HahahahhTell me who is the devil in your own words
Kiboko yake ni YESU,,jina lipitalo majina yote ,akisikia jina YESU,anakwama,,,Binadamu ni kiumbe hai wa namna ya pekee kabisa anayeweza kusema kwa nguvu zote kuwa hii ni nyeupe lakini moyoni mwake akiwa haamini hivyo au akiwa na ukweli tofauti.
Wote tunamjua sana shetani dubwana linalotisha na hata tunapomchora mawazoni na hata kwenye makaratasi ni kitu cha kuogofya kutisha na kuogopwa lakini huu ni unafiki mkubwa wa kiumbe mwanadamu kwakuwa shetani ni nzuri shetani anavutia shetani anaheshimiwa shetani ni maarufu shetani anasujudiwa mno.
Na kwakuwa shetani anayatambua yote haya ndio maana hana pressure na wewe anakuacha ufanye unafiki wako anajua kwa hakika kwake utarejea likitokea jambo tusilolipenda kabisa toka rohoni mwetu huwa na kwa maslahi yetu ambayo saa nyingine ni ya kujikweza humbomoa shetani hasa na kupambana naye kwa nguvu zote! Tukimseta kumlaani kwa kadiri ya pumzi zetu yeye hukaa kimya na kutabasamu.
Lakini likitokea jambo ambalo tunalipenda lakini ni naya hasa la kutosheleza tamaa na matamanio ya kimwili shetani huwa rafiki mwema na tuko tayari kufanya naye colabo bila kujua kuwa ni maagano hapa hupambani tena na shetani bali mnacompromise.Kichefuchefu cha undumilakuwili wa mwanadamu.
Unaingia nyumba ya ibada kwa imani yako ukiwa na matatizo lukuki Hapa unaenda kuomba msaada wa Mola wako ukifanikiwa unaenda kufanya uchafu huku ukiomba mambo yasije kuharibika... Mungu anakutizamana tu huku shetani akitabasamu kwa pozi.
Mwanadamu ni kiumbe dhaifu asiye na msimamo thabiti atumikiaye nguvu mbili kwa mara moja na wakati wote kwa shetani kidogo kwa Mungu kidogo na hayo ndio maisha yetu mpaka tunakufa na unafiki wote huku tukimpa shetani ushindi mkubwa.
Duu what a deep n nice reply..... Asantesana umenifurahisha mno hapo kwenye wizara za kishetani ngono dili bar na uongo... Yani ukiangalia ni halisi kabisaaaaKumjua na kumtumikia, inategemea unamfuata SHETANI katika Idara ama Wizara ipi....
Shetani nao wana Mamlaka ama tuite Serikali kama tulivyo sisi binaadam..
Hivyo wana mifumo katika utawala wao, wakiwa na Raisi..Mawaziri..Wabunge na zaidi ya tawala hadi ngazi ya chini zenye ujuzi..utii..na sifa nyingi za kiongozi zaidi ya zile za KIDUNIA...
Binaadam wa sasa tumekuwa ndumilakuwili, tukiuma na kupuliza..tukisema kwa kupayuka na kunong'ona..tukicheka na kununa .. kutii na kukaidi Katika muda huohuo...!!
Kwa maagano aliyoweka SHETANI kwa MUNGU ambaye ndiye tunaemuabudu sisi WANAADAMU.
Tunaambiwa kutoka katika Vitabu vya Dini kuwa.. alimuomba Mungu as integer exe ili atimize lengo lake..ampotoshe Mwanaadamu ili aweze kuchomwa nae pamoja katika MOTO wa milele...
Kwa ujinga na udhaifu wa BINAADAMU walio wengi, leo hii wameshindwa/tumeshindwa kujua tunawajibika kwa MUNGU ama SHETANI anaeongoza WIZARA ama IDARA ipi...!!?
Tunatii kwa SHETANI waziri wa NGONO..ukitoka hapo unapokea maagizo kutoka kwa SHETANI idara ya PROPAGANDA..ukirudi nyumbani kwa mwenza wako wewe ni UONGO kwa kwenda mbele...
Unaamka asubuhi ukijiandaa kwenda kutafuta RIDHIKI yako, unapokea maagizo toka law SHETANI waziri wa Uporaji na Tamaa...matokeo ukifika kazini unawaza kupiga DILI....
