sasa.Bahati nzuri jiji hili kila mtaa huwezi kukosa msikiti,na misikiti yote ina visima hivi vya maji yanayovyutwa kwa pump za umeme.
 
zaman kukuwa na tatizo tulikua twatangaziwa.ila sasa ni butuabutua.asubuh unaamka maji hakuna.yakitoka unaweza mwaga ukijua watoto wameyatia tope!!
 
Back
Top Bottom