Shibuda apania kugombea dhidi ya JK CCM, ajitoa ghafla

aaah Shibuda weeeeeeeeeeeeee.Chukua form ndugu yangu.JK anapaswa kuwa one term president ...kwa jinsi nilivochefuliwa na serikali ya JK hata kama huna sifa ntakupigia kura tu ili mradi JK asiwe rais
 
Kama akina Dr. Salim, Prof. Mwandosya, Dr. Magufuli, Idd Simba, Hans Kitine na wote waliogombea 2005 wamenywea it is time for 'Rajolina' to rise. Nani aliwahi kufikiria kuwa DJ Rajo angekuja kuwa Rais? tena akiwa na umri mdogo kuliko unaoruhusiwa na katiba ya nchi yao. Go Shibuda. Ni afadhali Rais akawa Shibuda kuliko huyu Muungwana.
..Hili nalo neno!
 
Kuna watu wanaogopa kujitokeza kusema ukweli juu ya mpasuko na makundi katika CCM. sasa kama kweli Shibuda atamvaa kikwete basi kura zao zitasema mambo mengi sana...tena sana. Tena wale walioasi kambi ndo fursa hii ya kulipa kisasa kwa MDAU wao. hehehehe ama kweli picha la kihindi linakaribia kuanza...go shibuda go man, "The strongest man is the one who stand alone and never afraid of MANENO YA BARAZANI"
 
hivi mnajua shibuda alikuwa anafanya kazi gani na mpaka sasa hivi bado anaifanya? wako wengi kama yeye.....

Tumwagie kaka , maana ni muda mzuri wa kumfahamu huyu mtu, na toa maoni yako unamvyomfahamu.

Maoni yangu we need people like Shibuda ndani ya CCM.

Jamaa anaonekana kama Lowassa fulani... I mean anaweza kuchangamsha nchi atleast, mambo yaende,but we do need to know him deeply, tusijezalisha akina Idd Amin,

But I do admire his courage , really I do.
 
Tanzania had neveer had a president better than Kikwete. it only that the katiba is restrictive we should have hime for the 3rd term. amalizie malengo yake. angalia kesi za mafisadi, kilimo kwanza nk

i thinkletz be fair the guy anajitahidi
 
Mkuu Waberoya,

Mheshimiwa Shibuda aliwahi kufanyakazi General Tyre miaka ya nyuma sales dept technical jamaa ambao walikuwa nae kipindi hicho wamenithibitishia bila shaka yoyote kwamba ni mtu wa system [usalama wa taifa].

Kwa maoni yangu Shibuda anazuga au ametumwa kuchangamsha jukwaa hana lolote labda kama mtaniambia siku hizi hawa jamaa wa system wameacha kuwa watiifu kwa maboss wao.
 
Shibuda for president...I Love this man! Anza kurusha makombora dhidi ya Kikwete tena yako mengi sana na hata ukitaka msaada wa makombora zaidi wewe sema tu wanaJF tulio wengi tutakusaidia. Tena usisitizize kuwe na debate at least mbili kabla wana CCM hawajaamua kumchagua nani awakilishe chama chao na zionyeshwe live kwenye TV hata akichomoa wewe hudhuria tu na kumpiga madongo zaidi.
 
Shibuda anajifurahisha tuu. Wacha aendelee kwani hakuna kitu kizuri kama day dreaming. Hivi rais wa nchi hii awe Shibuda Tehe tehe tehe

Acha hizo! kwani hatimizi sifa za kuwa Rais?
 
Tanzania had neveer had a president better than Kikwete. it only that the katiba is restrictive we should have hime for the 3rd term. amalizie malengo yake. angalia kesi za mafisadi, kilimo kwanza nk

i thinkletz be fair the guy anajitahidi

Ama kweli siye ni Wadanganyika! Kesi za mafisadi zinapigwa kalenda kila siku. Kilimo kwanza au "mafisadi kwanza" imesimama kutokana na ugomvi wa mafisadi Manji na Jeetu kuhusu mkataba wa kuingiza matrekta toka India na bado kuna Wadanganyika wanaona kesi za mafisadi na kilimo kwanza aka Mafisadi Kwanza ni plus kwa Kikwete! Kazi kweli kweli!
 
Gazeti lililoandika hii habari lifungiwe kwa siku 90 kwa kutumia kichwa cha habari chenye lugha kali za uchonganishi, tena linataka kumchonganisha Raisi na mwanachama ambaye tu anataka kutumia uhuru wake uliopo kikatiba.
 
Dunia ni uwanja wa fujo SHIBUDA komaa uingie kwenye kumbukumbu watu wakujue ndani na nje ya Tanzania.
 
Mkuu Waberoya,

Mheshimiwa Shibuda aliwahi kufanyakazi General Tyre miaka ya nyuma sales dept technical jamaa ambao walikuwa nae kipindi hicho wamenithibitishia bila shaka yoyote kwamba ni mtu wa system [usalama wa taifa].

Kwa maoni yangu Shibuda anazuga au ametumwa kuchangamsha jukwaa hana lolote labda kama mtaniambia siku hizi hawa jamaa wa system wameacha kuwa watiifu kwa maboss wao.

Asante naomba darasa zaidi, kwanza najua ni vigumu ku-prove kuwa jamaa ni usalama wa taifa kweli, unajua bongo tena. Let for now assume that ni usalama wa taifa.

Je usalama wa taifa hawaruhusiwi kugombea uongozi? je ni sheria ya kazi yao au, just unwritten rule.

Pili. mpaka leo hata Mrema wanasema alikuwa usalama wa taifa. lakini kwa yoyote aliyekuwa kwenye uchaguzi wa 1995, sidhani na wala sitaamini kuwa Mrema ni uslama wa taifa, na kama ni usalama wa taifa basi hawana sheria inayomzuia mmoja wao kugombea nafasi anayoitaka! siamini kuwa Mrema 1995 yalikuwa maigizo that was serious election ever!

Fafanua hiyo "watiifu kwa mabosi wao" au kwa sheria zao.

Ninaamini, (sina prove) UWT hawana hizo sheria kwani UWT ulikuwepo kabla ya vyama vingi, na kinachoendelea ni labda ushauri wa mambosi, kama bosi ni mtu wa JK basi hatataka mmoja apingane na JK. Maans ishu ya Shibuda ni serious sana nadani ya CCM , utani utani huu kama ni kweli jamaa anaweza kupita, akishinda watasemaje? kuwa alikuwa anatania!! hajaanza leo Shibuda gata 2005 he did the same thing

Naomba shule zaidi kwa yoyote.
 
Mkuu Waberoya,

Mheshimiwa Shibuda aliwahi kufanyakazi General Tyre miaka ya nyuma sales dept technical jamaa ambao walikuwa nae kipindi hicho wamenithibitishia bila shaka yoyote kwamba ni mtu wa system [usalama wa taifa].

Kwa maoni yangu Shibuda anazuga au ametumwa kuchangamsha jukwaa hana lolote labda kama mtaniambia siku hizi hawa jamaa wa system wameacha kuwa watiifu kwa maboss wao.

Mkuu,
kuwa ndani ya system si kwamba unakatazwa kuingia ikulu. Kumbuka 2005 kulikuwa na wagombeaji wengi toka CCM na wote ni usalama wa Taifa.
Isitoshe kwa sasa mambo yanavyokwenda ndani ya Tanzania ni kwamba nchi haina mwenyewe. Kila mtu anaweza kusema ama kufanya atakavyo.
Sijashangaa kabisa kwa huyu muheshimiwa kuja na ndoto yake ya kuingia Ikulu.
Lakini kwa kuwafananisha JK VS JC ni wazi kuwa JC atakuwa Raisi mzuri 100 times JK.
 
JC you meant John Shibuda??? (JS then), if so I do agree with you, watu wenye misimamo ya kujaribu huwa wanakuwa viongozi wazuri. halafu hiyo 100 times siyo kweli ni 100 million times
 
Asante mkuu nilikuwa namaanisha JS na wala si JC. Ukweli haufichiki JS anaweza kuwa Raisi mzuri kuliko JK hilo halina ubishi hata kidogo.
 
Katika kipindi cha tuongee cha Star TV asubuhi leo, Mhe Augustine Lyatonga Mrema amesema Rais Amani Karume anafaa kuendelea kuwa Rais wa zanzibar katika kipindi cha awamu ya tatu, licha ya ukomo wa kikatiba wa awamu mbili, akidai kwa kufanya hivyo atalinda maridhiano - yake na Seif Sharif Hamad Katibu mkuu wa CUF ambayo anaamini ni msingi mkubwa wa kurejea kwa amani na maelewano Zanzibar.

Anadai muda uliobaki kati ya sasa na oktoba kwenye uchaguzi mkuu hautoshi kutekeleza maridhiano kikamilifu na kama atakuja mwingine maridhiano yanaweza yasiendelee na zanzibar watareja kwenye mpasuko.

Pia anataka vyama vya siasa CCM na CUF vifutwe huko Zanzibar kwa kuwa hivyo ndivyo msingi wa machafuko zanzibar. Pia anataka Serikali ya Mseto iwepo Zanzibar kwa kuwa siasa ya wengi wape haiwezekaniki zanzibar.

Na anasema kugombea Urais ni Biashara kichaa kwake, na anasema Mwl Nyerere alimshauri kugombea ubunge, akapuuza na kugombea Urais, ikala kwake, na asiyesikia la mkuu, huvunjika mguu, na kwamba sasa anaamua kwenda kugombea Ubunge Vunjo, kwa kuwa Hayati Baba wa Taifa ni Muasisi wa CCM basi wana CCm wanapaswa kumuunga mkono.
 
mimi sikusikiliza hicho kipindi, lakini kama haya ni ya kweli, basi mzee ajitahidi kukutana na mheshimiwa rais amuombe amuandikie ka-note aende kuonana na madaktari kule alikopimwa akili!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom