Shibuda: CCM ni chama cha maskini na wanyonge

Shibuda: CCM ni chama cha maskini na wanyonge

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,815
Akichangia ktk hotuba ya wizara ya ardhi, mh John Shibuda, mbunge wa maswa kupitia CHADEMA amekisifia CCM kuwa ni chama cha maskini na wanyonge na ambacho kimelinda maslahi ya watanzania tangu uhuru.

Shibuda amemtaka waziri wa ardhi ahakikishe anatekeleza sera ya CCM ya kueatetea wanyonge kwa kuwaondoa wafanyabiashara wote wanaoishi kwenye nyumba za serikali maarufu kama quoters!!!!

Amewaita wafanyabiashara hao wanaoishi kwenye nyumba za serikali/Quoters kuwa ni wahujumu, wanyonyaji na hivyo waziri ahakikishe wanaachia nyumba hizo ili zitumiwe na watumishi wa umma ambao ni maskini.

Aidha ameitaka serikali iwauzie nyumba wafanyakazi waliokaa mda mrefu kuanzia miaka 20 kwani hawajajenga kwa kupenda bali ni kipato duni.
 
Ni kweli kabisa, serikali ya ccm ni serikali SIKIVU!...jamaa hajakosea!
 
Huyo ni tope, hakuna cha kamanda wala mpiganaji hapo....ni maaigizo ya magamba ndani ya chadema...CHADEMA WAACHANE NA HUYU MTU, KAZI ANAYOIFANYA CHADEMA HAMTAPONA!...
 
Huyo ni tope, hakuna cha kamanda wala mpiganaji hapo....ni maaigizo ya magamba ndani ya chadema...CHADEMA WAACHANE NA HUYU MTU, KAZI ANAYOIFANYA CHADEMA HAMTAPONA!...

Mkuu, wala usiogope; Shibuda kwa mikono yake miwili alichukua kamba na kujininginiza mwenyewe, kwa sasa ana rusharusha miguu tu; CHADEMA hatuna haja ya kupoteza mda wetu kuhangaika na mtu kama Shibuda; Tumewaachia wapiga kura wake wamsurubu wenyewe ifikapo 2015.
 
shibuda ameonyesha kuwa kweli amekomaa kisiasa.....huyu jamaa wa dunia ya kwanza
 
watu kama hawa wasipokuwepo kwenye jamii maisha yatakuwa boring. kaza buti mkuu urais 2015 hutaki?
 
Hakuna asiye jua hili vinginevyo abishe kwa maksudi tu lakini ukweli anaujua daima.
 
CCM mbona ni chama cha wakulima na wafanyakazi hao aliowataja ni segment kwenye izo category mbili.
Ingawa kwa sasa CCM uhalisia wake ni kuwa ni chama cha WAFANYABISHARA,WAKULIMA NA WAFANYAKAZI ndani yake segment kama ya UFISADI iko!
 
Huyu Shibuda huwa simuelewi!
Ni vigumu kumwelewa lakini yeye anajua anachokiamini ila ukimsikiliza kwa makini utapata kitu ila anatumia mafumbo mengi sana na fasihi pana sana.
 
Shibuda ngurubange kweli popo si popo mnyama si mnyama........
 
Tuache ulimbukeni wa kisiasa na fikra mgando! Kwani ni chama gani kimesajiliwa hapa nchini kwa ajili ya kundi fulani tu la watanzania? Tuache siasa zisizokuwepo watanzania sasa mnatakiwa kufungaka akili zenu! Huyo shibuda atuambie ni chama gani kilichosajiliwa hapa tanzania si kwa ajili ya hao anaowasema (wanyonge, wakulima)?
 
Ni kati ya watu ambao hawawezi kufukuzwa......."ruzuku" kwa kiswahili chepesi inaitwaje?
 
Back
Top Bottom