Shibuda: CCM ni chama cha maskini na wanyonge

Shibuda: CCM ni chama cha maskini na wanyonge

Msimbeze shibuda kwa maneno yake hayo...anajua alichokisema ni hakiwezekani kwa ccm ya sasa inayonuka rushwa na ufisadi.....!kwa maana nyingine ni kama kawatukana ccm
 
Akichangia ktk hotuba ya wizara ya ardhi, mh john shibuda, mbunge wa maswa kupitia chadema amekisifia ccm kuwa ni chama cha maskini na wanyonge na ambacho kimelinda maslahi ya watanzania tangu uhuru. Shibuda amemtaka waziri wa ardhi ahakikishe anatekeleza sera ya ccm ya kueatetea wanyonge kwa kuwaondoa wafanyabiashara wote wanaoishi kwenye nyumba za serikali maarufu kama quoters!!!! Amewaita wafanyabiashara hao wanaoishi kwenye nyumba za serikali/Quoters kuwa ni wahujumu, wanyonyaji na hivyo waziri ahakikishe wanaachia nyumba hizo ili zitumiwe na watumishi wa umma ambao ni maskini. Aidha ameitaka serikali iwauzie nyumba wafanyakazi waliokaa mda mrefu kuanzia miaka 20 kwani hawajajenga kwa kupenda bali ni kipato duni.

SHIBUDA anaweza kuwa mkweli kwa vile amevitumikia vyama vyote viwili, CHADEMA na CCM na inawezekana kabisa amepima chama kipi kinawatumikia watanzania kwa dhadi na kipi kimejaa usaniii
 
Msimbeze shibuda kwa maneno yake hayo...anajua alichokisema ni hakiwezekani kwa ccm ya sasa inayonuka rushwa na ufisadi.....!kwa maana nyingine ni kama kawatukana ccm

Siyo kwamba amejifunza kuwa kule aliko ni usanii mtupu na anajutia kwa nini amehama CCM?
 
Akichangia ktk hotuba ya wizara ya ardhi, mh john shibuda, mbunge wa maswa kupitia chadema amekisifia ccm kuwa ni chama cha maskini na wanyonge na ambacho kimelinda maslahi ya watanzania tangu uhuru. Shibuda amemtaka waziri wa ardhi ahakikishe anatekeleza sera ya ccm ya kueatetea wanyonge kwa kuwaondoa wafanyabiashara wote wanaoishi kwenye nyumba za serikali maarufu kama quoters!!!! Amewaita wafanyabiashara hao wanaoishi kwenye nyumba za serikali/Quoters kuwa ni wahujumu, wanyonyaji na hivyo waziri ahakikishe wanaachia nyumba hizo ili zitumiwe na watumishi wa umma ambao ni maskini. Aidha ameitaka serikali iwauzie nyumba wafanyakazi waliokaa mda mrefu kuanzia miaka 20 kwani hawajajenga kwa kupenda bali ni kipato duni.

Yaani nikimsikiaga huyu mtu roho inachafuka kabisa hata kula mashindwa
 
Tuache ulimbukeni wa kisiasa na fikra mgando! Kwani ni chama gani kimesajiliwa hapa nchini kwa ajili ya kundi fulani tu la watanzania? Tuache siasa zisizokuwepo watanzania sasa mnatakiwa kufungaka akili zenu! Huyo shibuda atuambie ni chama gani kilichosajiliwa hapa tanzania si kwa ajili ya hao anaowasema (wanyonge, wakulima)?
Mkuu, SHIBUDA kajifunza mengi kuwepo kwake CHADEMA, ukitaka kujua baadhi ya vyama Tanzania ni kampuni za watu wachache sikiliza maneno ya watu waliowahi kutumikia vyama vingine na kujiunga na hizo kampuni. SHIBUDA anashindwa tu kusema anajuta kuhama CCM.
 
tutaenda naye hivyohivyo tu kama gari bovu tukiona hawezi kutuathiri tutafika naye 2015 ila asahau ubunge kupitia CHADEMA labda safari hii aende NCCR au arudi kwaoCCM. CHADEMA sio size yake, tulifanya makosa kumkaribisha ila hatuna jinsi hebu twende naye hivyo hivyo kiubishi, ubishi. Tutafika!!
 
Ni kweli kabisa, serikali ya ccm ni serikali SIKIVU!...jamaa hajakosea!

Watu wasiyo wanafiki utawajua tu, SHIBUDA anakiri kile ambacho wana CHADEMA wenzake imekuwa ni tabu sana kukitamka japo ukweli, sijui ni uoga au nini, kila anayesubutu kukiri kuwa CCM haikamatiki atashushiwa zigo la lawama toka kwa viongozi wa juu ambao wanaona kwa kukiri kwao, ni kuhatarisha ulaji wao. Kwa mtindo huu hatuwezi kuijenga nchi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni haki mpeni, hongera SHIBUDA kwa kuonesha ujasiri, naita huu ni ujasiri kwa vile siyo jambo rahisi kutamka machoni mwa MBOWE kuwa CCM ni chama cha Wanyonge, anathani akufukuze kwenye chama bila hata kufuata taratibu.
 
Ni kweli kabisa, serikali ya ccm ni serikali SIKIVU!...jamaa hajakosea!

Serikali sikivu kwa lipi? Kwa masikio yapi? Masikio yaliyozibwa pamba na macho yenye miwani ya mbao? CCM tuijuayo na iliyokuwa sikivu ni ile ya kuanzia 1961 hadi 1985. Baada ya hapo ni serikali ya chama cha manyang'ao.
 
Shibuda bado anaishi kwenye UTOPIA!

Kama CCM ni chama cha Masikini na wanyonge, hao mafisadi na Matajiri waliingiaje kwenye government quaters? Au anataka kutuaminisha kwamba CDM ndiyo waliowaingiza?

I give Shibuda the benefit of doubt that was a TONGUE IN CHEEK to CCM!
 
SHIBUDA anaweza kuwa mkweli kwa vile amevitumikia vyama vyote viwili, CHADEMA na CCM na inawezekana kabisa amepima chama kipi kinawatumikia watanzania kwa dhadi na kipi kimejaa usaniii

In the same TOKEN kwa kuwa Dr. Slaa amevitumikia vyama vyote CCM na CDM hivyo anajua fika chama kipi cha MAFISADI NA USANII?!

THINK BIG DUDE
 
2015 tena aanze kuliaga bunge mapema tu, maana 2015 itakuwa ni ndoto...
 
Back
Top Bottom