Shetani: Adui rafiki asiye na kinyongo

Mada yako hii

Mleta mada umetoa fundisho zuri, tatizo lako umeijumuisha mada yako kama vile watu wote ni vuguvugu, yaani wanamfuata Mungu kidogo na Shetani kidogo
Ungesema "baadhi yetu"
Siyo kila mtu yupo kwenye hali hiyo,
Wako watu ni wafuasi wa shetani na hawamtaki Mungu kabisa na wana imani za Kishetani

Wako pia hao vuguvugu

Tena wapo Watu Wanafanya mapenzi ya Mungu na hawana nia ovu moyoni mwao.

Mleta mada umeonyesha kama watu woote ni wanafiki jambo ambalo sio kweli.

Nadhani unawajua mashoga, magaidi, ma satanist nk.

Pia unawajua wanafiki wa dini

Tena unawajua manabii, mitume, nk.

Sema baadhi ya binadamu ni ndumilakuwili na sio watu wote.
 
Ni kwa Neematu, na sio kitu cha kujigamba kuwa mimi ninayafanya yote yanipasayo kuyafanya. Mara nyingine tunaanguka pasipo sisi wenyewe kujua
 
Asante kwa angalizo nimekupata vema... Nia ilikuwa hiyo japo kwenye andishi sikuiweka
 
The times when you want to grant satisfaction to self desires like adultery thieving lying etc
So does that mean evil exist in human nature itself.That all these years we are fighting our nature? And 'compromising with the devil' is nothing but finding justification in whatever bad we do.later,realizing what we have done we blame it to, no,not ourselves,to 'Satan'.
 

Beauty is the nature within self[emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji779] [emoji779] [emoji779]
 
Samahani kukuuliza hili mbingunikwetu,Ila tokea umekuwa kiumbe kipya haujafanya dhambi?

Hichi ndicho alichokiongea mshana,uokoke usiokoke dhambi wote tunafanya.Tofauti iliyopo,aliyeokoka atakiri dhambi na kuomba msamaha na nakuendelea mbele.Na ambaye hajaokoka au mdhambi yeye sanasana amekata tamaa kuomba msamaha Maana anaona dhambi anarudia kufanya Basi bora yawe maisha yake.

Kwa maana nyingine kufanya dhambi ndio huko kidogo kwa shetani kidogo kwa Mungu.Na ndio maisha ya mwanadamu.Na ndio vita yetu ya kila siku.Kuna siku tunashinda na kuna siku tunashindwa.Hakuna aliye msafi.
 
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji115] [emoji817] [emoji779] [emoji779] [emoji779]
Hizi falme mbili tunaishi nazo kila sekunde ya maisha yetu
 
La muhimu hapa kwanza ni kuijua KWELI na kuyaongeza maarifa, hapo ndiko utakapojua wewe ni wa moto ama baridi au vuguvugu, kuna watu tutaangamia kwa kutoyajua tu maarifa, na kweli.

Maarifa juu ya kweli kama huna, utatenda kinyume na kweli na hivyo kupotea pasi kujijua.
 
Mmmh [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji115] [emoji115] [emoji115]
 
Sasa dhumuni lako ndugu ni nini haswa? Unataka shetani aonekane ni mzury au vp maana kiumbe kilicholaaniwa basi hata chembe ya uzury hawezi kua nayo hata kuweza kumpa thamani sawa na kibawa cha mbu!! Hakuna namna yyte yakumsafisha kiumbe kilicholaaniwa hata ufanyaje na sidhani kama utakua sawa kujaribu hata chembe kuubadilisha ukweli kua sawa!! Hayo ndo mani yangu!!!.
 
Tatizo lako ndugu mshana unapenda kuamini kile ulichokiamini pasipo kutaka kuaminisha wale unaotaka kuwaamisha kua hizi ni fact za uhakika.sawa watu huamini kua shetani ni dubwana lakutisha sasa ww unatoa wapi prouv kua shetani sio dubwana lakutisha maana kitu kilicholaaniwa maana yake matendo yake makazi yake mpaka maumbo yake na vizazi vyake vimelaaniwa na laana kikawaida mfano mzazi akimpa mtoto wake radhi au laana basi unaona kabisa athary kwa yule kiumbe kinavyokua anakua atachanganyikiwa mwisho anakua chizi kabisaa wa majalalali sasa sijui prouv zako unazitoleaga wapi ndugu!!!.
 
[emoji144] [emoji144] [emoji144] tundu007 nilichogundua kuna mengi bado huyafahamu vema ama una uelewa mdogo ndani yake
Kwenye hii mada naona kabisa umetoka nje ya mada na kujichanganya kabisa... Nafahamu hatuwezi kufanana mitazamo lakini kwenye kila hoja lazima tu establish hoja zenye mantiki na kujadilika
Kumbuka we are part n parcel of great thinkers
 
Uzury wako unajua kuyapangilia maneno kwahilo nakusifu!! Sema jambo lolote kuhusu kiumbe kilicho laaniwa hakiwezi kua kizury abdan asilaan!hata tukipambe vp!! Amfwatae shetani na yy atakwenda nae!na amfwatae muumba nae atakwenda kwa muumba!! Hakuna mjadala!
 
Ukisoma tena kwa makini nilichoandika utaona namzungumzia shetani katika muktadha gani
Ngoja nikupe mfano rahisi sana
Siku hizi kumiliki smartphone yenye memory kubwa ni kitu cha kawaida
Sasa kwenye hiyo cm yenye memory kumejazwa ya shetani na ya Kimungu.. Humo humo tumedownload misahafu humo huko tumeweka video chafu, humohumo kuna nyimbo za kidini na za kidunia
Humo humo kuna simu na msg za michepuko.... Lakini ni simu hii hii unaingia nayo ibadani na huiachi kila uendapo
Sasa wakati ukijenga picha ya shetani dubwana kubwa linalotisha sana lenye mapembe na katili unasahau kabisa kwamba umemhifadhi kwa uzuri mno ndani ya simu yako
 
Hahaaa aiseee halaf unaenda na kutoa sadaka kanisani na misaada kibao kwa yatima na wasiojiweza!
Hapo kuna mawili
Utabarikiwa kwa ule moyo wa kutoa
Kisha utahukumiwa kwa kile ulichokitoa... Hili huja baadae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…