Shibuda apania kugombea dhidi ya JK CCM, ajitoa ghafla

Kiongozi atakayenifaa na nitampa kura zangu zote 2010 ni huyu hapa
...."Kiongozi anayetufaa Tanzania , ni yule anayejua kuwa nchi yetu ni masikini na watu wake ni masikini. Na ukimwangalia usoni ...uone anaguswa na umasikini wetu. Vinginevyo hatufai...." J.K.Nyerere.
Ajue kuwa kuna watanzania zaidi ya million 30 hawana uhakika wa kupata mlo mmoja kwa siku.
Ni lazima asiwe na kigugumizi katika kutoa uamuzi wa haki kwa sababu si wakala wa mtu yeyote. Serikali yake lazima isimame upande wa wanyonge, ikisimama upande mwingine wanyonge hao hawana pa kukimbilia.
Kasi ya serikali yake iweze kushughulikia kero za wanachi ikiwemo rushwa kwa umakini pasipo kushinikizwa na mtu yeyote
 
Kuna wakati mtu akiwa anaongoza msafara inabidi utumie kichwa na kujiuliza mara mbili mbili.Niliwahi kuwa na shaka na Mrema, lakini, kama mambo mengine yalivyo, sasa hivi amejidhihirisha yeye ni nani. Sio kiongozi wa upinzani huyu. Ana lake jambo kichwani
 
Nadhani Hayati Mwl. Nyerere alisema hivyo akijua kuwa baadhi ya wagombea wa kiti hicho walikuwa na sifa ambazo zilikuwa kinyume na misingi hiyo.

Si tunayaona sasa?
 
NI CHEO AU TAASISI ?

Kwanza kabisa kama tunazungumzia uchaguzi mkuu 2010 ni lazima tuangalie uongozi husika kwamba je tunamchagua Rais au je ni mbunge???......

Rais

Hiki cheo ni ' very sensitive' na kinavuka mipaka ya cheo hadi kuwa Taasisi. Kwa hiyo u-rais ni Taasisi, na hivyo hatuangalii mtu mmoja peke yake... mfano sura nzuri aliyonayo...kisha tukachapisha picha za gharama ili watu wavutiwe na picha wachague...no no no...Kwanza Historia iliyothibitika ya huyo mtu inafanana vipi na uendeshaji wa nchi yetu katika kutatua matatizo tuliyonayo, kutumia nafasi tulizonazo, kupambana na mapungufu yaliyoko, na kukuza marejesho ya uimara tulionao.

Pili watu wanaombatana na huyu nao wachambuliwe kama mtu mwenyewe mhusika agombeaye kwa mfano anayetarajiwa kuwa 'first lady' au 'first gentle man' kichwa chake kimekaaje? maana FL/FM ni mtu wa muhimu sana katika nchi na inabidi wapiga kura waelimishwe juu ya hilo. Nchi inaweza ikafaidika sana au ikapata hasara kubwa kutegemeana tu na aina ya mke wa Rais ama mume wa Rais tuliyenaye. Halafu mgombea mwenza naye pamoja na mkewe au mumewe ni wa kuangaliwa pia maana ndiye Makamu wa Rais huyo.

Katika hilo ni vizuri pia kutazama 'kampani' ya mgombea je ni watu wa namna gani. Marafiki, washauri, familia, wapiga kampeni, chama chake, n.k maana haiwezekani kampani ikawa ni wavuta unga halafu yeye mwenyewe asiathirike kwa kiasi fulani na hilo, au pengine ni mafisadi, au wabaguzi, au wadini, au hawana uzalendo na nchi yetu na mengineyo mengi. Mtu mmoja amewahi kusema ' Rais hana marafiki wapya'. Hakuna Rais ambaye hukataliwa urafiki kwa hiyo atakaowaamini ni wale wa sikuzote ambao wamekuwa naye wakati wa hali ya kawaida, kabla hata ndoto ya urais wake haijaotwa na hao marafiki.....sasa je ni wazuri hawa?????

