Shetani: Adui rafiki asiye na kinyongo

Kumjua na kumtumikia, inategemea unamfuata SHETANI katika Idara ama Wizara ipi....

Shetani nao wana Mamlaka ama tuite Serikali kama tulivyo sisi binaadam..

Hivyo wana mifumo katika utawala wao, wakiwa na Raisi..Mawaziri..Wabunge na zaidi ya tawala hadi ngazi ya chini zenye ujuzi..utii..na sifa nyingi za kiongozi zaidi ya zile za KIDUNIA...

Binaadam wa sasa tumekuwa ndumilakuwili, tukiuma na kupuliza..tukisema kwa kupayuka na kunong'ona..tukicheka na kununa .. kutii na kukaidi Katika muda huohuo...!!

Kwa maagano aliyoweka SHETANI kwa MUNGU ambaye ndiye tunaemuabudu sisi WANAADAMU.

Tunaambiwa kutoka katika Vitabu vya Dini kuwa.. alimuomba Mungu as integer exe ili atimize lengo lake..ampotoshe Mwanaadamu ili aweze kuchomwa nae pamoja katika MOTO wa milele...

Kwa ujinga na udhaifu wa BINAADAMU walio wengi, leo hii wameshindwa/tumeshindwa kujua tunawajibika kwa MUNGU ama SHETANI anaeongoza WIZARA ama IDARA ipi...!!?

Tunatii kwa SHETANI waziri wa NGONO..ukitoka hapo unapokea maagizo kutoka kwa SHETANI idara ya PROPAGANDA..ukirudi nyumbani kwa mwenza wako wewe ni UONGO kwa kwenda mbele...

Unaamka asubuhi ukijiandaa kwenda kutafuta RIDHIKI yako, unapokea maagizo toka law SHETANI waziri wa Uporaji na Tamaa...matokeo ukifika kazini unawaza kupiga DILI....

Ukitoka mzigoni unapokea maagizo kutoka kwa SHETANI Mbunge wa Jimbo la POMBE..
unajikuta hufiki nyumbani mpaka kwanza upate moja moto na mchemsho...

Kwa kuyumba kwetu BINAADAMU na kukosa MSIMAMO ndio maana tunabaki kuwa WATUMWA na MAWAKALA wa SHETANI kila leo na kila sekunde.

Tumemsaliti MUNGU na kusahau lengo KUU la kuumbwa kwetu..
Tumejenga URAFIKI ambao ni kama UDUGU na kiumbe huyu ADUI.

Tumefikia hatima ya kuamini kuwa kila mwenye mafanikio ni lazima apitie MAAGANO na SHETANI waziri wa FEDHA na MALIHALISI....

Tumefikia hitimisho na kuamini hakuna MLINZI wa NCHI na VILIVYOMO tukikabidhi IMANI...HATIMA na MATARAJIO ya kesho katika ULIMWENGU huu kwa SHETANI waziri wa ULINZI..

Naunga mkono HOJA kaka Mshana..

Wewe ni GREAT THINKER....
 
Kiboko yake ni YESU,,jina lipitalo majina yote ,akisikia jina YESU,anakwama,,,
 
Duu what a deep n nice reply..... Asantesana umenifurahisha mno hapo kwenye wizara za kishetani ngono dili bar na uongo... Yani ukiangalia ni halisi kabisaaaa
Kuna watu nawaona hapa kila mtu na wizara yake [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji124] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji779] [emoji779] [emoji779]
 
Nadhan MUNGU hakumuumba shetani
 
Hapa mimi huwa namchora tofauti sana Shetani, kwanza angekuwa ni raia wa hapa duniani katika maisha haya angekuwa ni shujaa, mwenye upendo uliopitiliza kwa wanadamu au anaowatawala, ni mwenye kupenda haki na usawa. Sidhani kama Sir God na Lucifer wana bifu kuuubwaa sana, wangeshindana tu ideologies za kutawala, shetani akiamini njia au ideologies zake ni bora zaidi.

Kwahiyo kwangu shetani si mwenye malice, ana mapungufu ktk utambuzi kwakuwa ni kiumbe, hazijui siri kuu za uumbaji wa Mungu, brueprints. Angalia anavyohangaika kuyatatua matatizo ya malimwengu ktk utawala wake. Tumeongezeka, kuku kwa formula ya Mungu akue kwa miezi sita ndo aliwe, hapa atakuwa ametimiza formula za kiuumbaji wa vyote, shetani akatafute shortcut, miezi miwili tu kuku bonge, lakini kwakuwa hazijui formula za kwanini alitakiwa ajue kwa miezi 6, wake ukimla kwakuwa wamekwenda kinyume na ASILI, haitakuwa salama, sio adhabu bali formula zitagongana. Mifano ni mingi.
 
Nadhan MUNGU hakumuumba shetani
Vitu vyote vimeumbwa na Mungu. Na Mungu Anajua kila kitu. Japo hapo mwanzo shetani alikuwa ni malaika mkuu huko Mbinguni bila shaka Mungu Alijua kuwa huko mbele ya safari ataasi na kutuletea dhambi ambayo hatimaye nayo imetuletea kifo, magonjwa na matatizo lukuki. Kwa hiyo (1) Kama Mungu Aliumba kila kitu na (2) Mungu Anajua kila kitu basi tunalazimika kuhitimisha kuwa Mungu Alimuumba shetani hata kama hapo mwanzo alikuwa Mtakatifu huko mbinguni!

Kwa logic na akili ya kibinadamu maswali haya yanatatanisha sana. Lakini kwa Mungu naamini yanaeleweka na mipango yake ni mikamilifu. Imani!
 

 
Fantasy, acha kabisa kujilisha upepo. Are you a living saint?
Our souls are timeless, and we're here to learn and become better souls. The existence of evil is inevitable.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…