Ukitoka mzigoni unapokea maagizo kutoka kwa SHETANI Mbunge wa Jimbo la POMBE..
unajikuta hufiki nyumbani mpaka kwanza upate moja moto na mchemsho...
Kwa kuyumba kwetu BINAADAMU na kukosa MSIMAMO ndio maana tunabaki kuwa WATUMWA na MAWAKALA wa SHETANI kila leo na kila sekunde.
Tumemsaliti MUNGU na kusahau lengo KUU la kuumbwa kwetu..
Tumejenga URAFIKI ambao ni kama UDUGU na kiumbe huyu ADUI.
Tumefikia hatima ya kuamini kuwa kila mwenye mafanikio ni lazima apitie MAAGANO na SHETANI waziri wa FEDHA na MALIHALISI....
Tumefikia hitimisho na kuamini hakuna MLINZI wa NCHI na VILIVYOMO tukikabidhi IMANI...HATIMA na MATARAJIO ya kesho katika ULIMWENGU huu kwa SHETANI waziri wa ULINZI..
Naunga mkono HOJA kaka Mshana..
Wewe ni GREAT THINKER....

Nadhan MUNGU hakumuumba shetaniUmemaliza kila kitu. Ndo maana unakuta mtu anajifanya mcha Mungu kweli halafu unakuta eti kashikwa ugoni. Sasa mtu unajiuliza, what happened? Ni kwa sababu hii tunashauriwa sana kuwa ni hatari mno kuegemeza imani zetu kwa binadamu wenzetu hata kama ni watabiri wazuri kama TB Joshua, "wafufua watu" Kama Gwajima n.k.
Halafu kuna jambo Mshana Jr huwa linanikera kwenye hii ishu ya Mungu na Shetani. Kwenye Biblia inaonekana kwamba shetani na Mungu huwa wanakutana na hata kupiga stori mf. Ishu ya shetani na Ayubu. Hili linawezekanaje wakati tunaambiwa kwamba Mungu ni Mtakatifu mno kiasi kwamba kitu kichafu hakiwezi hata kumkaribia? Na kwa vile Mungu wetu Anajua kila kitu, kwa nini Ali-go ahead anyway na kumuumba shetani? Maswali haya huwa yananitatanisha sana na huishia tu kujipa moyo kwamba kwa akili hii ndogo ya kibinadamu hatuwezi kumwelewa Mungu katika ukamilifu wake. May be tutaelewa zaid tukifika mbinguni! Wewe unaonaje?
Vitu vyote vimeumbwa na Mungu. Na Mungu Anajua kila kitu. Japo hapo mwanzo shetani alikuwa ni malaika mkuu huko Mbinguni bila shaka Mungu Alijua kuwa huko mbele ya safari ataasi na kutuletea dhambi ambayo hatimaye nayo imetuletea kifo, magonjwa na matatizo lukuki. Kwa hiyo (1) Kama Mungu Aliumba kila kitu na (2) Mungu Anajua kila kitu basi tunalazimika kuhitimisha kuwa Mungu Alimuumba shetani hata kama hapo mwanzo alikuwa Mtakatifu huko mbinguni!Nadhan MUNGU hakumuumba shetani
Hapa mimi huwa namchora tofauti sana Shetani, kwanza angekuwa ni raia wa hapa duniani katika maisha haya angekuwa ni shujaa, mwenye upendo uliopitiliza kwa wanadamu au anaowatawala, ni mwenye kupenda haki na usawa. Sidhani kama Sir God na Lucifer wana bifu kuuubwaa sana, wangeshindana tu ideologies za kutawala, shetani akiamini njia au ideologies zake ni bora zaidi.
Kwahiyo kwangu shetani si mwenye malice, ana mapungufu ktk utambuzi kwakuwa ni kiumbe, hazijui siri kuu za uumbaji wa Mungu, brueprints. Angalia anavyohangaika kuyatatua matatizo ya malimwengu ktk utawala wake. Tumeongezeka, kuku kwa formula ya Mungu akue kwa miezi sita ndo aliwe, hapa atakuwa ametimiza formula za kiuumbaji wa vyote, shetani akatafute shortcut, miezi miwili tu kuku bonge, lakini kwakuwa hazijui formula za kwanini alitakiwa ajue kwa miezi 6, wake ukimla kwakuwa wamekwenda kinyume na ASILI, haitakuwa salama, sio adhabu bali formula zitagongana. Mifano ni mingi.
Vitu vyote vimeumbwa na Mungu. Na Mungu Anajua kila kitu. Japo hapo mwanzo shetani alikuwa ni malaika mkuu huko Mbinguni bila shaka Mungu Alijua kuwa huko mbele ya safari ataasi na kutuletea dhambi ambayo hatimaye nayo imetuletea kifo, magonjwa na matatizo lukuki. Kwa hiyo (1) Kama Mungu Aliumba kila kitu na (2) Mungu Anajua kila kitu basi tunalazimika kuhitimisha kuwa Mungu Alimuumba shetani hata kama hapo mwanzo alikuwa Mtakatifu huko mbinguni!
Kwa logic na akili ya kibinadamu maswali haya yanatatanisha sana. Lakini kwa Mungu naamini yanaeleweka na mipango yake ni mikamilifu. Imani!
I need a copy
Fantasy, acha kabisa kujilisha upepo. Are you a living saint?"Kwa shatani kidogo kwa Mungu kidogo na hayo ndiyo maisha yetu' Hapo Mshana Jr siyo kweli! Usiseme hayo ndiyo maisha yetu, sema hayo ndiyo maisha yako! Shetani amekudanganya na umedanganyika na kujipa moyo kuwa watu wrote wanafanya machafu ya shetani!
Japo wapo watu kama wewe wenye urafiki na matendo machafu ya kishetani, lakini wapo watu wengine wengi tu nikiwamo Mimi ambao tulifika mahali tukasema hapana kwa shetani na ndiyo kwa Mungu. Hii inatokea ukiamua kumwamini Yesu na kutubu dhambi zako. Ukifanya hivyo Mungu anakusamehe dhambi zako halafu anakuzaa Mara ya pili na unakuwa kiumbe kipya! Ukifanya hivyo unakuwa umeokoka!
Anachokisema mshana kinamhusu ambaye hajaokoka lakini akadai anamchukia shetani, hilo haliwezekani! Nje ya wokovu MTU hana uwezo wa kumpinga wala kumchukia shetani kwa dhati maana anakuwa bado ni mtumwa shetani.
Ushauri wangu kwa Mshana na wengine wote wenye mawazo kama yake ni kuwa:
1. Kama wanahitaji kwa dhati kuondokana na hali ya unafiki wa MTU kupenda mambo machafu ya kishetani huku akijifanya hampendi shetani ni kwamba wamwamini Yesu na kumkaribisha katika mioyo yao kama Bwana na mwokozi wa maisha yao. Hiyo inafanyika kwa kutubu dhambi zao na kuomba sala ya toba.
2. Sala ya toba wanayopaswa kuomba ni hii: "Bwana Yesu naja kwako, Mimi ni mwenye dhambi, ninaomba unisamehe dhambi zangu zote, ninazozikumbuka na ambazo sizikumbuki. Karibu Yesu katika moyo wangu uwe Bwana na Mwokozi wangu. Asante Yesu kwa kunisamehe na kuniokoa. Ninakushukuru Mungu katika jina la Yesu-Amina!
3. Kama umeomba sala hiyo hapo juu kwa moyo wa dhati umeokoka! Kw sasa una uwezo wa kumpinga shetani na akakimbia! Kwa sasa unaweza kuziambia tamaa za mwili kuwa wewe ni mtakatifu na zikakaa kimya! Sauti yako sasa INA mamlaka! Unauwezo WS kuiambia dhambi hapana na ikatii! Nami nakuombea sala ifuatayo: "Bwana Yesu katika jina lako takatifu naomba umpokee ndugu huyu ambaye ametubu kwa dhati mbele yako. Mwoshe kwa damu yako ya thamani. Umlinde na yule mwovu na umpe ushindi juu ya dhambi. MPE furaha na amani katika moyo wake, na umlinde na umponye dhidi ya magonjwa ypte. Nsomba Haya katika jina la Yesu -Amina.
4. Tafuta watu wsliookoka wanaoamini katika utakatifu na ushindi juu ya dhambi watakusaidia zaidi.