Shibuda kuondolewa CHADEMA leo

Shibuda kuondolewa CHADEMA leo

Status
Not open for further replies.
Shibuda sio #KIRUSI ndani ya chadema pekee. Woote wenyekutaka kujenga usawa nasiasa za kweli ndani ya chadema ,HUWA KIRUSI DAIMA. Ubwanyenye mtupu mle ndani.
 
Shibuda ni nyambizi mwenyewe alishakiri ni nyambizi ndani ya chadema
 
Samahani naona hapa watu wanazungumza kuhusu "chadema", hivi ni nini ama ni kitu gani hicho!? au labda ni wale waimbaji wa nyimbo za taarabu waliokuwa wakiimba pamoja na bibi kidude enzi zile!? Tafadhali naomba mwenye kujua zaidi kuhusiana na hili anijuze!
 
Naamini baada ya Chadema kumuondoa Zitto, they have learned their lesson by now!, kama wakimuondoa Shibuda sasa, then nitaamini Chadema will never learn!.

Ndani ya uongozi wa Chadema, kuna watu wenye busara sana, ambao kabla ya kufanya jambo, watafanya calculations za kitu kinachoitwa "risk mitigations" ili kuavoid "some negative consequences!", hivyo thay will advise chama do do the right thing, at the right time and do it right!. Ila pia ndani ya safu ya uongozi wa Chadema, kuna fools kibao!, na wengine ni vichaa kabisa!, thank God, kwenye kugombea uongozi, imetamkwa tuu "mtu mwenye akili timamu!", lakini hakuna kipimo chochote cha utimamu wa akili kinachofanyika!, ingekuwa wabunge wetu wanapimwa akili!, saa hizi wengi wa vichaa hawa wangelikuwa mahali panapowastahiki!.

Sasa kama Chadema hili hawalijui kuwa miongoni mwao kuna wenye busara, na kuna vichaa, hivyo wanapokaa kufanya maamuzi, wakiendelea kuupokea ushauri wa hao vichaa wao, bila wao kama chama kuwajua ni vichaa!, thai is their own funeral!.

Huu ukichaa, hauishii kwa viongozi tuu, umeshuka chini hadi kwa wanachama, wafuasi na mashabiki wao, wakiwemo hawa walio humu jf, wengi tuu ukiwasoma, utangundua ni vichaa kabisa, ila sio lazima mpaka hadi waokote makopo!.

Mingoni mwa viongozi vichaa wa Chadema, ni huyu mlengwa anaetakwa kufukuzwa!. Kuna type fulani ya vichaa, "they are better when contained than when let loose!", kwa formula ya "keep your friends close, your enemies closer!", Shibuda needs to be contained than let loose!", Shibuda sio Zitto, amefanyiwa tote aliyofanyiwa lakini amejinyamazia tuu, kwa sababu there is "brain in his head!", Shibuda ni "empty" kabisa, kumfukuza ni kama kumfungulia mbwa mwenye kichaa!, Chadema itaishia kuwa "embarrassed!.

Pasco.
usitufundishe uoga wewe tapeli....natambua uhusiano wako na Shibuda lakinitukitaka kumwondoa tuta mwondoa na hatuna cha kuhofia...
 
huelewi nini hapa? mwanachama halisi wa chadema ni mchaga. ndo maana lema pamoja na kutokuwa na cheo chochote katika chaguzi zilizofanyika anajua ya ndani zaidi kuliko hata Prof. Safari au Mwanasheria lisu na ndo maana anaweza kuongea hata kwenye vyombo vya habari. umesahau ya akina Zitto yeye ndo alianzisha kuutangazia umma?

Wanaenda kujadili nini juu ya Shibuda kama tayari amesha sema wanamuondoa?

Kina anaehamia cdm ni pandikizi?
Kama ndio hivyo mwana cdm halisi ni nani?
Au kauli hizi zinatumika makusudi ili kuendelea kushikilia chama?

Any way, long live cdm, tupate maendeleo ya kweli.
 
Tarehe 19 Machi 2013 Niliandika Hivi hapa Jamvini.

Kwa kifupi ningependa nitoe wosia kwa vyama vya SIASA hasa vyama vya Upinzani na hasa CHADEMA.

Imetokea kasumba ambayo imekuwa inakuwa kwa kasi ya ajabu ndani ya vyama vya upinzani. Ndani ya vyama vya upinzani umetokea upepo wa kutokuaminiana, kumetokea wimbi kubwa la kutuhumiana USALITI miongoni mwa wanachama. Mtu akionekana kuwa amekuwa na mawazo tofauti na wenzake hata anapokuwa tofauti na kundi dogo tu ndani ya Chama au na kiongozi mmoja tu ataitwa msaliti na kundi la upande wa pili. Wakati mwingine hata utofauti wa Hoja humfanya mwanachama mmoja aitwe msaliti.

Mtiririko wa matukio ya kuitana wasaliti ndani ya CHADEMA nilianza kuyasikia uchaguzi wa BAVICHA, baadaye tukayasikia akituhumiwa mheshimiwa Shibuda, yakaenda kwa Mh. Zitto Kabwe, yakamaliza na kuwachinjia baharini akina Mtela Mwampamba na Juliana Shonza na kundi lake,

Historia inanikumbusha ni suala la tuhuma za Usaliti zilizoisambaratisha NCCR- Mageuzi, chama kilichokuwa maarufu miaka yetu ya 90. Kundi la Mrema liliwatuhumu kundi la Mabere Marando kuwa ni wasaliti na Kundi la Mabere Marando lilimtuhumu Augustino Mrema na kundi lake kuwa wanatumiwa na CCM na Serikali. Kutokana na tuhuma hizo, viongozi na wanachama wa kila kundi wakawa busy na kupanga mashambulizi dhidi ya kundi lingine kila kukicha. Hatima yake ni kurushiana viti na majaribio ya kutaka kuuana katika Hotel ya Mkonge huko Tanga na huo ukawa ndio mwanzo wa kifo cha NCCR-MAGEUZI.

Ninaona tatizo hili linainyemelea CHADEMA, tatizo hili linahitaji kutibiwa, CHADEMA inahitaji kujenga demokrasia ya kukosoana bila kuchukiana na kuhisiana vibaya. Wanachama wa CHADEMA wamekuwa waoga kutoa mawazo yatakayokinzana na wanachama wenzao na hasa viongozi fulani fulani kwa kuogopa kuitwa wasaliti.

Na kutokana na udhaifu huu ni rahisi sana adui kupenya. Kwa mfano katika mkanda wa video unaonyesha Lwakatare akipanga njama za kuteka, kushambulia na kudhuru mtu. Sababu inayotajwa kuandaliwa kwa mkakati huo ni Zitto Kabwe. Kuwa Mh. Lwakatare alikuwa anapanga njama za kigaidi dhidi ya mwandishi wa habari kwa kile kilichosemwa ukaribu wake na Zitto. Sasa unajiuliza shida iko wapi kuwa karibu na Zitto Kabwe, majibu katika video hiyo hiyo yanasema anadhofisha juhudi za chama, kwa kifupi ni msaliti.

Sijui kama video hiyo ya kweli au si ya kweli, na wala sihitaji kujua hilo, Lakini, Sababu ya hisia za USALITI ndio chanzo cha uwepo wa video hiyo. Sasa kama video hiyo ni ya kweli, basi utaona kuwa idara nzima ya ulinzi na usalama chini ya Lwakatare ilivyopoteza dira, Badala ya kushughulikia ulinzi na usalama wa chama kutoka kwa maadui wa kweli imejikita kwenye hofu hofu ya kusalitiwa. Kama hiyo video sio ya kweli utaona kuwa maadui wametumia kuwepo kwa hali ya kutokuaminiana ndani ya CHADEMA na hivyo imewezekana kutengeneza video hiyo kwasababu ya mwanya uliotengenezwa na CHADEMA yenyewe, mwanya wa hisia za usaliti.

Sasa hivi ndani ya CHADEMA ili uonekane wewe ni mwanaharakati wa kisiasa wa kweli, na mpenzi wa CHADEMA wa kweli ni lazima uongelee watu wanaohujumu jitihada za chama, lazima uzungumzie watu unaodhani hawako upande wenu. Sasa wanachama wa CHADEMA hawazungumzii tena Itikadi ya chama, Hawazungumzi tena hoja za mipango mikakati ya chama inayohusiana na maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, watu wako busy na nani anatuangusha wapi na kwa vipi na wasababu zipi.

Sasa badala ya kuwa kwenye mapambano dhidi ya mpinzani wa CHADEMA anayefahamika CCM mapambano yamebadirishwa na kuwa ni mapambano kati ya kundi moja la CHADEMA dhidi ya kundi lingine la CHADEMA, hii ni HATARI sio tu kwa CHADEMA yenyewe bali hata kwa ustawi wa Demokrasia ya nchi yetu na Afrika kwa ujumla.

Niwasihi viongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA warudishe ajenda muhimu kwenye meza za mazungumzo za wanachama wao, kufanya juhudi za makusudi za kuondoa hisia za hujuma na usaliti na kuwafanya wanachama wajione wao ni kitu kimoja, wenye nia na lengo moja wanaoenda njia moja.
 
Mbunge wa Arusha mjini Mh Godbless Lema alisema hawataweza kuvumilia kuwaona wasaliti wakiendelea kudumu ndani ya chama hicho!!!Alisema hawatasita kuchukua hatua kwa yeyote anakiuka taratibu za chama akiwatolea mifano ya mh Zitto;Mwigamba;Mkumbo & etl!!!!Aliongeza kuwa wanda kukaa n kutoa maamuzi juu ya Shibuda!!!!! "Jumanne tarehe 14 tuakaa tutaamua hatima ya Shibuda;lazima aondoke"!Alisema

Maoni yangu: Chadema isimwonee haya vibara na vipandikizi vilivyoko ndani ya chima hicho.

Kutenda kosa sio Kosa ila kurudia kosa. Je wamezingatia taratibu za kikatiba safari hii??
1. Kumpa mashataka yake kwa maandishi
2. Kupewa siku 14 za kujieleza
3. katibu kupokea utetezi wa mtuhumiwa kwa maandishi
4. katibu kujiridhisha na utetezi huo kuwa pasipokuacha shaka mtuhumiwa ana kosa la kujibu
5. Kumpa taarifa ya uwepo wa kamati kuu kumjadili
6. Kumuita kujieleza mbele ya Kamati kuu kwa kumpa notice ya kuitwa shaurini inayoeleza kinagaubaga tuhuma zake
7. Kupata nafasi ya kujitetea mbele ya kamati Kuu??
 
Naamini baada ya Chadema kumuondoa Zitto, they have learned their lesson by now!, kama wakimuondoa Shibuda sasa, then nitaamini Chadema will never learn!.

Ndani ya uongozi wa Chadema, kuna watu wenye busara sana, ambao kabla ya kufanya jambo, watafanya calculations za kitu kinachoitwa "risk mitigations" ili kuavoid "some negative consequences!", hivyo thay will advise chama do do the right thing, at the right time and do it right!. Ila pia ndani ya safu ya uongozi wa Chadema, kuna fools kibao!, na wengine ni vichaa kabisa!, thank God, kwenye kugombea uongozi, imetamkwa tuu "mtu mwenye akili timamu!", lakini hakuna kipimo chochote cha utimamu wa akili kinachofanyika!, ingekuwa wabunge wetu wanapimwa akili!, saa hizi wengi wa vichaa hawa wangelikuwa mahali panapowastahiki!.

Sasa kama Chadema hili hawalijui kuwa miongoni mwao kuna wenye busara, na kuna vichaa, hivyo wanapokaa kufanya maamuzi, wakiendelea kuupokea ushauri wa hao vichaa wao, bila wao kama chama kuwajua ni vichaa!, thai is their own funeral!.

Huu ukichaa, hauishii kwa viongozi tuu, umeshuka chini hadi kwa wanachama, wafuasi na mashabiki wao, wakiwemo hawa walio humu jf, wengi tuu ukiwasoma, utangundua ni vichaa kabisa, ila sio lazima mpaka hadi waokote makopo!.

Mingoni mwa viongozi vichaa wa Chadema, ni huyu mlengwa anaetakwa kufukuzwa!. Kuna type fulani ya vichaa, "they are better when contained than when let loose!", kwa formula ya "keep your friends close, your enemies closer!", Shibuda needs to be contained than let loose!", Shibuda sio Zitto, amefanyiwa tote aliyofanyiwa lakini amejinyamazia tuu, kwa sababu there is "brain in his head!", Shibuda ni "empty" kabisa, kumfukuza ni kama kumfungulia mbwa mwenye kichaa!, Chadema itaishia kuwa "embarrassed!.

Pasco.

Analysis yako ni sahihi juu ya shibuda, ni kweli Shibuda ni empty na resourseful kwa masisiem. Shida ni namna za kumhandle unayoona ya kumweka karibu na CDM, hapa hupo sahihi, labda unge shauri chadema iwe imejitayarisha kwa kusafisha uharo wa shibuda. After all, chadema walishajitahidi sana kumvulilia nadhani ni kwa ajili za ruzuku inazotokana nayeye kuwepo. I agree Shibuda is a rabid dog na unajua wale virusi vza kichaa cha umbwa kifo ni asilimia 100, nafuu ebola hata ndui
 
Shibuda mbona siku nyingi alishajifukuzisha na kama akiendelea kubaki cdm narejesha kadi yangu
 
Naamini baada ya Chadema kumuondoa Zitto, they have learned their lesson by now!, kama wakimuondoa Shibuda sasa, then nitaamini Chadema will never learn!.

Ndani ya uongozi wa Chadema, kuna watu wenye busara sana, ambao kabla ya kufanya jambo, watafanya calculations za kitu kinachoitwa "risk mitigations" ili kuavoid "some negative consequences!", hivyo thay will advise chama do do the right thing, at the right time and do it right!. Ila pia ndani ya safu ya uongozi wa Chadema, kuna fools kibao!, na wengine ni vichaa kabisa!, thank God, kwenye kugombea uongozi, imetamkwa tuu "mtu mwenye akili timamu!", lakini hakuna kipimo chochote cha utimamu wa akili kinachofanyika!, ingekuwa wabunge wetu wanapimwa akili!, saa hizi wengi wa vichaa hawa wangelikuwa mahali panapowastahiki!.

Sasa kama Chadema hili hawalijui kuwa miongoni mwao kuna wenye busara, na kuna vichaa, hivyo wanapokaa kufanya maamuzi, wakiendelea kuupokea ushauri wa hao vichaa wao, bila wao kama chama kuwajua ni vichaa!, thai is their own funeral!.

Huu ukichaa, hauishii kwa viongozi tuu, umeshuka chini hadi kwa wanachama, wafuasi na mashabiki wao, wakiwemo hawa walio humu jf, wengi tuu ukiwasoma, utangundua ni vichaa kabisa, ila sio lazima mpaka hadi waokote makopo!.

Mingoni mwa viongozi vichaa wa Chadema, ni huyu mlengwa anaetakwa kufukuzwa!. Kuna type fulani ya vichaa, "they are better when contained than when let loose!", kwa formula ya "keep your friends close, your enemies closer!", Shibuda needs to be contained than let loose!", Shibuda sio Zitto, amefanyiwa tote aliyofanyiwa lakini amejinyamazia tuu, kwa sababu there is "brain in his head!", Shibuda ni "empty" kabisa, kumfukuza ni kama kumfungulia mbwa mwenye kichaa!, Chadema itaishia kuwa "embarrassed!.

Pasco.
Pasco! Salute! sio i salute you!

Asante kwa mchango huu na hitimisho adhimu maana bila hilo hitimisho leo ungeingia kwenye historia ya jumuiya ya vinyonga au kila sekunde wana rangi mpya.

Japo kila mchangiaji humu yupo kimkakati kunyunyizia bustani ili asikose japo pande la boga pindi yakiiva
ww naona unazidi. Hebu pima pimamaji yako ya uvichaa ulionena waliopo cdm; kisha linganisha na wengine.. pia umevaa wapi udaktari wa kupima ukichaa huo hadi tukuamini usemayo. Je wadai kuwa wewe leo ukijipima na joppo lote ...top brass ya cdm, upo juu yao kiufahamu ??!. wengi huku hatufurahishwi na authoritative contributions of yours!
kama umalenga mbunge adhimu wa A town; rumenoa thats true activist icone of Tz polical transformations. Let cdm do their own to clean their house. Do ur own as well.

kwa hayo machache ; wasalaam ndimi kukuru wa
 
CHADEMA wanakwepa kiini cha tatizo. Tatizo sio SHIBUDA. wameingia ndani ya bunge la katiba bila ya ajenda na walivyotoka nje wameshindwa kushawishi watanzania kujitoa muhanga. Shibuda alikuwa na ajenda ya wakulima na wafugaji. Kura ya maoni itathibitisha alikuwa sahihi pale theluthi mbili ya Tanzania bara itakapo piga kura ya ndio.

Shibuda kipau mbele chake ni masilahi ya wakulima na wafugaji sio kufurahisha CUF kwa kudai serikali tatu.

Sio polisi waliofanya maandamano na migomo ishindwe, bali ni uongozi wa chadema kukosa ushawishi. Unajuwa kabisa kilichofanya maandamano yashindwe kufanikiwa ni viongozi wa chadema kushindwa kushawishi watanzania wasiogope polisi. Viongozi wa chadema wanatakiwa waje na ajenda itakayo gusa hisia na mioyo ya watanzania kiasi cha kuwapa ujasiri wa kupambana na polisi.

Kilichotokea mashariki ya kati (uarabuni) ni watu kuguswa na ushawishi wa wanaharakati; yule mtu aliyejichoma moto mbele ya kituo cha polisi aliwasha moto ambao tayari ulikuwa unangojea kuwaka.

Huwezi kutegemea ajenda ya serikali tatu kumgusa mtanzania wa kawaida ambaye anataabika kupata ugali wake wa kila siku. Mtanzania wa kawaida haelewi serikali tatu itamsaidia vipi au itarahisisha vipi kupata ugali wake wa kila siku. Huwezi kutegemea ajenda ya serikali tatu kumpa ujasiri mtanzania wa kawaida kwenda kupambana na polisi. Na mbaya zaidi pale anapoambiwa kiongozi mwenye ajenda ya serikali tatu kaenda vakesheni nje nchi.

Kama kweli unataka kutoa ushauri wa kusaidia chadema, uongozi unapokosea lazima uwe na ujasiri wa kuwaambia ukweli.

Zaidi ya asilimia 70% ya watanzania ni wakulima na wafugaji, kwahiyo Mh. Shibuda alivyokuwa anawaambia ajenda iwe haki za wakulima na wafugaji alikuwa anatumia uzoefu wake kuwaambia ajenda itakayogusa mioyo ya watanzania ni ile ya wakulima na wafugaji.

Mbowe upeo wake mdogo umeshindwa kuelewa kwamba Tundu Lissu anasifa mbili tu, sifa nyingine muhimu hana, na kumfanya kuwa mshauri mkuu ni makosa. Sifa za Tundu Lissu ni usomi wa sheria na uaminifu. Hana uzoefu wa siasa wala uwezo wa kufanya maamuzi sahihi (He lacks experience and sound judgment).

Unaweza kuona hata humo ndani ya bunge la katiba vipau mbele vya Tundu Lissu au Ukawa vilivyokuwa vinabadilika. Ni kama mtu anayepapasa kwenye giza ambaye hajuwi ashike wapi. Alianza na hati ya muungano haipo, wanaushahidi kutoka umoja wa mataifa kuwa haijapelekwa, wakaamia tunatukanwa ndio maana tunatoka bungeni, baada ya hapo wakasema rasimu inapendekeza serikali tatu lakini CCM wanataka serikali mbili.

Lakini pia ikumbukwe humo ndani ya Bunge ya katiba, kuna wajumbe walihoji utaratibu uliotumika kukusanya maoni ya wananchi kwamba hauwakilishi sura halisi ya matakwa ya wananchi; ukasanyaji maoni ulipuuza baadhi ya maeneo (yaani bad sampling). hivyo hata hayo maoni yaliyoletwa na Warioba yanakosa uhalali kwasababu utaratibu wa ukusanyaji haukuwa sahihi.

Chadema kukosa dira au ajenda inaonekana pia kwenye operesheni zao; ukiangalia operation sangara, movement for change hakuna hata moja tuliyoona imefikia malengo fulani, zinayayuka hewani.

Hapa ndipo unapoona umuhimu wa uzoefu wa watu kama Shibuda. Kama ushauri wao ungekuwa unazingatiwa, sasa hivi CHADEMA ingekuwa inaonekana inapigania haki za wakulima na wafugaji sio serikali tatu ambazo hazi resonate to average Tanzanian. Mtanzania wa kawaida haelewi serikali tatu zitamsaidia vipi kuleta ugali nyumbani.

Msimamo wa kung'ang'ania serikali tatu ni ajenda ya kujenga mahusiano mazuri na CUF lakini sio ajenda ya kumtatulia mtanzania wa kawaida (mkulima, mfugaji, mvuvi) shida zake. Sasa Chadema watuambie watu wa tanzania bara ni masilahi ya kundi gani hayajazingatia katika katiba iliyopendekezwa.
Mkuu Salum, asante, maneno kuntu haya!, tatizo ni uelewa tuu wa wahusika, wanachama wao na wafuasi wao humu!.
Pasco.
 
Nadhani, mleta mada hana taarifa za kutosha juu ya kikao cha Kamati kuu ya CHADEMA na ajenda zake inayoanza kuketi leo na kesho. Let's hope hizi ni hisia zake tu kwa sababu kwa namna yeyote haingii akilini kuwa Shibuda afukuzwe CHADEMA kwa sasa eti ili iweje na ana nini hasa huyu jamaa?

Sibuda hana madhara wala faida yoyote kwa chama kwa kumwacha kama alivyo au hata kama ni kumfukuza/kumvua uanachama. I think ile hali tu ya huyu Shibuda kuwekwa katika orodha ya wanachadema waliokwishakupuuzwa siku nyingi "ignored list" kwake yeye ni adhabu tosha sana kihisia/kisaikolojia.

CHADEMA wala hawana sababu ya kumfanya mtu huyu kuwa ajenda katika kikao cha ngazi yoyote ile kuanzia msingi achilia mbali Kamati Kuu kwa sababu iwe isiwe Shibuda maisha yake ya kisiasa kama mbunge mwisho wake ni mara bunge hili litakapokufa mwakani mwezi July!!
 
Pasco! Salute! sio i salute you!

Asante kwa mchango huu na hitimisho adhimu maana bila hilo hitimisho leo ungeingia kwenye historia ya jumuiya ya vinyonga au kila sekunde wana rangi mpya.

Japo kila mchangiaji humu yupo kimkakati kunyunyizia bustani ili asikose japo pande la boga pindi yakiiva
ww naona unazidi. Hebu pima pimamaji yako ya uvichaa ulionena waliopo cdm; kisha linganisha na wengine..
  1. pia umevaa wapi udaktari wa kupima ukichaa huo hadi tukuamini usemayo. Je wadai kuwa wewe leo ukijipima na joppo lote ...top brass ya cdm, upo juu yao kiufahamu ??!.
  2. wengi huku hatufurahishwi na authoritative contributions of yours!
  3. kama umalenga mbunge adhimu wa A town; rumenoa thats true activist icone of Tz polical transformations.
  4. Let cdm do their own to clean their house. Do ur own as well.

kwa hayo machache ; wasalaam ndimi kukuru wa
Mkuu Kukara, kwanza asante kunisoma "in between the line!", kwa sababu humu jf, ni wachache wenye uwezo huo!.
  1. Hili la udaktari, just time will tell, nimesema top brass ina wenye akili na busara ila pia una vichaa!, kitendo cha hao wenye akili na busara kupokea ushauri wa vichaa wao na kuutekeleza bila kutumia akili zao na busara zao, huku nje tunawaona kama wote ni vichaa!, Namiini kwa ukichaa kwenye maamuzi ya ZZK now they have learnrd their lesson, na kama ilivyosemwa kutenda kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa!, wakirudia nitaamini kweli wote ni vichaa!.
  2. Pole!, Pasco wa jf ni mkweli daima na atasema ukweli daima bila kujali ukweli huo utamfurahisha nani na utamhurt nani!, kama wewe haufurahishwi, pole sana, ila huo ndio ukweli wenyewe, japo ukweli unauma!, ila ndio unasimama!.
  3. Pamoja na sifa zote hizo, lakini pia naamini unajua backround yake na modus operand yake!, tofauti ni haokoti makopo!.
  4. Mimi ni miongoni mwa tunaochangia fedha zetu kuiendesha Chadema, hivyo naitumia haki yangu ya msingi kusema chochote kuhusu lolote!, ila pia kuna sisi wengine, tunakerwa na kumuona mtu akijipakaza uchafu hata kama hakuhusu, wengine wataangalia pembeni kuavoid kinyaa, wengine watamuangalia kama kichekesho, na sisi wengine tunaoguswa, tutawish kumsaidia kwa kumwambia ukweli what s/he dores is not right!, asikie asisikie, it's up to h/im/er, alimradi aliambiwa!.
Thanks.

Pasco
 
Tarehe 19 Machi 2013 Niliandika Hivi hapa Jamvini.

Kwa kifupi ningependa nitoe wosia kwa vyama vya SIASA hasa vyama vya Upinzani na hasa CHADEMA.

Imetokea kasumba ambayo imekuwa inakuwa kwa kasi ya ajabu ndani ya vyama vya upinzani. Ndani ya vyama vya upinzani umetokea upepo wa kutokuaminiana, kumetokea wimbi kubwa la kutuhumiana USALITI miongoni mwa wanachama. Mtu akionekana kuwa amekuwa na mawazo tofauti na wenzake hata anapokuwa tofauti na kundi dogo tu ndani ya Chama au na kiongozi mmoja tu ataitwa msaliti na kundi la upande wa pili. Wakati mwingine hata utofauti wa Hoja humfanya mwanachama mmoja aitwe msaliti.

Mtiririko wa matukio ya kuitana wasaliti ndani ya CHADEMA nilianza kuyasikia uchaguzi wa BAVICHA, baadaye tukayasikia akituhumiwa mheshimiwa Shibuda, yakaenda kwa Mh. Zitto Kabwe, yakamaliza na kuwachinjia baharini akina Mtela Mwampamba na Juliana Shonza na kundi lake,

Historia inanikumbusha ni suala la tuhuma za Usaliti zilizoisambaratisha NCCR- Mageuzi, chama kilichokuwa maarufu miaka yetu ya 90. Kundi la Mrema liliwatuhumu kundi la Mabere Marando kuwa ni wasaliti na Kundi la Mabere Marando lilimtuhumu Augustino Mrema na kundi lake kuwa wanatumiwa na CCM na Serikali. Kutokana na tuhuma hizo, viongozi na wanachama wa kila kundi wakawa busy na kupanga mashambulizi dhidi ya kundi lingine kila kukicha. Hatima yake ni kurushiana viti na majaribio ya kutaka kuuana katika Hotel ya Mkonge huko Tanga na huo ukawa ndio mwanzo wa kifo cha NCCR-MAGEUZI.

Ninaona tatizo hili linainyemelea CHADEMA, tatizo hili linahitaji kutibiwa, CHADEMA inahitaji kujenga demokrasia ya kukosoana bila kuchukiana na kuhisiana vibaya. Wanachama wa CHADEMA wamekuwa waoga kutoa mawazo yatakayokinzana na wanachama wenzao na hasa viongozi fulani fulani kwa kuogopa kuitwa wasaliti.

Na kutokana na udhaifu huu ni rahisi sana adui kupenya. Kwa mfano katika mkanda wa video unaonyesha Lwakatare akipanga njama za kuteka, kushambulia na kudhuru mtu. Sababu inayotajwa kuandaliwa kwa mkakati huo ni Zitto Kabwe. Kuwa Mh. Lwakatare alikuwa anapanga njama za kigaidi dhidi ya mwandishi wa habari kwa kile kilichosemwa ukaribu wake na Zitto. Sasa unajiuliza shida iko wapi kuwa karibu na Zitto Kabwe, majibu katika video hiyo hiyo yanasema anadhofisha juhudi za chama, kwa kifupi ni msaliti.

Sijui kama video hiyo ya kweli au si ya kweli, na wala sihitaji kujua hilo, Lakini, Sababu ya hisia za USALITI ndio chanzo cha uwepo wa video hiyo. Sasa kama video hiyo ni ya kweli, basi utaona kuwa idara nzima ya ulinzi na usalama chini ya Lwakatare ilivyopoteza dira, Badala ya kushughulikia ulinzi na usalama wa chama kutoka kwa maadui wa kweli imejikita kwenye hofu hofu ya kusalitiwa. Kama hiyo video sio ya kweli utaona kuwa maadui wametumia kuwepo kwa hali ya kutokuaminiana ndani ya CHADEMA na hivyo imewezekana kutengeneza video hiyo kwasababu ya mwanya uliotengenezwa na CHADEMA yenyewe, mwanya wa hisia za usaliti.

Sasa hivi ndani ya CHADEMA ili uonekane wewe ni mwanaharakati wa kisiasa wa kweli, na mpenzi wa CHADEMA wa kweli ni lazima uongelee watu wanaohujumu jitihada za chama, lazima uzungumzie watu unaodhani hawako upande wenu. Sasa wanachama wa CHADEMA hawazungumzii tena Itikadi ya chama, Hawazungumzi tena hoja za mipango mikakati ya chama inayohusiana na maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, watu wako busy na nani anatuangusha wapi na kwa vipi na wasababu zipi.

Sasa badala ya kuwa kwenye mapambano dhidi ya mpinzani wa CHADEMA anayefahamika CCM mapambano yamebadirishwa na kuwa ni mapambano kati ya kundi moja la CHADEMA dhidi ya kundi lingine la CHADEMA, hii ni HATARI sio tu kwa CHADEMA yenyewe bali hata kwa ustawi wa Demokrasia ya nchi yetu na Afrika kwa ujumla.

Niwasihi viongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA warudishe ajenda muhimu kwenye meza za mazungumzo za wanachama wao, kufanya juhudi za makusudi za kuondoa hisia za hujuma na usaliti na kuwafanya wanachama wajione wao ni kitu kimoja, wenye nia na lengo moja wanaoenda njia moja.
Kaka.. sina cha kuchangia wala cha kuongeza zaidi ya kukwambia AHSANTE NA UBARIKIWE SANA.
kama kuna yeyote aliye na akili miongoni mwa wana chadema(nina wasiwasi kuwa wenye akili wote wanaonekana wasaliti), basi hawana budi kuliona hili ulilolisema. Mfano wa LWAX unatosha kuwaamsha usingizini
 
Pasco,

You must be cheating. Hakuna ukweli wowote unaotuambia hapa.Kwa mtazamo wako huu you sound like one of those lunatics like Shibuda, Zitto, Nape, Kinana and any other hooligans in CCM. Pasco tuna kujua wewe ni pro-CCM na huu ni ukweli ulio dhahiri. Na hapa unaonekana kabisa unawatukana baadhi ya Viongozi wa CHADEMA wakiwemo Viongozi wa Kitaifa pamoja na Wabunge wao. Yaani wewe kuona Godbless Lema anapendekeza Shibuda atimuliwe unamwona Mhe.Lema kuwa ni kichaa!!!

Huwezi kukaa na MBWA MWENYE KICHAA nyumbani kwako simply because ukimwaachia ataenda kung'ata watu. That won't be a solution at all. Dawa ya MBWA MWENYE KICHAA NI KUPIGWA RISASI ili asije akang'ata watu na kuwaambukiza KICHAA CHA MBWA (Rabbies)watu wengine.Ongeaa na Daktari yeyote wa mifugo atakuambia hiyo ndiyo dawa.

JOHN MADALE SHIBUDA tayari ni MBWA MWENYE KICHAA. Lazima apigwe risasi kwa maana ya kufukuzwa ndani ya chama. Shibuda must go at any cost! Atakachofanya baada ya hapo ni kuendelea kubweka na ukichaa wake lakini mwisho wa siku hiyo rabbies(KICHAA CHA MBWA) kinaenda kummaliza yaani lazma atakufa tu. Hataweza kuendelea ku-survive na ugonjwa huo!!!!

Ninachoweza kukisoma between the lines kwa mtazamo wa Pasco ni kwamba we know kuna mapandikizi ya CCM ndani ya CHADEMA yaliyotumwa kukidhoofisha chama kwa kufanya mambo ambayo ni kinyume na misimamo na sera za chama kama ambavyo kina Shibuda, Zito Kabwe, Mkumbo na wengineo. Mfano mdogo tu wa Shibuda wa hivi karibuni ni kuendelea kushiriki kwenye BMK ilhali akijua kabisa kuwa UKAWA unaojumuisha vyama pinzani ikiwemo CHADEMA waliamua kususia BMK kwa sababu zilizo wazi kabisa na zinaungwa mkono na Watz walio wengi lakini Shibuda aliasi uongozi wa CHADEMA na kuendelea kushiriki vikao mwanzo mpaka mwisho wa BMK!

Huyu mtu ni msaliti, kibaraka, mnafiki na ndumilakuwili na hatari. Hafai kuwa ndani ya chama chochote hata huko CCM walishamchoka. John Madale Shibuda is a lunatic,mental disabled and he must be surely kicked off!
CHADEMA fanyeni hima kumwondoa nduli huyu maana anaelekea kukiangamiza chama kabisa kwani tayari amesha kijeruhi kwa sehemu kubwa sana mpaka sasa.
 
Shibuda is theoretically CHADEMA M.p........
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom