=> Shibuda alikubali matokeo ya urais kabla ya CHADEMA kukubali alafu CHADEMA wakakubali.
=> Shibuda alikubali kumtambua rais kabla ya CHADEMA kumtambua rais alafu CHADEMA wakamtambua urais.
=> Shibuda alisema posho ni muhimu wakati CHADEMA wanasema zifutwe; alafu CHADEMA wakaona posho ni muhimu wakaendelea kuchukua posho mpaka leo.
=> Shibuda anaunga mkono serikali mbili CHADEMA wanaunga mkono serikali tatu.
=> Shibuda kaingia bunge la katiba na ajenda ya wakulima na wafugaji, CHADEMA wameingia na ajenda ya hati ya muungano haipo, alafu ajenda ikabadilika ikawa tunatukanwa, alafu ikawa serikali tatu.
=> Sasa hivi CHADEMA haipingi serikali mbili, inapinga jinsi kura zilivyohesabiwa ndani ya bunge la katiba.
=> Sasa hivi CHADEMA hawapingi jinsi kura zilivyohesabiwa ndani ya bunge la katiba, inapinga kura ya maoni kufanyika kabla ya daftari la wapiga kura kuboreshwa.
Kwasababu nilizozitaja hapo juu shibuda kafukuzwa mara moja.