Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,076
- 859,172
Binadamu ni kiumbe hai wa namna ya pekee kabisa anayeweza kusema kwa nguvu zote kuwa hii ni nyeupe lakini moyoni mwake akiwa haamini hivyo au akiwa na ukweli tofauti.
Wote tunamjua sana shetani dubwana linalotisha na hata tunapomchora mawazoni na hata kwenye makaratasi ni kitu cha kuogofya kutisha na kuogopwa lakini huu ni unafiki mkubwa wa kiumbe mwanadamu kwakuwa shetani ni nzuri shetani anavutia shetani anaheshimiwa shetani ni maarufu shetani anasujudiwa mno.
Na kwakuwa shetani anayatambua yote haya ndio maana hana pressure na wewe anakuacha ufanye unafiki wako anajua kwa hakika kwake utarejea likitokea jambo tusilolipenda kabisa toka rohoni mwetu huwa na kwa maslahi yetu ambayo saa nyingine ni ya kujikweza humbomoa shetani hasa na kupambana naye kwa nguvu zote! Tukimseta kumlaani kwa kadiri ya pumzi zetu yeye hukaa kimya na kutabasamu.
Lakini likitokea jambo ambalo tunalipenda lakini ni naya hasa la kutosheleza tamaa na matamanio ya kimwili shetani huwa rafiki mwema na tuko tayari kufanya naye colabo bila kujua kuwa ni maagano hapa hupambani tena na shetani bali mnacompromise.Kichefuchefu cha undumilakuwili wa mwanadamu.
Unaingia nyumba ya ibada kwa imani yako ukiwa na matatizo lukuki Hapa unaenda kuomba msaada wa Mola wako ukifanikiwa unaenda kufanya uchafu huku ukiomba mambo yasije kuharibika... Mungu anakutizamana tu huku shetani akitabasamu kwa pozi.
Mwanadamu ni kiumbe dhaifu asiye na msimamo thabiti atumikiaye nguvu mbili kwa mara moja na wakati wote kwa shetani kidogo kwa Mungu kidogo na hayo ndio maisha yetu mpaka tunakufa na unafiki wote huku tukimpa shetani ushindi mkubwa.