Jambo la tatu Rais mtarajiwa anaijua vipi nchi yetu kwa mapana na marefu na kina....na anaijua vipi dunia nje ya nchi yetu. Je ujuzi wake wa nadharia na uzoefu kivitendo unamwezesha vipi kuwa chaguo sahihi la kutumia maliasili tulizonazo, umoja wetu, kiswahili chetu, jamii zetu za kipekee kama wamasai na watindiga, visiwa vyetu, ardhi yetu, udongo wetu wa kipekee wenye rutuba ya asili, upole wetu watanzania, kupakana kwetu na nchi kama saba hivi na mengineyo ...kuyatumia kwa maslahi ya TAIFA LETU...kwa usawa bila kumbagua mtanzania yeyote...aidha kidini, ukabila...nk. Na tena anawezaje kuyaunganisha haya na dunia ya sasa tuliyonayo ya G20, G8, Rais mweusi marekani, Euro, European Union, Msisitizo wa masuala ya mazingira, usawa wa kijinsia, mapambano dhidi ya UKIMWI, UGAIDI, UKOLONI MAMBOLEO, MGOGORO WA KIUCHUMI, au mambo kama kuibuka kwa CHINA na INDIA, ugunduzi wa mafuta Uganda, Kukua kwa mikakati ya biashara bandari ya MOMBASA, utata wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mashirikiano ya kimataifa ya kijeshi na kijasusi, matumizi ya hali ya juu ya satelite ikiwemo kwenye ujasusi, dunia ya Credit Cards, Kukua kwa utalii wa wanyama wa ZOO badala ya National Parks, Migogoro ya Nyuklia, Mataifa mbalimbali kupigania mali ndani ya DRC Congo, Mgogoro wa Darfur, Somalia na mambo kama utekaji nyara Meli, Iraq, Afghanistan, Masuala ya Indonesia na Malaysia, Mambo ya utupaji taka za Sumu kwenye Nchi maskini, Uporaji wa Maliasili, na Mengineyo. Mambo yote hayo yanaweza yakatumika kwa faida ya nchi hii.

Nne Rais mtarajiwa kinachomsukuma hasa kugombea ni nini? Kama ni Kikwete kwa mfano je kinachomsukuma ni kuogopa kuwa wa kwanza kushika kipindi kimoja tu. Au kuna jambo la maana hakuweza kulifanya miaka ya kwanza mitano ambalo kuna uthibitisho kuwa ataweza kulifanya akiongezewa miaka mingine mitano au je kuna JIPYA???. Na jambo lenyewe au mambo hayo ni yepi??? Au kama ni mwingine je ana kusudi sahihi la kutaka kuingia ikulu....maana mambo yafuatayo ni miongoni mwa NIA HARAMU ZA KUGOMBEA URAIS.

1. Kutafuta urais ili kuweza kulipa fadhila au kulipa kisasi.

2. Kugombea urais kwa kuwa kundi fulani linakutaka uwe Rais lakini wewe mwenyewe huna nia thabiti ya kubeba majukumu mazito yahusikayo na Urais.

3. kugombea ili upatapo urais uisaidie dini yako ifanikishe masuala yake ya kidini.

4. Urais kwa ajili ya kuboresha maslahi binafsi.

5. Urais ili kuweka historia kuwa kabila lako au ukoo wako au dini yako wamekamata Ikulu mara kadhaa.

MTU YEYOTE AKIJIUZA AU KUJINADI KWA KUTUMIA HAYO HAPO JUU AU YEYOTE YAFANANAYO NA HAYO,.. NDUGU WAPIGA KURA WENZANGU...HATUFAI. Wako watu ukiwauliza kwa nini wanagombea wanasema "nimeombwa na wananchi". Mtu kama huyu HAFAI. HAJUI ANACHOFUATA IKULU.

Ni vizuri Rais aweze kujua namna ya kutengeneza mapato bila kutegemea misaada ya nje. Lakini anuie kabisa kabisa kutumia mapato ya nchi kwa HEKIMA. RAIS MFUJAJI HATUFAI. RAIS ASIYEKUSANYA KODI HATUFAI. RAIS FISADI AU MWENYE MARAFIKI MAFISADI HATUFAI. RAIS ASIYE NA MSIMAMO HATUFAI.

Mbunge

Huyu ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo lake. Unaweza kukuta Mfanyabiashara akaamua kugombea ubunge kwa ajili ya POWER na si maslahi ya wananchi. HUYU HAFAI KUWA MBUNGE.

Unaweza kukuta mlalahoi akaamua kugombea ubunge kwa ajili ya kwenda kupata ULAJI BUNGENI, huyu naye HAFAI. Ama mwingine kastaafu sasa anatafuta kwenda bungeni kama KIJIWE cha kupumzikia na kupiga soga na usingizi wa reja reja....HATUFAI KABISAAAAA.

Wanaokerwa kweli kweli na matatizo ya wananchi na wana uwezo wa kuyatetea BUNGENI na kwingineko wanafahamika. Wachaguliwe wao bila kuangalia vyama wanavyotoka. 2010 tuchague uwezo wa mtu na siyo chama chake, dini yake, pilau zake n.k

MUUZA SURA YEYOTE ATOSWE. NA HATUTAKI WANAOKREMU KUWA MATATIZO TULIYONAYO NI EPA NA RICHMOND PEKE YAKE. TUWAHOJI KIUNDANI NA WACHUNGUZWE KWA KINA KAMA WANATUFAA AU LA.

NI DHAMBI KUCHAGUA MTU AU MTU KUCHAGULIWA KISHA AKAWA KUMBE NI KIONGOZI ASIYEFAA. NI UBAKAJI WA HAKI NA DEMOKRASIA YA KWELI YA WANANCHI WA TANZANIA..... NI HERI MNYONGWE HADI KUFA.... BORA MSIGOMBEE KABISA!!!!!!!!!!
 
Pamoja na hayo yote anatakiwa awe na silaha zitakazomsaidia kupambana na kujikinga na hatari zozote na mashambulizi kutoka kwa maadui wake. Silaha hizi sio silaha tulizozoea kuziona kwa macho yetu kama bunduki, mapanga na visu la hasha hizi ni silaha muhimu sana katika maisha ya mtu yeyote anayetegemea kuwa kiongozi katika nchi yetu hii ya Tanzania.
Silaha hizo ni matendo, tabia na mienendo mizuri ya kiongozi. Hizi ni silaha kubwa na nzito zaidi kuliko bunduki, bastola, rungu, mishale, mikuki, mabomu na kadhalika.
Pia kiongozi atakayenifaa mwaka 2010 asiwe ni mtu wa kulipa kisasi. Baadhi ya viongozi wanapenda kulipa kisasi, jambo hili lina kwamisha maendeleo: "Kisasi ni nia au kusudio la kulipiza ubaya aliofanyiwa mtu. Hapaswi kulipa kisasi. Akifanya hivyo yeye si kiongozi. Kuudhiwa, kukosewa, kudharauliwa, kutukanwa, kusingiziwa au kuandikwa vibaya magazetini ni mambo ya kawaida kwa kiongozi".
Zaidi ya yote ni lazima awe Mbunifu, Mwanamikakati, Manaharakati na mwenye mawazo mapya. Kiongozi lazima uwe mbunifu mwenye mikakati, mwanaharakati na mwenye mawazo mapya. Haiwezekani yeye (KIongozi) akawa ni wa kutekeleza mikakati, mbinu na mawazo ya wengine. Ya kwake yako wapi? Je, atakumbukwa kwa lipi? Atasifiwa kwa lipi? Atalaumiwa kwa lipi?

Mjadala uendelee
 
Kiongozi atakayenifaa na nitampa kura zangu zote 2010 ni huyu hapa
...."Kiongozi anayetufaa Tanzania , ni yule anayejua kuwa nchi yetu ni masikini na watu wake ni masikini. Na ukimwangalia usoni ...uone anaguswa na umasikini wetu. Vinginevyo hatufai...." J.K.Nyerere.
Ajue kuwa kuna watanzania zaidi ya million 30 hawana uhakika wa kupata mlo mmoja kwa siku.
Ni lazima asiwe na kigugumizi katika kutoa uamuzi wa haki kwa sababu si wakala wa mtu yeyote. Serikali yake lazima isimame upande wa wanyonge, ikisimama upande mwingine wanyonge hao hawana pa kukimbilia.
Kasi ya serikali yake iweze kushughulikia kero za wanachi ikiwemo rushwa kwa umakini pasipo kushinikizwa na mtu yeyote

Ndugu yangu,Tanzania sio nchi maskini.Hebu kaa chini utafakari kwa kina kuhusu hili.
 
Ndugu wanaJF nimeona nianzishe thread hii ili tupeane mawazo kuhusu mgombea urais kupitia CHADEMA, mimi ni mpenzi wa mageuzi si ya kisiasa tu bali pia ya ki-fikra ki-uchumi na ki-maendeleo kwa ujumla. Nimejaribu kuangalia ndani ya CHADEMA nimeona katika uchaguzi ujao kama M/kiti wa Chadema Mh. Mbowe hatagombea basi Prof. Baregu atafaa zaidi kama akishika bendera ya ugombea urais 2010.

Ni maoni yangu tu wanaJF naomba mawazo yenu kupitia ujumbe wa posts zenu humu JF kama atakuwa na sifa tunazozitaka ikiwezekana tumuombe Ndugu John Mnyika kwa vile yupo humu ayawasilishe rasmi kwa Prof. Baregu ili pindi fomu zitakapotoka tumsindikize akachukue.

Asanteni...Charity Starts At Home of Great Thinkers

Kama wao walishinda kwa nini sisi tushindwe?

BAREGU FOR PRESIDENT 2010.......Hakuna kulala
Baregu%282%29.jpg
 
Ni wazo zuri kwanza tupate CV yake na ameingia lini upinzani isije kuwa walewale tu kwa mwenye CV yake ailete humu jamvini tuichambue.
 
Asante mkuu ila kwa sababu umeanza kusema -Charity Starts At Home of Great Thinkers

1.Nchi hii siyo ya CCM wala haitakuwa ya Chadema, nadhani ni muda mzuri wa kupigania mabadiliko ya katiba, serikali iwe ya umoja, itokane na asilimia za kura walizopata kwenye chaguzi, kila chama kiwe na mkono serikalini, hivyo ni jukumu la vyama vya upinzani kuwaza hili kwanza na ilikuwa first assignment since 1992

2. Tukimaliza hapo tubadili katiba ya kumpunguzia madaraka rais (kuteua jaji mkuu, mkuu wa polisi, wakuu wa majeshi, director wa PCCB, n.k)

3. Tukimaliza hiyo kazi kubwa tuanze na tume ya uchaguzi ambayo ni ya CCM, ikwe ya kitaifa

Baada ya hapo ndio tuwaze uchaguzi wa rais tukiwa tumeshajenga taifa la wote kwa ajili ya wote.

Then tuanze kuwaza uchaguzi wa rais na Chadema wamsimamishe mgombea wao , ambao wa sasa unamtaka Baregu.

kwa sasa naamini vyama vya upinzani ukwemo wewe hamna anayewazia hayo mambo matatu hapo juu, yanasemwa yananyamaziwa na watu wanaenda kwenye chaguzi, kana kwamba kuna siku vyama vya upinzani vitapata rais! kuoitia tume hii na system hii!



Ok, lets assume kila kitu kiko sawa Tanzania ndio nakuuliza sasa;

1. Je kwa nini Baregu?

2. Una matarijio gani ya chadema kushinda urais,( I mean strategy)

Ishu ya sasa ya Baregu , iwe handled kwa haki na yeye atafanyika daraja la wengi kupata haki, si kila anayenyimwa haki kama baregu akimbilie urais, kuna wengi wa design ya Baregu watakuja nchi hii na solution ni tupigane haki ipatikane.

However, kama chama watamtaka nani wa kuzuia??
 
Asante mkuu ila kwa sababu umeanza kusema -Charity Starts At Home of Great Thinkers

Ok, lets assume kila kitu kiko sawa Tanzania ndio nakuuliza sasa;

1. Je kwa nini Baregu?

2. Una matarijio gani ya chadema kushinda urais,( I mean strategy)

Waberoya
Ni sawa kabisa unavyosema kwanza tupiganie katiba halafu ndipo tuwaze uchaguzi, ni kitu kinachowezekana lakini si kwamba hilo litatokea leo au kesho it takes time na elewa kwamba kubadili katiba ni mapambano kati ya watawala na watawaliwa, watawala au walio madarakani wataona ni njia ya kunyang'anywa walicho nacho kwa hiyo watafanya kila mbinu ili kuchelewesha mabadiliko na ujue wakati wanachelewesha si kwamba chaguzi zitasimama wao watakuwa wanaweka mgombea wao hata kama vyama vingine vitasusa kwa kila chaguzi. Kwa hiyo wakati vyama vya upinzani vikiweka mikakati ya kubadili katiba ni bora vikajiandaa na chaguzi zilizopo.

Kuhusu Tume huru ya uchaguzi ni kweli si huru na tunajua itakuwa biased kwa vile inateuliwa na rais itapendelea aliye iteua lakini hiyo vile vile isivikatishe tamaa vyama vya upinzani kutojiandaa na uchaguzi.

Umesema kwa nini prof. Baregu hilo ni pendekezo langu tu Mkuu nimemuona Baregu anasifa zote za kuwa mgombea kama Mbowe ataamua kutogombea lakini haizuii kama kuna mtu unayemuona anafaa zaidi kumpendekeza hata hivyo nimesema prof Baregu akuchukue fomu aingie kwenye kura za maoni ndani ya chama chake hivyo anaweza kupambanishwa na wana Chadema wengine anaweza ateuliwe au asiteuliwe. Hilo la matarajio ya Chadema kushinda nitajibu baadaye.
 
Baregu siyo material ya uraisi. Aendelee kufanya wanayofanya maprofessa wenzake akina Wole Soyinka, Mazrui, Ngungi, ..
 
Baregu must first know how to live without a job, like most Tanzanians live!
Ile ruzuku amegewe na Chadema,sooner or later you will see sparks flying around!!
 
Kuna wengine, wenye ushawishi katika jamii, walishaapa. Nshomile never on earth! Sifagilii ukabila, ila duh!
 
Kuna wengine, wenye ushawishi katika jamii, walishaapa. Nshomile never on earth! Sifagilii ukabila, ila duh!

Kama Chadema wakiwa na system kama ilivyo ya CCM nitakubaliana nawe kwamba watajaa Nshomile serikalini lakini kama Chadema wakija na system yao tofauti sidhani kama itakuwa tatizo. Nafikiri prof. yuko fit angalia hata hili tukio anavyoli handle hababaiki na alikuwa anajua what will happen lakini alikuwa na msimamo tunataka watu wa aina hiyo.
 
Baregu siyo material ya uraisi. Aendelee kufanya wanayofanya maprofessa wenzake akina Wole Soyinka, Mazrui, Ngungi, ..


hata maprofessa wanaweza kufanya vizuri ktk Urais. Watizame wenzetu Ghana na rais wao Prof. John Atta Mills. Nchi yao inasonga mbele kama kawaida.

