Shibuda kuondolewa CHADEMA leo

Shibuda kuondolewa CHADEMA leo

Status
Not open for further replies.
CHADEMA wanakwepa kiini cha tatizo. Tatizo sio SHIBUDA. wameingia ndani ya bunge la katiba bila ya ajenda na walivyotoka nje wameshindwa kushawishi watanzania kujitoa muhanga. Shibuda alikuwa na ajenda ya wakulima na wafugaji. Kura ya maoni itathibitisha alikuwa sahihi pale theluthi mbili ya Tanzania bara itakapo piga kura ya ndio.

Shibuda kipau mbele chake ni masilahi ya wakulima na wafugaji sio kufurahisha CUF kwa kudai serikali tatu.

Sio polisi waliofanya maandamano na migomo ishindwe, bali ni uongozi wa chadema kukosa ushawishi. Unajuwa kabisa kilichofanya maandamano yashindwe kufanikiwa ni viongozi wa chadema kushindwa kushawishi watanzania wasiogope polisi. Viongozi wa chadema wanatakiwa waje na ajenda itakayo gusa hisia na mioyo ya watanzania kiasi cha kuwapa ujasiri wa kupambana na polisi.

Kilichotokea mashariki ya kati (uarabuni) ni watu kuguswa na ushawishi wa wanaharakati; yule mtu aliyejichoma moto mbele ya kituo cha polisi aliwasha moto ambao tayari ulikuwa unangojea kuwaka.

Huwezi kutegemea ajenda ya serikali tatu kumgusa mtanzania wa kawaida ambaye anataabika kupata ugali wake wa kila siku. Mtanzania wa kawaida haelewi serikali tatu itamsaidia vipi au itarahisisha vipi kupata ugali wake wa kila siku. Huwezi kutegemea ajenda ya serikali tatu kumpa ujasiri mtanzania wa kawaida kwenda kupambana na polisi. Na mbaya zaidi pale anapoambiwa kiongozi mwenye ajenda ya serikali tatu kaenda vakesheni nje nchi.

Kama kweli unataka kutoa ushauri wa kusaidia chadema, uongozi unapokosea lazima uwe na ujasiri wa kuwaambia ukweli.

Zaidi ya asilimia 70% ya watanzania ni wakulima na wafugaji, kwahiyo Mh. Shibuda alivyokuwa anawaambia ajenda iwe haki za wakulima na wafugaji alikuwa anatumia uzoefu wake kuwaambia ajenda itakayogusa mioyo ya watanzania ni ile ya wakulima na wafugaji.

Mbowe upeo wake mdogo umeshindwa kuelewa kwamba Tundu Lissu anasifa mbili tu, sifa nyingine muhimu hana, na kumfanya kuwa mshauri mkuu ni makosa. Sifa za Tundu Lissu ni usomi wa sheria na uaminifu. Hana uzoefu wa siasa wala uwezo wa kufanya maamuzi sahihi (He lacks experience and sound judgment).

Unaweza kuona hata humo ndani ya bunge la katiba vipau mbele vya Tundu Lissu au Ukawa vilivyokuwa vinabadilika. Ni kama mtu anayepapasa kwenye giza ambaye hajuwi ashike wapi. Alianza na hati ya muungano haipo, wanaushahidi kutoka umoja wa mataifa kuwa haijapelekwa, wakaamia tunatukanwa ndio maana tunatoka bungeni, baada ya hapo wakasema rasimu inapendekeza serikali tatu lakini CCM wanataka serikali mbili.

Lakini pia ikumbukwe humo ndani ya Bunge ya katiba, kuna wajumbe walihoji utaratibu uliotumika kukusanya maoni ya wananchi kwamba hauwakilishi sura halisi ya matakwa ya wananchi; ukasanyaji maoni ulipuuza baadhi ya maeneo (yaani bad sampling). hivyo hata hayo maoni yaliyoletwa na Warioba yanakosa uhalali kwasababu utaratibu wa ukusanyaji haukuwa sahihi.

Chadema kukosa dira au ajenda inaonekana pia kwenye operesheni zao; ukiangalia operation sangara, movement for change hakuna hata moja tuliyoona imefikia malengo fulani, zinayayuka hewani.

Hapa ndipo unapoona umuhimu wa uzoefu wa watu kama Shibuda. Kama ushauri wao ungekuwa unazingatiwa, sasa hivi CHADEMA ingekuwa inaonekana inapigania haki za wakulima na wafugaji sio serikali tatu ambazo hazi resonate to average Tanzanian. Mtanzania wa kawaida haelewi serikali tatu zitamsaidia vipi kuleta ugali nyumbani.

Msimamo wa kung'ang'ania serikali tatu ni ajenda ya kujenga mahusiano mazuri na CUF lakini sio ajenda ya kumtatulia mtanzania wa kawaida (mkulima, mfugaji, mvuvi) shida zake. Sasa Chadema watuambie watu wa tanzania bara ni masilahi ya kundi gani hayajazingatia katika katiba iliyopendekezwa.
 
Katika dhana inayoendela ya kuwaondoa wasaliti ndani ya Chadema; kamati kuu ya chama hicho kitakaa leo jumanne kujadili mambo mengi likiwamo la chaguzi za serikali za mitaa na nyendo za badhi ya watu ndani ya chama hicho!!!!!
Akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika siku ya juma mosi tarehe 11 katika kata ya moshono korna ya kiserian;

Mbunge wa Arusha mjini Mh Godbless Lema alisema hawataweza kuvumilia kuwaona wasaliti wakiendelea kudumu ndani ya chama hicho!!!Alisema hawatasita kuchukua hatua kwa yeyote anakiuka taratibu za chama akiwatolea mifano ya mh Zitto;Mwigamba;Mkumbo & etl!!!!Aliongeza kuwa wanda kukaa n kutoa maamuzi juu ya Shibuda!!!!! "Jumanne tarehe 14 tuakaa tutaamua hatima ya Shibuda;lazima aondoke"!Alisema

Maoni yangu: Chadema isimwonee haya vibara na vipandikizi vilivyoko ndani ya chima hicho.

Pamoja na Shibuda kwenda kinyume na matakwa ya uongozi wa chama bado CDM hawawezi thibisha kosa lake kwa mujibu wa katiba yao. Aliyeteua wabunge wa Bunge Maalum la Katiba ni Raisi kwa mujibu wa sheria husika
 
Hapa nani kamuacha mwenzie CHADEMA au SHIBUDA? Huyo SHIBUDA kisha sema uchaguzi unaokuja agombei kupitia CHADEMA.
 
Mkigusa mziki wa shibuda mtajuta nawambia!
 
Hapa nani kamuacha mwenzie CHADEMA au SHIBUDA? Huyo SHIBUDA kisha sema uchaguzi unaokuja agombei kupitia CHADEMA.

Hahahahahaaaah watu mnajua kufukunyua mambo humu.... eti shibuda ndo kaiacha chadema, kwahiyo chadema wanatafuta flagi za bure!!! Lakini mi nilikua nawauliza kuhusu zitto, wanamfukuza lini?
 
Wanaenda kujadili nini juu ya Shibuda kama tayari amesha sema wanamuondoa?

Kina anaehamia cdm ni pandikizi?
Kama ndio hivyo mwana cdm halisi ni nani?
Au kauli hizi zinatumika makusudi ili kuendelea kushikilia chama?

Any way, long live cdm, tupate maendeleo ya kweli.

Kama na wewe ni msaliti jiandae kuondoka. Mamluki hawatakiwi CHADEMA.
 
Hahahaaa Pasco uchambuzi wako ni noma eti shibuda ni empty kabisa ni sawa na mbwa kichaaa!
 
Last edited by a moderator:
Sio kwa shibuda, mtemi wa wawasukuma

Chadema wana uthubutu wa kuchukua maamuzi magumu tatizo maamuzi yanachelewa sana. Linapojitokeza tatizo unatakiwa kulikabili mapema vinginevyo linaweza likaleta madhara badala ya kuwa tiba. Strike the iron when it is still hot. Katika siasa unapochukua maamuzi magumu ya kumtimua kiongozi karibu na uchaguzi ni kuwa utapoteza muda mwingi kushughulikia yatokanayo badala ya kuhangaikia kampeni. Wote hao wanaoitwa wasaliti walifahamika muda mrefu na ushahidi ulishapatikana muda mrefu hivyo hatua zingechukuliwa mapema bila kuwapa muda wa kuendelea kukiharibu chama.
 
Wamemchelesha sana huyu jamaa, tunataka chama ifikapo uchaguzi mwakani asiwe amesahaulika au kuachwa msaliti yeyote ndani.
Sio wamemchelewesha bali hiyo saccos ya tengeru mmewakabidhi masela ndio waiongoze tegemeeni kifo cha mende. A good example mtaona uchaguzi wa serikali za mitaa mtakavyoumbuka. Zama za chadema zimepita zama zijazo ni za kuporomoka chadema.
Amini usiamini hivyo ndivyo itatokea
 
Wananchi gani wamchague tena? Hata uchaguzi uliopita ni cdm kilichoshinda hakuwa yeye. Kama zinamtosha kichwani analijua hilo.
 
Wangevuta muda wakamuondoa last minute ya uchaguzi 2015 ; sasa hivi ataamia chama kingine na atashinda 2015 maana wananchi watamchangua.....

Acha Kumfariji huyo mamluki,hii ndio awamu yake ya mwisho na ubunge atausikia tu kwenye bomba
 
Sio wamemchelewesha bali hiyo saccos ya tengeru mmewakabidhi masela ndio waiongoze tegemeeni kifo cha mende. A good example mtaona uchaguzi wa serikali za mitaa mtakavyoumbuka. Zama za chadema zimepita zama zijazo ni za kuporomoka chadema.
Amini usiamini hivyo ndivyo itatokea

Unajifariji bure,tumejipanga kushinda uchaguzi huo na huku nilipo lazima tuibuke kidedea,ccm tulishaizika kitambo
 
Sio kwa shibuda, mtemi wa wawasukuma

Wasukuma wepi hao? Mbona mimi mwenyewe msukuma na simjui huyo shibuda zaidi ya kumsikia kwenye shughuri za magamba? Ntemi mbuli ohe nanhwe ungenuyo? Hamo ulu ntemi o mitunga ga lumumba!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom