shetani na Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

shetani na Mungu

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Raia Fulani, Jul 21, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  hapo Tanga kuna shamba moja la minazi lililopakana na usharika mmoja ambao una sehemu ya makaburi yaliyozungushiwa uzio na kuwekewa "mfano wa geti". getini yupo mlinzi mmoja mzee mchovu hivi akilinda watu kutovunja misalaba. usiku mmoja vibaka wawili wakaenda kwenye hilo shamba kuiba nazi. walipoangua za kutosha wakajaza kwenye gunia moja na fasta wakalikokota kuelekea kule makaburini. walijua mlinzi wa pale ni mchovu tu, wakavuka geti na nazi mbili zikaanguka pale. wakasikia mtu akikoroma usingizini hapo jirani. kwa hofu wakaziacha na kuzama ndani karibu kiasi na getini wakaanza kugawana nazi kila mtu na gunia lake. "hii yangu hii yako, hii yangu hii yako..." mlinzi akashtuka usingizini akasikia wakigawana ila asijue nini kinagawanywa. kwa hofu akatoka hadi nyumbani kwa mchungaji ambapo si mbali na kumweleza. mchungaji akawaza na kumwambia, "Ni mungu na shetani wanagawana roho. twende tukasikilize vizuri" hao hadi pale na kila mmoja akakaa upande wake wa geti. wakasikia wanavyogawana hadi wakamaliza, kisha mmoja wao akasema, "bado! kuna zile mbili pale getini." mlinzi kusikia vile akazirai pale pale na mchungaji haikujulikana kapitia wapi
   
 2. GP

  GP JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  teh teh , dah ebwanaeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee hapo lazima uzimie, au utoke duki nene sana!!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Peter Tosh alipata kusema(namnukuu):
  EVERYONE WANTS TO GO TO HEAVEN, BUT NONE WANTS DIE!
  Ndo mambo hayo ya Mchungaji na Mlinzi.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kufa kubaya wajameni ila tufanyeje. Tungejua tutafikia wapi isingekuwa ishu
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mziwanda wewe ulikuwa umejificha wapi kipindi hicho.... lol! Hii kali mzee.
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Duh.. hii kali! Sijui wangegawanaje hizo nazi ('roho') za getini.. pasupasu au zote anachukua Mungu?
   
 7. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Haya bwana.
  Hii yangu, hii yangu.
   
 8. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  mambo ya satelite mkuu!
   
 9. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2009
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu Mziwanda naomba usijiite mtu wa watu huku uswahilini mwanamme akiitwa mtu wa watu ina maana ingine kabisa.
   
 10. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Yesu na Maria! Itabidi basi ni adapt na mazingira
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Jul 26, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mmmmh! hataaa... hapa kama wewe si yule mzee mlinzi, basi wewe ndiye yule mchungaji...!

  Bisha kama ndio kweli!....!
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  duh! Ningekuwa miongoni mwao ningesimulia vingine mkuu. Nilikuwa shuhuda tu
   
Loading...