[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/John_Atta_Mills[/ame]



Baregu for President!!
 
Ninavyomjua Prof.Baregu,

1 He has strong character of leadership, good academician in politics and political science.
2 Known figure, respected person in and out of Tanzania anaipenda nchi yake ndio maana alisema badala ya kwenda kutafuta kazi nje atastaafu anafundisha Tanzania.
3 Open minded ana uwezo mkubwa tu wa ku-analyse mambo
4 he is trustworthy known to live with people hana majivuno hajikuzi na hana makuu, honestly and integrity si mtu wa kupenda kujilimbikizia mali.
5 prof. ni mtu wa vitendo walks the talks huwa anatenda anachokihubiri
6 he is confident in leadership role huwa anakiamini anachokisema au anachokifundisha
7 tolerant of ambiguity and remains calm and cool head tumeona kwenye sakata lake hili la kufukuzwa wala hababaiki ni kwamba anajua anachokifanya.

for that I know prof. Baregu I think he will make a good president
 
kutaka baregu agombee uraisi wakati mnajua kamisa uchaguzi una mizengwe kwenye nafasi hio ni kupoteza kichwa cha maana sana kwenye jamii yetu.mimi nataka prof baregu agombee ubunge kwanza hili akaongeze joto.

wapinzani wanatakiwa waungane kwenye nafasi ya uraisi na nafasi za ubunge wanatakiwa kila jimbo ambalo wanaona chama fulani kina wafuasi wengi basi kiungwe mkono.muhimu hapa ni bunge kwanza kulitawala baada hapo urais utapatikana tu.
 
1. Constitutional right
2. Academician cum politician who happens to know political, economic and social problems facing the country.. through various research, publications of his own. My support to Lipumba na Baregu is based on this facts. My dream is to go away with pure politician e.g. JK, Malecela, etc, within the presedential circle ..they normally prefer status quo!
3. Sijawahi kusikia kama ni materialistics yaani mtafutaji wa pesa nyingi..hivyo ni unlikely kuwa na kampuni ikulu..
4. International recognized figure, mpenda mageuzi alianzia enzi za NCCR mageuzi he is doing fine with chadema..
5....
6....

Ninavyomjua Prof.Baregu,

1 He has strong character of leadership, good academician in politics and political science.
2 Known figure, respected person in and out of Tanzania anaipenda nchi yake ndio maana alisema badala ya kwenda kutafuta kazi nje atastaafu anafundisha Tanzania.
3 Open minded ana uwezo mkubwa tu wa ku-analyse mambo
4 he is trustworthy known to live with people hana majivuno hajikuzi na hana makuu, honestly and integrity si mtu wa kupenda kujilimbikizia mali.
5 prof. ni mtu wa vitendo walks the talks huwa anatenda anachokihubiri
6 he is confident in leadership role huwa anakiamini anachokisema au anachokifundisha
7 tolerant of ambiguity and remains calm and cool head tumeona kwenye sakata lake hili la kufukuzwa wala hababaiki ni kwamba anajua anachokifanya.

for that I know prof. Baregu I think he will make a good president

All these are certainly a good points, japo kuna zingine hatujaprove bado. Vipi kuhusu kuondolewa chuo kikuu ni failure ya nani? Baregu, viongozi wa chuo au serikali? na je alijua kuwa kuna siku atasimamishwa? kama alijua alifanya nini? kama hakujua je hakuona sign yoyote ya kumwonyesha kuwa hilo jambo litatokea?
 
Baregu must first know how to live without a job, like most Tanzanians live!
Ile ruzuku amegewe na Chadema,sooner or later you will see sparks flying around!!

Sidhani kama Prof. Baregu anashida na ajira ya chuo kikuu chetu. Please understand the move, is beyond monthly salary.
 
Back
Top Bottom